Last edited by a moderator:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna habari kuwa rais ametua hapo jana ili kusaidia kamati ya mashauriano kufikia muafaka! Kuna ukweli wowote??Pamoja sana Mkuu, kwa sasa niite tu Mtanzania kwani ndo kiungo chetu sote. Tuwe pamoja na tushirikiane katika hili ili jahazi lifike salama
Kama ni kweli simiyu yetu naye ni mjumbe wa bunge hili basi nchi hii imelaaniwa na pale wamejaa wahuni na wajinga wajinga tu, hamna la maana.
ina maana Simiyu Yetu ni mmoja kati ya wale 201?
Mkuu, ni kweli Rais alitua hapa jana. Ujio wake si kwa sababu ya kusaidia kupata maridhiano juu ya vifungu hivyo bali alikuja kwa ajili ya vikao vya kawaida vya CCM. Ni imani yangu na yako kuwa uwepo wake hapa Dodoma utasaidia kufikia maridhiano katika vifungu shindaniwaKuna habari kuwa rais ametua hapo jana ili kusaidia kamati ya mashauriano kufikia muafaka! Kuna ukweli wowote??
Kuna habari kuwa rais ametua hapo jana ili kusaidia kamati ya mashauriano kufikia muafaka! Kuna ukweli wowote??
Mkuu, ni kweli Rais alitua hapa jana. Ujio wake si kwa sababu ya kusaidia kupata maridhiano juu ya vifungu hivyo bali alikuja kwa ajili ya vikao vya kawaida vya CCM. Ni imani yangu na yako kuwa uwepo wake hapa Dodoma utasaidia kufikia maridhiano katika vifungu shindaniwa
Mkuu, katika maridhiano ya awali ambayo yalifikiwa siku ya Ijumaa, ni kwamba Kamati ya Mashauriano ilifikia muafaka wa kura ya Siri. Hata hivyo kuna masuala mengi yalikuwa hayajakaa sawa na pia walipitejesha kwenye makundi yanayounda bunge hilo, baadhi ya makundi yaliendelea kuwa na msimamo wa matumizi ya kura ya Wazi. Ikumbukwe kuwa matumizi ya kura za Siri yameridhiwa kwa lengo la kuendeleza mshikamano na umoja wa kitaifa hasa ikizingatiwa kuwa kuna makundi hasa vyama vya siasa walitamka wazi kuwa ikiwa kura ya wazi itatumika, watajiondoa kwenye mchakato wa katiba na kwenda mahakamani kusimamisha mchakato huo. Ni kutokana na mazingira hayo ndipo ulazima wa kura ya siri ulipojitokeza. Hii ni kusema kuwa kura ya Siri haijatokana na hoja bali na mazingira yaliyopo ndani na nje ya bungeNaomba kupewa dondoo kuhusu maridhiano yaliyofikiwa ktk vifungu vya 37 na 38 kabla semina haijaanza.
cc. Chabruma
cc. MaishaPesa
cc. Simiyu Yetu
cc. Mjumbe mwingine yeyote mwenye kujua hili
Mkuu, ni kweli Rais alitua hapa jana. Ujio wake si kwa sababu ya kusaidia kupata maridhiano juu ya vifungu hivyo bali alikuja kwa ajili ya vikao vya kawaida vya CCM. Ni imani yangu na yako kuwa uwepo wake hapa Dodoma utasaidia kufikia maridhiano katika vifungu shindaniwa
Mdau mwenzangu, kama nilivyoeleza kuwa Rais hayupo hapa kwa ishu ya katiba bali kwa shughuli za kichama. Hata hivyo kwa vile hoja hii ipo mezani, ni wazi kuwa anaweza kutumia fursa hii kushiriki kutafuta muafaka. Binafsi siamini kuwa Rais JK anaweza kushinikiza msimamo wa chama hasa ikizingatiwa kuwa Rais wetu ni msikivu na anaamini maamuzi ya pamoja na anaheshimu mawazo ya walio wengi.Mkuu, unaweza ukawa sahihi lakini kumbuka jakaya ni mwana ccm, na ccm kwa mujibu wa wajumbe wake wafurukutwa (sendeka) wanataka kura ya wazi, na kwa mujibu wa matamko yao huo ndo msimamo wa chama. Je, nitakua sahihi nikisema jakaya kaja kushinikiza maridhiano yawe upande wa msimamo wa chama ama la? Kwa nini?
Mkuu, katika maridhiano ya awali ambayo yalifikiwa siku ya Ijumaa, ni kwamba Kamati ya Mashauriano ilifikia muafaka wa kura ya Siri. Hata hivyo kuna masuala mengi yalikuwa hayajakaa sawa na pia walipitejesha kwenye makundi yanayounda bunge hilo, baadhi ya makundi yaliendelea kuwa na msimamo wa matumizi ya kura ya Wazi. Ikumbukwe kuwa matumizi ya kura za Siri yameridhiwa kwa lengo la kuendeleza mshikamano na umoja wa kitaifa hasa ikizingatiwa kuwa kuna makundi hasa vyama vya siasa walitamka wazi kuwa ikiwa kura ya wazi itatumika, watajiondoa kwenye mchakato wa katiba na kwenda mahakamani kusimamisha mchakato huo. Ni kutokana na mazingira hayo ndipo ulazima wa kura ya siri ulipojitokeza. Hii ni kusema kuwa kura ya Siri haijatokana na hoja bali na mazingira yaliyopo ndani na nje ya bunge
Samahani wadau, kwa haraka mwenye orodha ya wajumbe wanaounda kamati ile ya maridhiano, atuwekee hapa tunaweza kufahamu nini kitaletwa Bungeni kabla ya wasilisho lao....