Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 11 Machi 2014

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 11 Machi 2014

vp,olesendeka na leo atamwaga chozi???? alianza yule sura mbaya kipindi cha mauaji ya arubino na sasa kafuata huyu morani,akitoka yeye nadhani itakuwa zamu ya jangili au mr dhaifu!
 
kura ya siri au ya wazi nashauri ipigiwe kura ya siri hapo suluhisho litapatikana
 
Kamati ya mashauriano imeshindwa kazi kwa nini Kifungu cha 37 na 38 kuhusu uamuzi wameacha wazi
Mkuu, binafsi siamini kama kamati ya mashauriano imeshindwa kazi. Unajua hili suala la katiba mpya ni suala la maridhiano na si kutaka kujionesha nani ni mshindi. Pia mashauriano hayawezi kufanyika kwa fast tracking kwani mwisho wa siku mnakuja kukimbiana. Ukumbuke kuwa hawa wanasiasa hawaaminiani hata kidogo.
 
Mkuu Chabruma, ubarikiwa sana!. Jee unamjua huyo mwenye hilo jina la Chabruma na alifanya nini?!.
Pasco
Nilitaka kulitumia hilo jina.Jinsi huyo shujaa Alivyotutendea Wangoni nilidhani sitolitendea haki! Je,analitendea?
 
kura ya siri au ya wazi nashauri ipigiwe kura ya siri hapo suluhisho litapatikana
Mkuu jambo hilo lilijitokeza jana. Mwalimu Ezekiel Oluoch alitoa mapendekezo hayo. Ila swali likaja kwa nini tutumie kura ya siri kuamua aina ya upigaji kura? Kwa ninimisiwe kura ya wazi kuamua aina ya upigaji kura? Ni kutokana na mazingira hayo ndipo uamuzi wa kamati ya mashauriano ulipoonekana una mantiki
 
Je,al shabaab au boko haram wangevamia hilo bunge na kuwateka hao wajumbe,utatoa chozi kuwalilia?
 
Mkuu, imekuwaje tena? Kwenye suala la Katiba, watanzania ni wamoja.

Ni kweli mkuu Watanzania tu Wamoja, ila kuna kundi la kishetani liitwalo ccm wana umoja wao japo wanangangania kuishi Tanzania
 
Naamini wabunge Leo watatii amri ya Pandu ya kuwahi ukumbini saa tatu Barabara....huku wakivalia nadhifu....naaam maaana Leo sio semina tena.
 
Hodi Hodi Wadau wote wa Mtandao wetu pendwa, mtandao nambari one Tanzania, mtandao usio na mafungamano yoyote, Mtandao wa Jamiiforums! Natumaini kuwa leo mmeamka salama bukheri wa afya njema. Wale wote ambao kwa bahati mbaya hali zao kiafya si nzuri basi tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wapate nafuu ili angalau wapate fursa ya kuchungulia humu juu ya yale yanayoendelea Bungeni Dodoma. Na kama kuna waliotangulia mbele za haki, basi tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie makazi mema huko.

Wadau, kwa siku ya leo kama Mwenyekiti Pandu Amir Kificho alivyotangaza jana ni kuwa Bunge Maalum litaanza saa 3 kamili asubuhi na kazi itakuwa moja tu ambayo ni KURIDHIA RASIMU YA KANUNI ZA BUNGE MAALUM baada ya kusomwa kwa AZIMIO na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni Prof MAHALU. Kwa leo tutarajie hali ya utulivu kuendelea kutamalaki hasa kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Kamati ya Mashauriano ambayo kiukweli imefanikiwa kuweka mazingira ya utulivu Bungeni.

Kama Kawaida, natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wetu mbalimbali waliopo ndani na nje ya nchi. Kwa upekee kama kawaida Mkuu Skype pamoja na Mheshimiwa Simiyu Yetu watakuwa wanatoa ushirikiano uoahitajika. Stay aconnected

asante
ila vp kura ipi imepita ya sir au ya wazi
 
Pamoja sana Mkuu. Hakika mmeufanya mtandao huu kuwa mbele ya vyanzo vingine vya habari hapa nchini katika suala hili la Katiba mpya. Yaani hata mtu asipoangalia TV au kusikiliza Radio, anapata kile kinachojiri kwa wakati. Hongereni sana wakuu
Sahihisho dogo ni kuwa ktk Kiswahili neno 'hongera' halina wingi, kwa hiyo hakuna 'hongereni'.
 
hii mada ina harufu ya upuuz flani wa kishabiki!

