Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yanga wamekunyima usingizi ukajikuta una ubahatisha asb huelewi asb kilichojiri au
na huyu Sitta je!!!!!!halafu mbona sioni updates zozote hapa
Bunge movies
Sitta ana affiliation ya uchama, updates muda bado, subiri kuanzia saa kumi jioni.
Laiti kama tanzania ingalikuwa ni gari ningeshuka na kupanda jingine yaani hawa wabunge wa ccm siamini kama wangetutenda hivi kwenye katiba mpya ambayo ni roho ya nchi haina tofauti na kuolewa halafu mume akakuletea mwanamke mwingine kwenye kitanda kilekile mnacholalia na wewe ungalipo ndani inauma sana jamani hivi ni nani aliyeturoga? Tumtafute.
Kwa mambo yanayotokea huko Dodoma, inaonyesha wazi kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanafanya kila mbinu ili waweze kukaa hapa kwa miaka zaidi ya kumi kwa lengo la kuvuna mapesa.
Pia imeonekana ya kuwa Dodoma kuna watu toka pande mbali mbali wakifanya mambos. Kamfano, usiku vijimbwana wanaonekana wazuri sana utazani vi miss na vimejazia. Lakini usubui pombe ikiisha na kufumbua macho unatamani kukimbia usirudi tena.
Mautamu tamu yote hayo jamani, ndio maana wanahairisha mikutano kwa style ya kuzozana kama walitoroka hospitali ya milembe.
Napenda kutoa hongera kwa Mr. Mwigulu kuchaguliwa kuwa Naibu Waziri, na pia Mr. Ridhiwani kugombea huku Chalinze na zaidi wajumbe wa Bunge la Katiba. Ila nawaomba tu mtangulizeni Mungu awaumbe kama apendavyo ili mfanye kazi kwa mapenzi ya MUNGU na sio vinginevyo.
MUNGU TUBARIKI WOTE. JINA LA BWANA LIBARIKIWE!
nilishawai kusema humu javini kwamba,sifa kubwa ya kiongozi wa ccm ni kutokuwa na haibu ya kuzomewa na ndivyo alivyodhibitisha Lukuvi anasema amezoea kuzomewa kwake sio tatizo hata kama anaongea pumbaWadau, amani iwe nanyi.
Kama kawaida yetu tutaendelea kuwaletea mtiririko wa mijadala Bungeni Dodoma. Kwa sasa Bunge lipo kwenye mchakato wa kukamilisha kupitisha vifungu vya Kanuni za Bunge. Mtakumbuka kuwa vifungu vyote 87 vimepitishwa isipokuwa kifungu cha 37 na 38 ambavyo kwa ujumla wake vinahusu ufanywaji wa maamuzi ndani ya Bunge Maalum. Mjadala hapa ni ama matumizi ya Kura ya Wazi au ya Siri. Mtakumbuka kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 7 Machi, Mwenyekiti Kificho aliunda Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele hivyo. Kamati bado haijamaliza kazi yake na leo wanaendelea na mashauriano. Semina kwa siku ya leo itaendelea kuanzia saa 5 Asubuhi mara baada ya Kamati ya Mashauriano kumaliza kazi yake.
kama kawaida, nitakuwa sambamba na wadau wengine kuwaletea updates zote. Natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa mdau wetu ambaye ni Mbunge wa Bunge hili Maalum, Simiyu Yetu. Pia kwenye Mjadala, natarajia kuwaona akina Skype na MaishaPesa. ​Stay Connected
======================================================================================
UPDATES 1
Wadau, semina imechelewa kuanza kwa vile Kamati ya Mashauriano ilikuwa inaendelea na kikao chake. Kwa sasa kikao kimemalizika na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo James Mbatia, Steven Wasira, Askofu Donald Mtetemela na Sheikh Jongo wameingia Ukumbini. Ni wazi kuwa muda si mrefu Semina itaanza. Tuwe na subira
Kwa mambo yanayotokea huko Dodoma, inaonyesha wazi kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanafanya kila mbinu ili waweze kukaa hapa kwa miaka zaidi ya kumi kwa lengo la kuvuna mapesa.
Pia imeonekana ya kuwa Dodoma kuna watu toka pande mbali mbali wakifanya mambos. Kamfano, usiku vijimbwana wanaonekana wazuri sana utazani vi miss na vimejazia. Lakini usubui pombe ikiisha na kufumbua macho unatamani kukimbia usirudi tena.
Mautamu tamu yote hayo jamani, ndio maana wanahairisha mikutano kwa style ya kuzozana kama walitoroka hospitali ya milembe.
Napenda kutoa hongera kwa Mr. Mwigulu kuchaguliwa kuwa Naibu Waziri, na pia Mr. Ridhiwani kugombea huku Chalinze na zaidi wajumbe wa Bunge la Katiba. Ila nawaomba tu mtangulizeni Mungu awaumbe kama apendavyo ili mfanye kazi kwa mapenzi ya MUNGU na sio vinginevyo.
MUNGU TUBARIKI WOTE. JINA LA BWANA LIBARIKIWE!
Mimi niliangalia bunge session ya asubuhi nikashindwa kuelewa walikutana kujadili nini hasa????
Manake wanaanza wanabishana then ghafla wanahairisha hadi jioni...