...Reexamination ya leo imekuwa fupi sana; nilitegemea mawakili wa serikali wangetaka ufafanuzi kutoka kwa shahidi kwenye yale maeneo "aliyoonekana ku-support" upande wa utetezi lakini wapi! Kwa mfano, nilitegemea maswali kama;
- ulimaanisha nini uliposema hukuona neno Sabaya kwenye extraction? (Sikusikia hilo swali).
- jana nilikusikia ukisema hukuona mipango ya vitendo vya ugaidi kwenye extraction yako; ulimaanisha nini wakati kesi hii ni ya ugaidi? (Sikusikia hilo swali).
- jana ulisema wewe ni askari polisi na kama ungeona mipango ya vitendo vya uhalifu ungeandika kwenye ripoti yako; mweleze mheshimiwa jaji ulimaanisha nini; (Sikusikia hilo swali)..
Hizo ni kati ya hoja za msingi zinazobeba shauri zima la uhalifu/ugaidi wa Mbowe na wenzake; badala ya kutaka ufafanuzi wa kina wanauliza maswali ya kijinga na kuomba shauri liahirishwe hadi kesho kwani leo hawana shahidi mwingine! Ok, waendelee kutafuna pa diemu fedha za serikali hazina mwenyewe.