Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 11 Machi 2014

Mkuu, kama wamekubaliana hivyo ni jambo jema kuliko kuendelea kusuguana kwa jambo dogo kama hili la kura.
mimi nahisi mkuu wa kaya atakuwa amewatuliza ccm hapo dodoma waachane na hizo propaganda za kura ya wazi
 
Askofu Amosi Mhagachi anachangia. Anasema kuwa ikiwa wabunge watasahau kazi nzuri ya waasisi wetu ni wazi kuwa tutapotea. Anasema kuwa sauti ya wengi ni sauti ya amungu. Anawataka wabunge kuunga mkono Azimio
 
Askofu nawaasa wajumbe kutenda yaliyomema wasipofanya hivyo wataadhibiwa hivyo ni vema kutenda mema hasa ambayo yanayompendeza mungu na watanzania kwa ujumla.
 
Askof Amos amesistiza kukubaliana na azimio la kanuni na anakaa
 

Naunga mkono hoja! Jana nilisema kama Simiyu Yetu ni mjumbe wa bunge hili ni aibu kwangu kuendelea kujiita Mtanzania. Ndugu Chabruma una uthibitisho mwingine zaidi ya maneno ya Simiyu Yetu? Ukithibitisha naanza harakati za kuusaka uraia wa nchi nyingine kuliko kutungiwa katiba na watu aina ya Simiyu Yetu. Ni bora kwenda hata Somaliland.
 
Last edited by a moderator:
mimi nahisi mkuu wa kaya atakuwa amewatuliza ccm hapo dodoma waachane na hizo propaganda za kura ya wazi
Mkuu, ni mawazo yako. Sina hakika na hilo ila yawezekana ukawa sahihi
 
Mkuu, sina hakika na hilo?
 
Mtikila ameanza visa....kwa nini hapewi nafasi?
 
Jusa anaeema kuwa maslahi ya Zanzibar na yatalindwa. Uwepo wa theluthi mbili kwa Zanzibar katika kufanya maamuzi ni ishara tosha kuwa Zanzibar inaheshimiwa

Mkuu Chabruma Nimeanzia kati sijaweza kupitia kila post, naomba kufahamu issue ya kura ya wazi au siri imeishia wapi?

 
Last edited by a moderator:
Mjumbe wa kamati mhe Jusa amemsifia sana mh Tundu Lisu kwa umahiri wake na uelewa mkubwa ktk sheria. Akiongea kwa niaba ya kamati amesema Mh Tundu Lisu amekuwa akitumia muda mwingi sana kusoma vitabu na sheria na si kusoma tu bali alitumia pia uzoefu na utundu wake wa kuzijua kanuni hadi kusaidia kupatikana kwa kanuni bora za kuliongoza bunge maalum.

Hongera sana jembe Tundu Lisu Watanzania tumeona kazi yako. Mungu akupe hekima na uelewa zaidi.

Source TBC
 
Mtikila anang'aka kwa kutopata nafasi ya kuzungumza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…