Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 22, 2021. Mahakama yatupilia mbali hoja tatu za utetezi. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 23, 2021

Maamuzi haya yalijulikana toka mwanzo. Anatimiza alichoagizwa. Anachohangaikia ni kitafuta mahali pa kujibanza ili atoe hukumu inayoendana na dhamira yake.

Kibatala na timu yako, nina hakika unafahamu kuwa huyu jahi ni miongoni mwa wale wasiojulikana waliopelekwa na marehemu mahakamani kuvuruga mfumo wa mahakama. Na sasa, hangaya anawatumia.

Lakini msikate tamaa. Endeleeni na mapingamizi kila inapostahili kwani haya yatakuja kusaidia huko mbeleni.

Mbowe, inapowezekana, endelea kuwakataa hawa wasiojulikana waliopachikwa mahakama, japo hata akitolewa huyu, sba atamweka mwingine kutoka kwenye kundi lao. Lakini ni vema waendelee kuwabadilisha ili list yao, umma uifahamu. Na wapo wengi. Ndiyo maana tukipata katiba mpya, na uongozi wenye weledi kuanzia serikalini na bungeni, mahakama inatakiwa kuundwa upya.
 
bac sawa ndugu Jaji tumeukubali uamuzi wako wa leo, naona sasa tunarudi tena Rau Madukani kwa mama Pendo.
 
Jaji kapindua meza,HII kali
Hahahah - mtaelewa tu kwamba hakuna kesi ndogo, kwamba serikali haina ushahidi, ana kwamba mawakili wa serikali na polisi ni watupu kichwani
 
Hii kesi ina hukumu tayari, tangu siku ile ya BBC na Sirro alivyosema walishaamua kumfunga Mbowe.
Nafsi zitawasuta wakimfunga Mh.Mbowe.Ewe Binadamu una khofu ya nini kama unamuamini Mola wako muumba wa nchi na mbingu...??
Ewe Binadamu elewa kwamba Mwenyezimungu hasemi uwongo..."Dhulma haidumu na ikidumu huangamiza"....dalili zipo nyingi na tumeziona.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Maamuzi haya yalijulikana toka mwanzo. Anatimiza alichoagizwa
Kwa hiyo humo mahakamani mnatafuta nini?
 
Kuna timu inapigwa magoli lakini mashabiki wake ndio wanashangilia! Mpaka sasa ni 9-1!
 
Mawakili wajitoe tu jaji awahukumu anavyotaka ili nafsi zao zofurahi
 
Hivi mnahangaika na maamuzi ambayo yako tayari? Mawakili wa Mbowe, jitoeni Tiganga atoe hukumu apandishwe kuwa Justice of Appeal.
 
Jaji: Nimeona Kwamba Siyo lazima Kielelezo hicho kuwa na Amri ya Mahakamani, Kwa sababu hiyo naitupilia Mbali Sababu zote tatu za Mapingamizi ya Kuzuia Kielelezo hicho, NATOA AMRI
Yaani kila pingamizi halina maana? Kazi ipo kweli kweli, njaa mbaya sana
 
Uamuzi wa jaji ni wa kuunga unga ili tu aweze kutimiza yale ambayo wabambikaji wa kesi hii wameamuwa kuyatimiza. Jaji ametupilia mbali hoja ya kielelezo kutolewa kwa amri ya mahakama kama kielelezo hicho kinatakiwa kwenye kesi zaidi ya moja na mahakama zaidi ya moja. Je ni kweli kielelezo hicho kinatumika kwenye kesi nyingine? Mahakama nyingine?

Kwanza alisema hivi…


Jaji: Kwa namna hiyo basi ni Kweli Kwamba Kielelezo hakiwezi Kutolewa pasipo Amri ya Mahakama.
Kisha akasema hivi…
Kwa maoni yangu, jaji amekuwa very contradictory! Anasema “kielelezo kinaweza kutumika kwa kesi au mahakama zaidi ya moja”, hakusema kwamba hicho kielelezo kinatumika kwenye kesi zaidi ya moja au mahakama zaidi ya moja. Bali amesema “kinaweza”

Duh!
 
Je!Kwa maamuzi haya haki imetendeka na kuoneka kuwa imetendeka?
 
Jaji anatafuta kila njia ya kumfurahisha Samia. Labda pengine atabahatisha cheo kama mwenzake.

1) Jaji Mkuu - kada wa CCM aliyekuwa akishiriki vikao na Magufuli, Bashiru na Polepole
2) Msajili wa mahakama - TIS
2) Jaji Kiongozi - TIS
3) Jaji Tiganga - TIS (baada ya kesi lazima naye apewe cheo)
4) Wapo majaji wengine 8, wote waliteuliwa na marehemu kuwa majaji - TIS

Kesi ya Mbowe, haitasikilizwa na jaji yeyote wa mahakama, zaidi ya hawa maafisa wa TIS waliochomekwa mahakamani kuvuruga mfumo wa mahakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…