UZI UNASOMEKA 'YANAYOJIRI BUNGENI DODOMA LEO JUMANNE TAREHE 11/03/2014' - Unaweza kunionyesha sehemu yoyote yenye dalili za kishabiki kuhusiana na mada tajwa? Au mimi ndo sikuelewi vizuri. Ninavyoelewa mimi kwa kuwa namfuatilia sana anayetujuza yanayotokea huko bungeni, anatupatia matukio juu ya masuala na mambo mengine yanayohusiana na mwenendo mzima wa utungaji wa katiba ya JMT.
 
Bila kupitisha kanuni juu ya jinsi ya kipiga kura ni upuuzi mtupu!kikao bila maamuzi ni upuuzi pia.CCM kwa nini hamtaki kura ya siri?hivi mtathubutu kuja kutuambia wananchi KURA NI SIRI YAKO?CHAGUA MGOMBEA UNAYEMTAKA.hamna uchungu na kodi zetu karibu mwezi sasa mnajadili kanuni tuu
Kura ya siri ni ya kumchagua mtu, siyo ya kufanya maamuzi ya Bunge. Ni hivyo ulimwenguni kote.
 
Mkuu, Ole Sendeka hajambo na amejaa tele. Ile kanuni ya upigaji kura ilishapita baada ya kufanyika marekebisho kidogo. Kwamba badala ya kusema kuwa maamuzi yataamuliwa kwa kura ya siri, imeandikwa kuwa yataamuliwa kwa kupiga kura ambayo itaamuliwa na Bunge amaalum. Ni hayo tu mkuu

Lakini promotion ya kura ya siri imefanikiwa tutegemee ndiyo itatumika, kila kona ya nchi kura wazi imepigwa vita.safi sana.narejea Kakobe na swaga ya luga za watawala gongana.
 
Nakushukuru mkuu kwa taarifa unazoendelea kutuletea humu jf kutoka dom,Asubuhi nimeangalia ITV
ambapo nimeshuhudia Mh.Lukuvi akishauri waendelee na bunge la katiba,kwani vipengere vya 37 na 38 vitatumika mwishoni hivyo vitapata ufumbuzi baadae,ameungwa mkono na waziri Simbachawene.
Mimi ktk hili nina maoni tofauti,
Naona si sahihi kukubaliana na hili coz vipengere hivyo vitatumika kila mahali patakapoleta kutoelewana,lazima pataamuliwa kwa kura.sasa kama tutasema hivo vipengere si muhimu ,tunatengeneza mtafaruku mkubwa utakaudumu mpaka mwisho wa bunge na pengine tusifikie mwisho.
Napendekeza,kwa kuwa nchi bado ina katiba,tuangalie katiba ya sasa inasemaje kuhusu jambo lenye mvutano linaamuliwaje? tuifuate ili kutatua mzozo huu uliodumu sana kwenye vikao hivi.
Katiba inapendekeza demokrasia ya kutumia kura ya siri,hivyo basi wabunge wa bunge maalu, watumie kura ya siri kuamua mfumo wa kupiga kura utakaotumika kuandaa katiba.Wapige kura ya siri
Kura zitakazoshinda tutumie mfumo huu badala ya kuendelea kuvutana bila tija huku fedha ya walipakodi ikiendelea kutumika.
 
Hodi Hodi Wadau wote wa Mtandao wetu pendwa, mtandao nambari one Tanzania, mtandao usio na mafungamano yoyote, Mtandao wa Jamiiforums! Natumaini kuwa leo mmeamka salama bukheri wa afya njema. Wale wote ambao kwa bahati mbaya hali zao kiafya si nzuri basi tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wapate nafuu ili angalau wapate fursa ya kuchungulia humu juu ya yale yanayoendelea Bungeni Dodoma. Na kama kuna waliotangulia mbele za haki, basi tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie makazi mema huko.

