Wabunge wote wameunga mkono hoja hiyo na bunge linaahirishwa. Kuna mbunge anataka ipigwe kura ya siri ili wabunge waamue kama bunge liahirishwe au la. Ni vioja tu
Wakuu naomba kuwa wazi tangu nianze kuhudhuria vikao mbali mbali hiki cha bunge la katiba ni kiboko hata watu wazima tunaowaheshimu kabisa wamekuwa kama watoto du! Hii pasua kichwa any way tutafika kwa namna yoyote ile.
Mwenyekiti anawashukuru wabunge kwa umoja wanaouonesha. Anawaomba wajumbe kuendelea na spirit hii. Pia anasisitiza wabunge kuwahi. Bunge linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi
Mie pamoja na Mkuu Skype tunawashukuru sana wale wote walioshiriki pamoja nasi. Basi tuwatakie kila la kheri na kama kawaida tutaungana hapo kesho. Alamsiki
ujinga wa watanzania ni mtaji mkubwa sana kwa CCM.
Makitu hayo hayo yanapirisha upuuzi wa wazi kisha yanaendelea kuchaguliwa tena.
Masikini nchi na taifa langu. Watu wataendelea kuangamia kwa kukosa maarifa.
Tunashuhudia mara kadha wa kadha hali inapokuwa tete katika bunge maalum la katiba, hawa wajumbe hupewa nafasi za kuongea labda ni kutokana na busara walizo nazo ama ni kutokana na nafasi walizo nazo za uenyekiti wa vyama wanavyoongoza. Mimi cjui ila wapo wenye busara kuliko hawa, wapo wenyeviti wa vyama pia kama kina Mrema. "Ama kweli mcheza ngoma ndiye huchagua wimbo"
Kura ya wazi itaharibu kabisa katiba, na kuleta chuki ambayo hatujawahi kuiona Tanzania. Na mkipitisha hii na hata wabunge na madiwani na kura zite ziwe za wazi.
Binafsi huu ubabe wa viongozi wa serikali,matusi,kejeli na kelele za wajumbe naona kama hatutapata katiba bora,Mfano leo j3 mjumbe 1 amemtukana mwenzake kuwa 'kubwa jinga halina adabu' kweli katiba mpya tutaipata kwa staili hii?