Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Mkuu mimi siku hizi siamini sana ktk cv za watu, na badala yake naamini ktk utendaji na ufanisi wa mtu. Jitu la namna ya simiyuyetu unaweza kuta ni miongoni mwa yale majitu ya siku hizi yanayojiita dr.dr.dr.dr. XXXX pasipo hata kua na chapisho japo moja tu achilia mbali udaktari wa tiba kisha linatukana wananchi walipa kodi kwa kudai eti serikali haina fedha za kulipa mishahara mikubwa huku mchwa (wanasiasa) wakipeana maposho manono.

Nimekuelewa Mkuu Skype ..Hali ni mbaya sana.. 🙁
 
Last edited by a moderator:
hapa tuikumbuke hoja ya mnyika tu,kwamba nchi imefika hapa kwa udhaifu wa .. na .. na .. Ukijaribu kutafakari yaliyojitokeza bungeni leo ni muendelezo wa CCM kutugeuza watanzania wote ni watu wa ovyo sana!wanasema tukutane jioni tupitishe kanuni na hayo mambo ya wazi au ya siri ni ya mbele haina haja kuyapatia ufumbuzi sasa,kama hivyo ndivyo kuahirishwa ahirishwa kwa bunge na kuundwa kwa kamati ya mwafaka lilikuwa kwa maana ipi?kwanini tumepoteza muda hivi huku mkijifanya mlikuwa na majibu?kwa nini mwatuchezea watanzania?au ndio kiburi cha kututawala kwa zaidi ya miaka 50?ezekiel oluoch ametoa wazo zuri lakin mbele ya ccm limeonekana la kipuuzi,naanza kukosa imani kwa hawa mashehe na maaskofu waliomo humo bungeni,kwanini hawayakemei mambo haya?wanamuogopa nani?wajue watajibu mbele za MUNGU kwa kufumbia kwao upuuzi huu unaoendelea bungeni!ALL IN ALL MAMBO HAYA HUWA YANA MWISHO JAPO HUO MWISHO TUTAKUWA TUMESHAUMIA AU KUNUKA DAMU KABISA.MUNGU SIKIA KILIO CHETU WATANZANIA
 
Wadau, amani iwe nanyi.

Kama kawaida yetu tutaendelea kuwaletea mtiririko wa mijadala Bungeni Dodoma. Kwa sasa Bunge lipo kwenye mchakato wa kukamilisha kupitisha vifungu vya Kanuni za Bunge. Mtakumbuka kuwa vifungu vyote 87 vimepitishwa isipokuwa kifungu cha 37 na 38 ambavyo kwa ujumla wake vinahusu ufanywaji wa maamuzi ndani ya Bunge Maalum. Mjadala hapa ni ama matumizi ya Kura ya Wazi au ya Siri. Mtakumbuka kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 7 Machi, Mwenyekiti Kificho aliunda Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele hivyo. Kamati bado haijamaliza kazi yake na leo wanaendelea na mashauriano. Semina kwa siku ya leo itaendelea kuanzia saa 5 Asubuhi mara baada ya Kamati ya Mashauriano kumaliza kazi yake.

kama kawaida, nitakuwa sambamba na wadau wengine kuwaletea updates zote. Natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa mdau wetu ambaye ni Mbunge wa Bunge hili Maalum, Simiyu Yetu. Pia kwenye Mjadala, natarajia kuwaona akina Skype na MaishaPesa. ​Stay Connected

======================================================================================
UPDATES 1

Wadau, semina imechelewa kuanza kwa vile Kamati ya Mashauriano ilikuwa inaendelea na kikao chake. Kwa sasa kikao kimemalizika na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo James Mbatia, Steven Wasira, Askofu Donald Mtetemela na Sheikh Jongo wameingia Ukumbini. Ni wazi kuwa muda si mrefu Semina itaanza. Tuwe na subira

ndugu yangu Chabruma hivi Mh E. Lowassa yumo mjengoni, kwani sijasikia comment zake hata kidogo kuhusu hoja yeyote iwe kura ya wazi au ya siri. Au ndio kifungo cha kutaka uraisi hakikwepa wananchi wasijue msimamo wake. lakini kwa kumsemea anaonekana anataka kura ya siri
 
wabunge wa ccm washenzi na wahuni wakubwa ndo wanaruvuga bunge

Watanzania tunavua tulichopanda mkuu? CCM hawastahili kuongoza nchi hii hata kwa dakika moja... sema ndio hivyo tena wananchi bado wamelala
 
Laiti kama tanzania ingalikuwa ni gari ningeshuka na kupanda jingine yaani hawa wabunge wa ccm siamini kama wangetutenda hivi kwenye katiba mpya ambayo ni roho ya nchi haina tofauti na kuolewa halafu mume akakuletea mwanamke mwingine kwenye kitanda kilekile mnacholalia na wewe ungalipo ndani inauma sana jamani hivi ni nani aliyeturoga? Tumtafute.
 
Ninashauri wapige kura ya siri na ya wazi. halafu matokeo ya kura zote yajumlishwe, mfano: siri: ndiyo, hapana 5, 2 + wazi: ndiyo, hapana, 4, 6, respectively (sahawia)= ndiyo: 9; hapana: 8.
 
ndugu yangu Chabruma hivi Mh E. Lowassa yumo mjengoni, kwani sijasikia comment zake hata kidogo kuhusu hoja yeyote iwe kura ya wazi au ya siri. Au ndio kifungo cha kutaka uraisi hakikwepa wananchi wasijue msimamo wake. lakini kwa kumsemea anaonekana anataka kura ya siri
Mkuu, EL yupo Bungeni kama kawa. Siku zote yupo ingawa hajawahi kuchangia hata siku moja. Kuna wazee wengi tu ambao wanahudhuria vema ila kwenye kuchangia hawamo. Nadhani wanavuta kasi ya Rasimu yenyewe ya Katiba
 
Ninashauri wapige kura ya siri na ya wazi. halafu matokeo ya kura zote yajumlishwe, mfano: siri: ndiyo, hapana 5, 2 + wazi: ndiyo, hapana, 4, 6, respectively (sahawia)= ndiyo: 9; hapana: 8.
Ni wazo zuri mkuu. Ila katika ishu ya katiba, cha muhimu si kujua nani ameshinda bali maridhiano. Wakipiga kura, ni wasi kuwa CCM itashinda na hivyo kuonekana kuwa kila kitu ccm inadominate
 
Back
Top Bottom