Wadau, kwa siku ya leo kama Mwenyekiti Pandu Amir Kificho alivyotangaza jana ni kuwa Bunge Maalum litaanza saa 3 kamili asubuhi na kazi itakuwa moja tu ambayo ni KURIDHIA RASIMU YA KANUNI ZA BUNGE MAALUM baada ya kusomwa kwa AZIMIO na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni Prof MAHALU. Kwa leo tutarajie hali ya utulivu kuendelea kutamalaki hasa kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Kamati ya Mashauriano ambayo kiukweli imefanikiwa kuweka mazingira ya utulivu Bungeni.

Kama Kawaida, natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wetu mbalimbali waliopo ndani na nje ya nchi. Kwa upekee kama kawaida Mkuu Skype pamoja na Mheshimiwa Simiyu Yetu watakuwa wanatoa ushirikiano uoahitajika. Stay aconnected
Mkuu hiyo avatar yako itatufanya wanaume tuandamane,hilo jengo liko mji gani?
 
Ni kweli mkuu Watanzania tu Wamoja, ila kuna kundi la kishetani liitwalo ccm wana umoja wao japo wanangangania kuishi Tanzania

Ingekuwa hivyo CCM wasingesubiri maridhiano. Wangetumia wingi wao kushinikiza ipigwe kura, wazi au siri, kuamua kama kura iwe ya wazi au ya siri. Kwamba wameendelea kushauriana na wachache hadi maridhiano inaonyesha kuwa tuko nao pamoja wala si shetani.
 
Nakushukuru mkuu kwa taarifa unazoendelea kutuletea humu jf kutoka dom,Asubuhi nimeangalia ITV
ambapo nimeshuhudia Mh.Lukuvi akishauri waendelee na bunge la katiba,kwani vipengere vya 37 na 38 vitatumika mwishoni hivyo vitapata ufumbuzi baadae,ameungwa mkono na waziri Simbachawene.
Mimi ktk hili nina maoni tofauti,
Naona si sahihi kukubaliana na hili coz vipengere hivyo vitatumika kila mahali patakapoleta kutoelewana,lazima pataamuliwa kwa kura.sasa kama tutasema hivo vipengere si muhimu ,tunatengeneza mtafaruku mkubwa utakaudumu mpaka mwisho wa bunge na pengine tusifikie mwisho.
Napendekeza,kwa kuwa nchi bado ina katiba,tuangalie katiba ya sasa inasemaje kuhusu jambo lenye mvutano linaamuliwaje? tuifuate ili kutatua mzozo huu uliodumu sana kwenye vikao hivi.
Katiba inapendekeza demokrasia ya kutumia kura ya siri,hivyo basi wabunge wa bunge maalu, watumie kura ya siri kuamua mfumo wa kupiga kura utakaotumika kuandaa katiba.Wapige kura ya siri
Kura zitakazoshinda tutumie mfumo huu badala ya kuendelea kuvutana bila tija huku fedha ya walipakodi ikiendelea kutumika.

Siyo kwamba hilo halijulikani, tatizo ni CCM ILIYOJIDEKEZA TANGU ILIPOJIPA HESHIMA YA KUSHIKA HATAMU. Sheria kwao inapata nguvu inapokuwa na maslahi kwao, kama ni vinginevyo wapo tayari kuwa juu yake! Hii ni tabia ambayo wasipojifunza kuiacha basi ni wazi CCM italeta machafuko nchi hii. Tolerance ya raia wengi kwangu inaonekana imefika mwisho!
 
Pamoja sana Mkuu. Hakika mmeufanya mtandao huu kuwa mbele ya vyanzo vingine vya habari hapa nchini katika suala hili la Katiba mpya. Yaani hata mtu asipoangalia TV au kusikiliza Radio, anapata kile kinachojiri kwa wakati. Hongereni sana wakuu
This is true, nikianza kupitia update utafikiri na cheki tv live, big up ndugu zangu mnaotupa hizo update mkiongozwa na chabruma. Ushauri mnaotumia lugha za matusi na kejeli ni vyema kuacha
 
Back
Top Bottom