Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Ndiyo ni chombo muhimu lakini kwa kadiri wanavozidi kuchelewa kufikia maamuzi ndivyo kodi zetu zinavyozidi kuteketea, mkuu mimi nina uchungu na kodi zetu tu na si vinginevyo japo napenda maridhiano yaliyo bora.
Ni kweli mkuu. Hakika kitendo cha kukaa muda mrefu bila ya kufikia muafaka kwenye hoja iliyo dhahiri, ni wazi kuwa kodi zetu zinapotea
 
Zingatia: Tayari mawazo mahususi (specific) ya wananchi kuhusu katiba yalishakusanywa na kuwekwa kwenye rasimu ya katiba! Nani hao wengine waliotumwa na wananchi?
 
Mkuu Skype heko sana, nafikiri mdau alihitaji list ya wajumbe wanaounda kamati ya mashauriano, namu napenda kuwajua ni akina nani ili tujue uamuzi wa siri/wazi utakuwa muelekeo upi?

Miongoni mwao ni hawa hapa, wengine siwajui:

1. Mizengo Pinda.
2. Haruna Lipumba
3. Freeman Aikael

cc. Acuity (kumradhi mkuu sikuelewa kwa haraka nikabandika majina ya wajumbe wa bunge hili)
 
Last edited by a moderator:
Kama ni kweli simiyu yetu naye ni mjumbe wa bunge hili basi nchi hii imelaaniwa na pale wamejaa wahuni na wajinga wajinga tu, hamna la maana.

Bila watu kama wakina simiyu siasa haija balance na hata bunge lenye wakina simiyu nalo ni bunge wananiacha hoi wiki ya tatu hawajamaliza kanuni
 
Mkuu Skype heko sana, nafikiri mdau alihitaji list ya wajumbe wanaounda kamati ya mashauriano, namu napenda kuwajua ni akina nani ili tujue uamuzi wa siri/wazi utakuwa muelekeo upi?
Mkuu, kwa bahati mbaya orodha ya kamati ya mashauriano haikuwekwa bayana. Ila wajumbe ninaowafahamu kwa haraka haraka ni Mbowe, Mbatia, Lipumba, Askofu Mstaafu Donald Mtetemela, Sheikh Jongo, Cheyo, Wasira na wengine. Wamo pia wajumbe kutoka wwle 201
 
Miongoni mwao ni hawa hapa, wengine siwajui:

1. Mizengo Pinda.
2. Haruna Lipumba
3. Freeman Aikael
Pamoja sana Mkuu. Nilisahau hilo jina la Pinda. Pia yupo Anna Makinda
 
Jaji warioba ndio aliekuja kuongea na sisi
Wananchi na tukamtuma kwa wingi wetu wa
Asilimia 61 tumeshatoa mongozo
Hawa Maccm wametumwa na nani?
 
Pamoja sana Mkuu. Nilisahau hilo jina la Pinda. Pia yupo Anna Makinda

Binafsi kwa maoni yangu sina imani tena na mtu huyu kwa ujeuri na dharau alizonazo kwa wananchi, anyway wacha nisubiri matokeo ya kikao hicho.
 
Jaji warioba ndio aliekuja kuongea na sisi
Wananchi na tukamtuma kwa wingi wetu wa
Asilimia 61 tumeshatoa mongozo
Hawa Maccm wametumwa na nani?
Mkuu, mchakato wa Katiba mpya ni pamoja na Bunge la Katiba. Hivyo kuwa na subira juu ya yanayoendelea. Wote wana lengo moja tu
 
Mkuu, Mwigulu alikuwepo sikunya Ijumaa na Jumamosi. Leo sijamuona ila nina hakika kuwa yupo kwq vile kuna vikao vya CCM vinaendelea na Mwenyekiti taifa yupo hapa kwa siku tatu

dah! mwenyekiti nae kaja? basi tutakesha kupata huo muhafaka.
 
Binafsi kwa maoni yangu sina imani tena na mtu huyu kwa ujeuri na dharau alizonazo kwa wananchi, anyway wacha nisubiri matokeo ya kikao hicho.
Mkuu, katika mchakato huu wa katiba, hata kama watu mnatofautiana kiasi gani, kuaminiana ni jambo la maana sana
 
Back
Top Bottom