MAKAMBA:LOWASA ALIFUKUZWA KAZI,
HAKUJIUZULU!
Katibu mkuu mstaafu wa CCM luteni mst Yussuf Makamba amesema kuwa aliyekua Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa alikua ameshafukuzwa kazi kabla ya kujiuzulu.
Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais za CCM katika kiwanja cha Kawawa mjini Kigoma.
Akifafanua suala hilo mzee Makamba amesema kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM katika kikao kilichokaa mjini Dodoma, baada ya kuridhika kuwa Lowasa alihusika na kashfa ya Richmond,iliteua watu watatu kwenda kumuona Rais Kikwete kumueleza kuwa kwa maslahi ya nchi na chama amfute kazi Waziri Mkuu wake Edward Lowasa kwakua kamati ya uongozi imeridhika kuwa alimuita na kashfa ya Richmond na kulifedhehesha taifa.
Watu hao watatu walikua katibu mkuu wa CCM wakati huo mzee Makamba, mzee Samuel Malecela na mama Anna Abdallah.
"Tulipofika kwa Rais Kikwete tulikutana na Lowasa nje akitokea ndani kwa Rais, tukaingia na kumkuta bwana mkubwa. Tukapewa kahawa. Kisha tukamueleza kuwa tumetumwa na kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kuwa Waziri mkuu amehusika na kashfa ya Richmond na kwa heshima ya CCM na taifa amfukuze kazi.
Rais Kikwete akatuuliza,
...hamjakutana nae hapo nje?
Tukajibu...tumekutana nae anatoka...
Akasema...nimekwisha kumwambia kuwa kwa heshima ya taifa na CCM hawezi kuendelea kuwa waziri mkuu tena na kwamba nateua waziri mkuu mwingine...
Makamba alisema kuwa baada ya Rais kumfukuza kazi Lowasa, kesho yake asubuhi Lowasa aliamkia bungeni na alipopewa nafasi ya kujitetea alisema tatizo nu uwaziri mkuu na kwamba amemuandikia barua Rais aachie ngazi.
"Ukweli ni kwamba Rais alishamfukuza kazi Lowasa usiku wa kuamkia siku aliyotangaza kiachia ngazi na kujiuzulu. Lakini tuliamua kumsitiri. Sasa kwakua kaamua kusema, nasi tumekuja kueleza akiba tuliyoweka."
Na Mwandishi wetu,
Kigoma