#COVID19 Yaliyojiri JamiiForums Clubhouse kwenye Mjadala wa UVIKO-19, Umechanja au haujachanja? Nini mtazamo wako?

Binafsi sijachanja na Sina hakika Kama nitachanja.Ahsante
 
serikali ya mabavu ya ccm walifanya big mistake kumtishia Gwaajima na kamati za bunge,wangekuwa weledi wangeunda kamati ya wataalam wa afya na kumuita Gwajima na kuzungumza tena live huku watanzania wote tukiona,sichanji wala sina mpango kabisa
 
Mualikeni gwaji na polepole mkijibu maswali yao asubuh nachanja mapemaaaaa sana
 
Nasema hili , na huu na mtazamo binafsi.

Kuna watu wengi sana hawajaona umuhimu wa kupata chanjo.

Lakini bado, wataalamu wetu wa afya wameshindwa kuja na ushawishi wa kwanini ni muhimu kupata chanjo, kuna watu hawana elimu za Afya na wanabaki na swali ambalo hadi sasa halijajibiwa kwa usahihi kuwa Kwanini watu waliochanjwa wanaweza kupata maambukiz sawa na watu ambao hawajapata chanjo, kwanini waliochanjwa wanapaswa kuvaa barakoa na kuchukua tahadhari sawa na watu ambao bado hawajachanjwa?
 
Pamoja na kuwa kuchanja ni hiari lakini muitikio wa watu ni mdogo sana. Wataalamu wa Public health wafanye hamasa ya kuelimisha jamii.

posters au mabngo, Instagram na redio na TV.
 
sijachanja sintashiriki
 
Hiyo mijadala mnapoteza muda tu, kwa dunia ya leo kunamtz ambaye hajui kuwa chanjo ya uvico tayari ipo nchini na kuchanjwa ni hiari?

1. Sichanji, kwasababu siyo lazima. Cd4 buku jero zinanitosha.
2. Covid nilishaugua, ni ugonjwa unaotibika wenyewe tu, yaan kama mafua tu. (USINIIGE)
3. Virusi vya covid naona kila siku wanaibuka generation mpya, nasubiri pia nipate hao akina delta, MU n.k ili nijipime kama naweza kuwashinda (Nitaweza tu if God wishez)

Nb, Personally sipendi kabisa kutumia dawa ovyoovyo hasa hizo za viwandani, ni baada ya wizara husika kuruhusu dawa za Quinine miaka hiyo kwaajili ya kutibu malaria na zikanipelekea uziwi permanently hadi leo. Never and never trust anybody.

OVER.
 
Mbali nakuangalia waliochanja na ambao hawajachanja ukizingatia Uviko-19 umeonekana ni gonjwa ambalo utakuwepo muda. Mpango gani uliopo wa wataalamu wetu wa Afya kuja na chanjo zetu kama Taifa ? Maana mataifa mengine tunaona wanakuja na chanjo zao. Tusisahau pia Taifa lipo katikati ilihali ni lazima ikitokea unataka kutoka nje ya nchi.
 
naona wapi mjadala?
 
Binafsi nimechanja Johnson kama miezi miwili iliyopita.nikiri kuwa niliipata nje ya nchi na kiukweli sijapata madhara yeyote na niseme tu unaedza pata mafua na kikohozi ama dalili za covid kwakuwa nimezungukwa na kundi kubwa la ambao hawana chanjo. Lakini bado naamini kuchanja ni bora zaidi kuliko ambaye hajapata chanjo. Watanzania wengi walijengewa hofu na rais marehemu Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…