Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 11 Machi 2014

Mbowe naye anaunga mkono Azimio kwa asilimia 100. Anamshukuru Pinda na Balozi Seif Ali Idd kwa kuongoza vema kamati ya mashauriano. Anawashukuru viongozi wa dini sheikh Jongo na askofu Mtetemela kwa kuyaondoa mapepo yaliyokuwa yanawaharibu. Pia amemshukuru mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kwa kuibua wazo la kusoma dua kabla ya kuanza kikao
 
Baada ya mjadala tutaonge zaidi na wewe pengine unataka kumifahamu vizuri njoo dodoma tuonane mkuu.
 
Sheikh Kundecha sasa anaongea. Anasema kuwa ukamilifu ni wa Mwenyezi Mungu. Kwamba hatarajii kuona ukamilifu kwenye kazi za mwanadamu. Hata hizi kanuni zina mapungufu na kuna mwanya wa kushughulikia mapungufu hayo
Majina ya wachangiaji ni yaleyale. Nyuma ya Mbowe yupo muasisi wa Mageuzi nchini, James Mapalala, hatajwi kabisa!
 
Mbowe anaendelea kwa kumshukuru viongozi wa dini kwa kusaidia kuleta hali ya utulivu bungeni.
Mkuu, pamoja sana. Hakika Mbowe ameongea maneno ya busara sana
 
Majina ya wachangiaji ni yaleyale. Nyuma ya Mbowe yupo muasisi wa Mageuzi nchini, James Mapalala, hatajwi kabisa!
Mkuu, ni kweli kabisa. Ila pengine ugeni mjengoni unawasumbua wabunge wengi wageni
 
Mh jusa ambaye alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kutunga kanuni naye anatoa neno kuhusu mchakato mzima wa kutunga kanuni na kuunga mkono azimio husika.
 
Kama utakua umewasikiliza kwa Umakini sana Lipumba na Mbowe,Ni dhahiri kua Kamati ya Maridhianao imekubaliana na Kura ya Siri.
 
Jusa anampongeza sana Lissu kwa mchango mkubwa alioutoa kwenye Kamati ya Kanuni
 
Kama utakua umewasikiliza kwa Umakini sana Lipumba na Mbowe,Ni dhahiri kua Kamati ya Maridhianao imekubaliana na Kura ya Siri.
Mkuu, kama wamekubaliana hivyo ni jambo jema kuliko kuendelea kusuguana kwa jambo dogo kama hili la kura.
 
Ismail Jusa anateuliwa na kificho kusema neno, anaanza kuongea..
 
Jusa anaeema kuwa maslahi ya Zanzibar na yatalindwa. Uwepo wa theluthi mbili kwa Zanzibar katika kufanya maamuzi ni ishara tosha kuwa Zanzibar inaheshimiwa
 
Mkuu, kama wamekubaliana hivyo ni jambo jema kuliko kuendelea kusuguana kwa jambo dogo kama hili la kura.
Ni kweli mkuu misuguano siyo mizuri make hujenga matabaka na hata kuacha makovu ya kudumu.
 
Mkuu hapa hakuna habari ya vyama tunatunga katiba ya watanzania mhona unataka tuanze kujadili vyama na siasa kama unataka siasa nenda kalenga na chalinze.
we mbona huungi mkono hoja uatachangia lini katika bunge hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…