Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Hii haina tofauti na kubaka demokrasia.
 
Wasipomaliza suala hili na kuendelea na malumbano....walah kesho naenda bungeni kuchukua kodi zangu.....
 
Mh Lukuvi Leo bungeni wakati akichangia kanuni zenye mzozo(37 na 38) alikumbana na zomea zomea ya wajumbe kuonesha kwamba hawakubaliani naye na hata kutoa kauli kwa wajumbe kwamba yeye ameshakuwa sugu wa kuzomewa hivyo haoni shida, mambo yalivyokuwa magumu kwake alitamka kuwa Nanukuu;

Jamani wajumbe Nilimwona Mwenyekiti Akishirikiana na tundu Lissu kurekebisha kanuni hizi hivyo vifungu hivi viko sawa,
Pole mh. Lukuvi
 
CCM woga wa nini?????, hata kumchagua Riz kugombea ubunge kura ilikwa ya siri
 
Kwa mambo yanayotokea huko Dodoma, inaonyesha wazi kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanafanya kila mbinu ili waweze kukaa hapa kwa miaka zaidi ya kumi kwa lengo la kuvuna mapesa.

Pia imeonekana ya kuwa Dodoma kuna watu toka pande mbali mbali wakifanya mambos. Kamfano, usiku vijimbwana wanaonekana wazuri sana utazani vi miss na vimejazia. Lakini usubui pombe ikiisha na kufumbua macho unatamani kukimbia usirudi tena.

Mautamu tamu yote hayo jamani, ndio maana wanahairisha mikutano kwa style ya kuzozana kama walitoroka hospitali ya milembe.

Napenda kutoa hongera kwa Mr. Mwigulu kuchaguliwa kuwa Naibu Waziri, na pia Mr. Ridhiwani kugombea huku Chalinze na zaidi wajumbe wa Bunge la Katiba. Ila nawaomba tu mtangulizeni Mungu awaumbe kama apendavyo ili mfanye kazi kwa mapenzi ya MUNGU na sio vinginevyo.

MUNGU TUBARIKI WOTE. JINA LA BWANA LIBARIKIWE!
 
Huyu ni mtu mjinga kuliko wote aliyewahi kutokea hapa TZ.
Anajidaigi anajua wakati he know nothing only upambe tu labda ndiyo anajua
 
Naye Tundu Lissu awe makini na hizo sifa anazopewa na ccm siku hizi, sifa zimezidi lazima kuna jambo
 

Kama lingekuwa gari la kwenda wapi?
 

Wakae wale washibe wapumue
 
Eee Mungu wa mbingu na nchi naomba jicho lako liangalie Dodoma na Sikio lako lielekeze hapo kwenye Bunge la Katiba,tazama kuna watu wanataka kutuharibia kuandikwa katiba itakayo tufaa sisi Watanzania tuliopo sasa na vizazi vijavyo kwa maslahi yao wenyewe ,sasa ukamhukumu kila atakaye tenda uovu huu na hukumu hii ikadumu mpaka kizazi cha nne cha uzao wake,siku zao zikawe chache,upanga,ukiwa na uharibifu vikawaandame usiku na mchana.

Kwa vile wamejitukuza sana wanaona wao ndo kila kitu eeeh Bwana kumbuka ulichomtendea Mfalme Nebukadreza mpaka alipokiri aliye juu ndiye anaye miliki na kutawala,mkono wako ukaunyoshee juu yao na familia zao mpaka watakapo jua wao ni wanadamu tu tena ni mavumbi na wewe ubaki kuheshimiwa mbinguni na duniani tena mkono wako ulionyooshwa mwanadamu hawezi kuurudisha nyuma,na atakayetoa wazo lake katika kuharibu mchakato huu hapo bungeni ahesabiwa sawa na yule aigusaye mboni ya jicho lako eeh Bwana na kuwa amesimama kinyume ya kila neno lililo jema mabaya yasiondoke hemani mwake siku zote za maisha yake ya kuishi duniani.
 
Waliairishe, waitishe bunge kwa ajili ya bajeti the warudi waandelee na mazingaombwe yao!!
 
nilishawai kusema humu javini kwamba,sifa kubwa ya kiongozi wa ccm ni kutokuwa na haibu ya kuzomewa na ndivyo alivyodhibitisha Lukuvi anasema amezoea kuzomewa kwake sio tatizo hata kama anaongea pumba
 
Swala hili nimeonekana kutishia umoja wa bunge la katiba, hasa maana yapo makundi mawili makuu yenye kuvutana kuhusu ama kura ya wazi ama ya siri, nadhani hekima iliyo onekana ni kuachia "Hekima" ya mwenyekiti kuamua aina ipi kutumika kila inapofikia wakati wa kuamulia jambo fulani huenda kwakusoma mazingira na uzito wa jambo lenyewe, kitu ambacho ninakielewa, ingekua vibaya sana kuachia hili kugawa bunge katika hatua hizi za mwanzo namna hii, hataivyo, hii huenda ikawa kama kuhairisha matatizo kwakuwa ninaona mwanya wa shida kutokea mbeleni pale ambapo mwenyekiti wakudumu ata amua juu ya namna ya kupiga kura kwa kufuata matakwa ya chama flani kinyume na vile ambavyo wengi wangetegemea kulingana na hali iliyopo, hivyo kutoa moral right ya upande mwingine wa wabunge ku riot. kwakifupi ninasema ninaelewa mazingira yaliyo pelekea kufikia kutungwa na kupitishwa kwa kanuni hii ila ninasema itategemea sana uthabiti wa "hekima" hiyo ya mwenyekiti wa bunge. lazima atambue nafasi yake na asikubali kuyumbishwa na influence za vyama. comrades, nashukuru
 

ccm hawajawahi tokea uhuru au kuzaliwa kwao kuendesha mambo bila kuwa na contol nayo, kinachotokea hivi sasa ni kwamba ccm ina struggle kutaka ku control mambo na upande wa pili unakataa na ccm haiwezi kukubali kuachia mambo yaende kama inavyotakiwa bila kuwa na uwezo wa kuamuru yale wanayoyataka. ile nguvu waliyokuwa wakiitumia kwa akina makinda na yule msaidizi wake ya kuendesha bunge kwa kutumia remote control ndio kilio chao kwahiyo dawa ni moja zipigwe kura kuamua kama kura zitakuwa za siri au la.nashindwa kuelewa kwanini hilo halifanyiki??
 
Mimi niliangalia bunge session ya asubuhi nikashindwa kuelewa walikutana kujadili nini hasa????
Manake wanaanza wanabishana then ghafla wanahairisha hadi jioni...

Thats the best part of it..... hatari sana mkuu. Ndio bunge letu hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…