Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Nilishasema toka mwanzo CCM hata wangemsimamisha yule mkulima bado watashinda tu sababu UKAWA hamna mgombea makini Dr.Slaa atabikia kuwa rais kivuli tu.

Mawazo mfu haya.
 
Nape mkali jamani anaulizwa maswali na waandishi wa habari anawaambia wakitaka wakasome katiba ya chama inasemaje...

Kawa mkali kama Mbogo...


ukali wa nini sasa...si tayari mtu wake yumo tano bora na ndiye mshindi
 
Wote map.imbi hawafai...full stop...!!!

Lowassa ndio chaguo la watu...!!!

Sasa tunaelekea ukawa...bora tukose wote....CCM imejizika..!!!
 

Pen ya JK Sio ya 200 /=
 
Last edited by a moderator:
Wakuu hapa Dodoma ni kama kumepita ugonjwa wa mnyoofu sababu hali si muhali hata kidogo!

Watu wamenyong'onyea sana and keep my word CCM inaenda kupitia kipindi kigumu sana.
Kwanza nitangaze msimamo wangu kuwa sio shabiki wa CCM. Ningependa kuona CCM inapumzishwa angaa kwa muhula mmoja ili tujaribishe utawala mbadala na yenyewe ijifunze kuwajibika. Lakini kwa uamuzi wa kukata jina la mzee wa maamuzi magumu mapema ni hatua moja ya kihistoria katika uhai wa chama kwa kuzima utamaduni, tena utamaduni mbaya, ambao alikuwa ameuasisi kuwa ili ufanikiwe kuteuliwa ni lazima kwanza ufisidi (maana hatujawahi kuelezwa mzee wa maamuzi magumu hufanya biashara gani wakati toka akiwa kijana ni mtumishi wa umma) ili upate hela za kukufanya 'ukubalike', yaani ununue ukubalifu!!! Kuzima utamaduni huu kunaweza kuwasaidia kurejesha imani ya baadhi ya wanaCCM waliokuwa wameanza kukata tamaa kuwa wenye chama sasa ni vibaka.
 
walisema hawakukutana barabarani

Zaidi Lowasa alivokuwa bagamoyo akasema kwa kikwete pia ni kwake

Ile kauli niliitafakari sana.

Ina maana na Salma pia Ni wa kwake Lowasa

Hii post imenichangamsha asubuhi hii.
 
Katka kizaz changu pia nimeshudia mizengwe hii ktk siasa za tz, daah nitasimulia wajukuu wangu....
tusubr tuone kama wana plan B
 
waliokuwa wanasema patachimbika nasubir pachimbike, sasa naona kimyaaaa! walikopotelea hata sijui!
Halafu asubuhi hii wanakimbilia St Gasper Hotel wameenda kujipanga walete (sijui ni fujo huko NEC?)
Huli kundi la akina Kingunge, Nchimbi, Sofia, Kimbisa na team zao wataadhirika sasa hivi ni bora kukubali kushindwa maana zaidi ya hapo ni kipigo hakuna cha kuchimbika wala Balali kurudishwa
 
Sasa ngoja tuone nani mwingine anayekatwa leo.

Je mpinzani namba moja wa EL atapita?!!
 
Sasa roho yangu imetulia na hata nikinywa maji yanashuka. Sikuwa na raha tangu CCM waanze mchakato wao wa kumtafuta mgombea wao. Ingawa mimi si mmoja wao,utanzania wangu ulinifanya niogope na kusikitika kila wakati. Masikitiko yangu yalikuwa juu ya uelekeo wa Tanzania yangu.

Jamaa alipotangaza nia na kuchukua fomu,wasiwasi wangu ulizidi hadi kunikondesha. Sikuogopa jamaa kuwa atashinda kwenye uchaguzi hapo Oktoba. Niliogopa kumuona jamaa akigombea pamoja na makandokando yote aliyonayo. Nikaanza kusali na kuomba ili tuepushwe na dhahama hii kama nchi. Tumesikika na kusikilizwa.

Kimsingi,sasa nitashiriki uchaguzini kama mpigakura nikiwa na amani. Jamaa ameshakatwa huko huko kwenye chama chao. Vyama vyote leteni wagombea wenu lakini si jamaa. Jamaa hafai!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…