Mkuu, pole sana. Ni pigo kubwa kwa timu yetu hii. Hakika hii katikakatika ya umeme inaharibu mambo mengi sana. Ona sass tunavyompoteza mdau wetu mhimu
Mkuu, katika maridhiano ya awali ambayo yalifikiwa siku ya Ijumaa, ni kwamba Kamati ya Mashauriano ilifikia muafaka wa kura ya Siri. Hata hivyo kuna masuala mengi yalikuwa hayajakaa sawa na pia walipitejesha kwenye makundi yanayounda bunge hilo, baadhi ya makundi yaliendelea kuwa na msimamo wa matumizi ya kura ya Wazi. Ikumbukwe kuwa matumizi ya kura za Siri yameridhiwa kwa lengo la kuendeleza mshikamano na umoja wa kitaifa hasa ikizingatiwa kuwa kuna makundi hasa vyama vya siasa walitamka wazi kuwa ikiwa kura ya wazi itatumika, watajiondoa kwenye mchakato wa katiba na kwenda mahakamani kusimamisha mchakato huo. Ni kutokana na mazingira hayo ndipo ulazima wa kura ya siri ulipojitokeza. Hii ni kusema kuwa kura ya Siri haijatokana na hoja bali na mazingira yaliyopo ndani na nje ya bunge
Ni mjinga kwa sababu alipewa bahasha na pinda..kanunuliwa.Mkuu, suala la matusi si jema sana karika mjadala huu. Hata kama ni mjinga, ana nafasi yake katika mashauriano
Mkuu, sina hakika kama Simiyu Yetu ni miongoni mwa wale 201. Anaweza kuwa mbunge wa kuchaguliwa
Ndiyo. wakitaka kura ya wazi wapige wao peke yao.
Mkuu, nadhani watakuwa hewani maana nawaona hapa wapo. Pengine wanasubiri mjadala uanze ndo wawe hewani
Mkuu hili suala la misimamo ya kichama ndo linachelewesha mambo. CHADEMA wao walitangaza muundo wa serikali tatu na kura ya siri. CCM wao wamekuja na serikali mbili na kura ya wazi. Ni vitu viwili tofauti na hivyo kuliweka jambo hili la katiba kwenye rehani. Wanasiasa wameteka mjadala huu wa Bunge la Katiba badala ya wananchi wa kawaida. Hii ni kutokana na wao kuwa wengi. Mfumo uliopendekezwa wa kuwa na makundi matatu ya wabunge ndo unatuathiri katika hilithen jamaa anaweza kuwa yuko fresh ila itikadi za vyama zinatutesa sana mkuu! si ndio kama jivi jambo la wiki moja linachukua mwezi coz itikadi na maslahi binafsi
Mkuu, kwa bahati mbaya orodha ya kamati ya mashauriano haikuwekwa bayana. Ila wajumbe ninaowafahamu kwa haraka haraka ni Mbowe, Mbatia, Lipumba, Askofu Mstaafu Donald Mtetemela, Sheikh Jongo, Cheyo, Wasira na wengine. Wamo pia wajumbe kutoka wwle 201
inamaana Leo tbc hawapo hewani live