Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na Wenzake. Tumaini Swila amaliza ushahidi. Mawikili wa Serikali wafunga Ushahidi. Jaji kutoa uamuzi 18/02/2022

Kwahiyo kwa waliositisha ushahidi ndio washindi?
Hapana- ndiyo maana jaji ameona aangalie yeye atoe uamuzi. Ili tuendele kuwa na kazi ya kufanya na kushinda mahakamani na kupata mihogo ya kukaanga na keki mara moja moja - Mbowe na wenzake waje wajitetee
 
Hapana- ndiyo maana jaji ameona aangalie yeye atoe uamuzi. Ili tuendele kuwa na kazi ya kufanya na kushinda mahakamani na kupata mihogo ya kukaanga na keki mara moja moja - Mbowe na wenzake waje wajitetee
Hayo mengien niyako baada ya kukosa hoja.
 
1400+ pages proceedings in two days!! Tena bila submission!! This better end with a no prima facie case ruling.
 
Hii nchi ina watu wajinga wetu sana. Comte ni moja wao. Jamaa nashindwa kujua anaamini jambo gani katika maisha yake. Amekuwa kama kondoo.
Familia yake ina shida sana kuwa na mzazi kama huyu.
 
Taratibu za mahakama tu!
Nikiwambia Kibatala bado sana kwenye sheria hamuelewi. Kwa mjibu wa sheria ya makosa ya uhujumu uchumi- NO CASE TO ANSWER - haina nafasi.
 
Hii nchi ina watu wajinga wetu sana. Comte ni moja wao. Jamaa nashindwa kujua anaamini jambo gani katika maisha yake. Amekuwa kama kondoo.
Familia yake ina shida sana kuwa na mzazi kama huyu.
soma hiyo sheria ya makosa ya uhujumu uchumi kama unaamni uko sawa
 
Wapi amesema hivyo lete hiyo hoja yake hapa tuone.
Jaji: Shahidi tunakushukuru kwa ushahidi.

Wakili Kidando: Baada ya ushahidi wa shahidi huyu wa kumi na tatu tunaialika Mahakama yako chini ya kifungu 41 (1) cha sheria ya Uhujumu Uchumi ione washtakiwa wote wanne wana kesi ya kujibu hivyo hatua nyingine kwaajili ya kujitetea ifuate kwa upande wetu tunafunga kesi hii.

Jaji: Mahakama imekubaliana na maombi ya upande wa mashitaka kufunga kesi hii.

Wakili Kibatala: Baada ya upande wa mashtaka kufunga kupitia kifungu hicho cha 41 tunaomba mahakama hii itupe nafasi ya kufanya mawasilisho ya mwisho.

Lakini pia tuna maombi mawili ombi la kwanza Mahakama itupe mwenendo wa kesi lakini pili tupewe nafasi yakufanya mawasilisho ya mwisho oral.

Jaji: Kwanini unataka kufanya mawasilisho orally.

Kibatala: Tulikuwa tumeshajadiliana mwanzoni na kunafaida fulani fulani tutazipata.

Wakili Nashon Nkungu: Kwa niaba ya mshtakiwa wa kwanza: Tunaomba mawasilisho ya mwisho tuyafanye kwa njia ya mdomo na kupewa mwenendo wa kesi.

Wakili John Mally: Niunge mkono hoja za mawakili wenzangu na kuomba kufanya mawasilisho ya mwisho kama kuna kesi ya kujibu au la.

Wakili Fredrik Khiwelo: Kwa niaba ya mshtakiwa wa tatu: Niungane na wenzangu lakini pia na mimi ningeomba kupatiwa mwenendo wa kesi kwaajili ya kufanya mawasilisho ya mwisho kwa njia ya mdomo.

Wakili Kidando: Tukirejea kifungu cha 41 bado upande wa mashtaka tunaomba kufanya kwa nija ya maandishi

Shauri hili ukizingatia limeanza Septemba mwaka jana hatujajua itachukua muda gani kupata mwenendo wa kesi.

Jaji: Hadi leo PS wangu ameshachapa kurasa 1,400 nikichanganya za jana na leo zinaweza kufika 1,600 nilikuwa nafikiria hapa nadhani nipatiwe dakika kumi tukajadiliane.

Mahakama imerejea baada ya majadiliano na mawakili wa pande zote.

Jaji:
Baada ya kusikiliza na kupitia hoja za pande zote mbili na kuzingatia kifungu cha 41 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, Mahakama hii itatoa uamuzi Februari 18, 2022 kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la saa nane mchana na washtakiwa mtaaendelea kubaki chini ya uangalizi wa Magereza.
 
Mkuu, unajua tena! Kesi ndani ya kesi zilikuwa nyingi, mpaka tunawasahau mashahidi waliopita!
Ila BOAZ, alihitahika sana!
Boaz kaingia mitini na kuleta mtafaruku mkubwa....


Mzee mzima na hadhi yake aje achezee maswali ya madogo kina John Malya.... Hata kama ni mimi walahi ningesepa. Bora lawama kuliko fedheha
 
..Jaji amekataa ombi la upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao kwamba Watuhumiwa hawana kesi ya kujibu.
 
Sheria bhaana.... Embu kuweni serious..

Kuuliza kituo cha puma kipo sehemu gani.. mwendokasi ipo wapi.

Ni kama mnapiga story.

Mnaleta siasa mnasema kibatala anapiga pin.

Defence artoney kazi yake ni kuweka dought upande wa mashitaka... Shitaka la mbowe sio la mashahidi....

Kesi za kigaidi hazina mambo ya common law system.
Hapo ni kutimiza wajibu ila kila kitu ni planned kama kuachiwa ataachiwa kama kupigwa pin atapigwa...

Ila sisi tulio kwenye nyuma ya keyboard hatutakiwi kubeza chochote... Hii sio siasa.

Tunakula tunapata muda wa kuchat kisa amani iliyotengenezwa na serikali iyo iyo inayomtuhumu mbowe gaidi.

Matukio ya ugaidi yapo duniani na anayefanya hatumjui...

Tuache vyombo vifanye kazi zake..
 
Aliyepeleka kesi kakimbia , Jaji anasema ataamua kama kuna kesi au la ijumaa , only 2 days to go , kurasa za maelezo ya kesi hiyo zilizochapwa ni 1500 , atazimalizaje kuzipitia , ikiwa maamuzi yenye mapingamizi ya kurasa 2 tu alitumia hadi wiki mbili kutoa maamuzi ?



 

Hujui na huijui sheria na mienendo ya kesi
 
Nikiwambia Kibatala bado sana kwenye sheria hamuelewi. Kwa mjibu wa sheria ya makosa ya uhujumu uchumi- NO CASE TO ANSWER - haina nafasi.
Mkuu kwani uamuzi wa jaji wa tar 18 unahusu Nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…