Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Nahisi watu wa Lowassa watakuwa advantage ya Magufuli...
 
wakuu nipo dodoma sasa hivi mji mzima umetapakaa mashimo marefu nafikiri kuna mgodi umeanzishwa hapa ama labda wazee wa "patachimbika akikatwa" wameshafanya yao
 

Tatizo lako umejaaa Udini,Ukanda ,Ukabila

Tanzania we are past that

Again uache tabia yako ya kukomaa kuaminisha kwamba una uhakika sana na Mambo.........Kumbe ni bendera
 
CCM wamekuwa mabingwa wa kuvunja katiba na kanuni walizojiwekea wenyewe. Wamekuwa wakifanya hivyo with impunity. Wa-CCM wamekuwa wakishadadia huo uvunjwaji wa katiba na kanuni walizojiwekea kwasababu uvunjwaji wa katiba na kanuni hizo ulikuwa unafanywa kuinufaisha CCM.

Wana-CCM hawakufahamu kwamba uvunjwaji wa katiba wa mara kwa mara ni sawa na kula nyama ya mtu. Kwamba mtu aliyezoea kula nyama ya mtu hataacha kamwe. Wana-CCM walifikiri kwamba nyama ya mtu ambayo CCM itaendelea kula ni nyama za wapinzani na Watanzania wasio wana-CCM. Wa-CCM hawakuamini kwamba ipo siku CCM pia itakula nyama ya wana-CCM wenzao.

Waliofikiri hivyo, they were myopic and terribly wrong. Kwani usiku wa kuamukia leo CCM imewadhihirishia kwamba yenyewe ni cannibal hata nyama ya wana-CCM inaweza kula.

Ukisoma Katiba ya CCM, kikao chenye mamlaka na uwezo wa kuchuja na kukata majina ya watia nia wa Urais wa JMT ni Kamati Kuu (CC). Katiba ya CCM inasema kwamba CC ndiyo yenye mamlaka ya kukata majina na kupendekeza majina yasiyozidi 5 kwenda NEC kwaajili ya kupigiwa kura.

Vikao vingine kama Kamati ya Wazee na Kamati ya Maddili havina mamlaka wala uwezo wa kukata hata jina la mtia nia mmoja hata yule wa STD VII, ingawa kigezo cha elimu alikuwa hakikidhi.

Kamati ya wazee na Kamati ya maddili vitawajadili watia nia wote na kutoa maoni na mapendekezo yao kwa CC. Majina yote na mapendekezo ya kamati ya maadili na Wazee yatapelekwa CC kwaajili kuwapata watia nia 5 watakaopelekwa NEC kupigiwa kura.

Lakini kama mlivyomsikia Nchimbi and Co. ni kwamba majina yaliyofika kwenye CC sio ya watia nia wote (38). Ni majina machache tu ndiyo yaliyopelekwa CC. Maana yake ni kwamba kuna majina mengine yalikatwa na kamati ya wazee na kamati ya maadili, kinyume na katiba ya CCM, kwani hivyo vikao viwili havina mamlaka ya kikatiba ya kukata hata jina la mtia nia mmoja.

Make no mistake mimi sina sympathy na hao waliokatwa kinyume na katiba ya CCM. Kwani CCM imekuwa ikifanya hivyo all long na hao wanaolalamika leo walikuwa wakishangilia kwasababu uvunjwaji huo wa katiba na kanuni ulikuwa unafanywa kwa wasio wana-CCM kwa malengo ya kuinufaisha CCM.

Mifano ipo mingi ya ujunjwaji wa katiba. Mfano miswaada ya gesi na petrol iliyopitishwa majuzi ambapo mafuta na gesi ni swala la Muungano hivo ilibidi lipitishwe na 2/3 wa wabunge kutoka Tanganyika na Zanzibar.

Wote tunafahamu ukiukwaji wa katiba na kanuni uliofanywa na Sitta kwenye BMK ambao umeishia kum cost kwenye mbio za Urais wa CCM, maana hata yeye hayumo kwenye 5 bora.

Last but not least, ule msemo aliotufundisha baba wa Taifa kwamba ukizoea kula nyama ya mtu hutaacha kamwe, sasa umetimia kwani CCM wamevunja katiba yao wenyewe tena kwa wana-CCM wenzao!
 
Kamanda hiyo ndiyo safu ya rais na waziri mkuu wa Tanzania.

Daa!!! Maana hiyo UKAWA wanapoteza muda wao bure.

Makamanda nadhani mmesoma huu ujumbe.
 
UKAWA naona bado mnaendelea kuwachambua wagombea wa CCM mtachagua wenyewe nani mnaweza kupambana naye.
Mbona wewe unapenda sana kumchambua raisi wako mtarajiwa Dr.Slaa au yule yupo ccm? mmeshanganyikiwa
 
Hapo kwenye rangi pananipa kicheko cha sipati picha ikiwa hivo...!!
Wakuu Mungu amesikia maombi yetu, UKAWA hiyooooo namuona Dr Silaa akipanga baraza la mawaziri Waziri Mkuu Mbatia, mwanasheria mkuu Tundu Lisu, Waziri wa ardhi Harima Mdee waziri mambo ya ndani Godbless Lema na....
 
Lowassa atulie, asubiri huruma ya Rais ajaye, ambaye Magufuli ana nafasi kubwa; labda akatwe mapema, asiingie tatu bora.
 
Nawashauri wana JF Msimuamini mtu anaitwa Pasco ni mwongo,mbahatishaji asiyeaminika na anayejifanya kuwa anajua sana

Ni mtu wa kuogopwa sana kama UKOMA

tayari ameshaanza kubadili mwelekeo..nimemwambia mahali kuwa huyo pombe wake urais atausikia tu..
 
Huyo membe nasikia ni ndugu na kikwete so wanataka kuridhishana.
 
Kwa msisitizo, rais bado ni Lowassa ila kupitia nje ya CCM, infact nashauri ndie awe mgombea wa UKAWA!.

Pasco

UKAWA wakiruhusu Lowasa akajiunga nao...Nitakuwa wa Kwanza kuwakataaa.....Nitapiga kampeni wasipewe kura

LOWASA ni Mwizi kila mtu anajua hilo...Ni MWIZI anayejitapa kwa WIZI wake
 
Kwa msisitizo, rais bado ni Lowassa ila kupitia nje ya CCM, infact nashauri ndie awe mgombea wa UKAWA!.

Pasco

Pasco unazidi kujishushia heshima humu Jf UKAWA mgombea uraisi ndani saa 24 tunamtangaza Lowasa labda aende ACT
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…