Ni mtazamao wa chama Tawala baada ya kuchekecha kila aina ya uwezekano wa kupitisha kifungu cha upigaji kura ya wazi au siri. Chama kimeona haitakuwa rahisi kwa sasa kupitisha kipengele chao cha kura ya wazi kwa kuwa wajumbe walio wengi (the 201) hawafahamiki tabia zao na misimamo yao.
Chama kimejipanga kama inavyoelekea kuamuliwa kwamba Bunge lianze, na kipengele hicho kirudiwe wakati bunge likiendelea. Ktk kipindi cha bunge kuendelea, CCM watajipanga jinsi ya kuwaingia wajumbe wengine walio nje ya chama. Watawashawishi kwa ahadi na itakapobidi pesa zitatumika kuwashawishi. Pia wanategemea kumtumia Sitta kwanza ajenge uaminifu kwa wajumbe, wamuone ana niya njema kama dalili zinavyijiojyesha sasa hivi, baadaye atumie uzoefu wake kuwarubuni wajumbe. Rais atakapofungua rasmi bunge pia atatumika kuwaonyesha kwamba wananchi wanahitaji kuwaona kila hatua wanayopitia. Ataonyesha umuhimu wa kura ya wazi ili mitaani pia waone ni njia nzuri. CCM watakapokuwa wamejiridhisha wataomba kura zipingwe kuamua hicho kipengele.
Msiri wetu amasema hayo wakati pia akiwa na wasiwasi kwamba "......hata kama milioni mia moja kwa kila mjumbe anayekubali zitatolewa, hakuna aliye na uhakika kwamba wakipiga kura watafanya kama watakavyoahidi, maana bunge hili lina wasomi ambao misimamo yao mingine ni migumu kuigeuza...."
Huo ndo muujiza unaosubiliwa. Hakika kuna tatizo hapa maana jioni hii, M/kiti anasema wajumbe waje wamevaa kibunge. Bunge linaelekea kuanza wakati hakuna kanuni zilizo kamili. yaani zikiwa na utata. Kila mjadala mwisho wake ni kura, kura yenyewe haieleweki. Binafsi nadhani pia M/kiti Pandu kisha choka matusi ya wazoefu wa bungeni.
Tusubiri.