Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

anaanza kwa kusema kaxi waliyotumwa imemalizika.anasema kanuni za sasa za maamuzi zitakua kwa kura
 
Kanuni ya 37 na 38 zitaelezea kwamba, utaratibu wa uamzi utakua ni wa kura, na itawekwa fasili kwenye kanuni ya 38 kuelezea ni namna gani ya kura itakayofanyika
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni anasema kuwa kazi ya kukamilisha kupitisha vifungu vya kanuni imekamilika. Anasema kuwa wabunge watapata nakala za kanuni za marekebisho leo mchana. Kuhusu kanuni za 37 na 38 anasema kuwa kanuni hizo zitaelezea tu kuwa utaratibu utakaotumika kufanya maamuzi ni wa kura. Pia wataongeza ibara nyingine ambayo itasema kuwa aina ya kura itakayotumika itaamuliwa na Bunge. Mwenyekiti wa Kamati amemaliza kuwasilisha
 
Mwenyekiti anaeleza kuwa kwa vile kamati ya mashauriano inaendelea na kazi yake, ni wazi kuwa mwenyekiti wa kamati asingesema zaidi ya yale aliyosema. Anasema kuwa nakala za kanui hizo zitapatikana kuanzia saa 9 Alasiri. Anasemamkuwa kazi ya kikao cha jioni ni kuridhia kanuni hizo kwa tamko litakalosomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni. Kwa sasa Mwenyekiti anasema kuwa kwa sasa bunge halina cha kujadili
 
Mwenyekiti qnawataka radhi wajumbe kwa kuchelewa kuanza. Badala ya saa tano kamili, na sasa ni saa sita na robo. Amesema kuwa hiyo imetokana na mashauriano yaliyokuwa yanaendelea na kamati husika

Tunashukuru sana mkuu kwa updates unazotoa! For real una deserve tuzo hapa jf! Barikiwa sana tupo pamoja kutoka nanjilinji, kilwa lindi.
 
Mwenyekiti anasema kamati ya maridhiano bado inaendelea kujadili kuhusu utaratibu wa kupiga kura na wabunge wataamua jioni saa kumi na moja.
 
Kuna mjumbe anasisitiza wajumbe wawe serious na shughuli. Inaonekana pande mbili bado zinavutana. Anasisitiza endapo na jioni hali itakua blah blah basi bunge lisimame. Sijui jina la huyu mjumbe ila anahoja nzuri sana.
 
Ni mtazamo wa wengi kuwa CCM kupinga maoni ya wananchi hususani suala la serikali tatu ni kiashiria cha utawala ulifitinika na unao karibia mwisho wake

Hakuna anayeweza kupinga msimamo wa chama kama taasisi, kutoa maoni lakini inapofikia walio wengi wananchi wameamua basi maoni ya Taasisi hayana uhalali tena. Zaidi ya yote naamini hata katika maoni ya watanzania walio taka serikali 3 pia wanaccm wamo.

Sasa hili la kusema ccm kama taasisi wanahitaji serikali 2 linatoka wapi tena ? mtazamo wangu ni kwamba sio ccm inayotaka serikali 3 bali ni viongozi wachache wa ccm ndiyo wenye maslahi na serikali 2.

MUNGU bariki bunge la katiba lifanye majadiliano yenye tija kwa mstakabali wa taifa kwa ujumla wake na si kwa maslahi ya makundi .
 
Kafulila anaongea.hakuna kinachoendelea, anadai kuna pande mbili zinazovutana.anashauri kama jioni wakishindwa kuafikiana semina ivunjwe ili kupatikane muafaka.anatia hoja
 
Kafulila anataka bunge liahirishwe kwa kipindi ili majadiliano yafanyike nje ya vikao vya Bunge. Hii ni kutokana na wabunge kuchukua muda mrefu kujadiliana juu ya upigaji kura. Hata hivyo Mwenyekiti anasema kuwa Bunge halitaweza kuahirishwa kwa vile limetokana na Tangazo la Rais hivyo si jambo jepesi kuliahirisha
 
Mwenyekiti anapangua hoja ya mjumbe aliyependekeza bunge lisimame hadi muafaka ufike kuepusha kutafunwa kodi zetu. Mwenyekiti anasema haiwezekani kwa kua eti rais alilifungua
 
Mwenyekiti anasema kama hoja ni kuvunjwa kwa bunge bali mwenye jukumu la kuvunja ni la Raisi maana kufsnyika kwa bunge kumukuja kwa tangazo la Rais
 
Back
Top Bottom