Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Kwani ungeondoa neno la kuniita "Mwehu" ungepata hasara gani?

Any way umeonyesha ni namna gani wazazi wako walivyo (mtoto umleavyo ndivyo akuavyo)

Kwani Engineer husomea masomo gani?
Mkuu achana naye huyo. Mkandarasi ni Contractor na anaweza kuwa mtu yoyote sio lazima awe amesoma masomo maalum. Ila Mhandisi ni Engineer naye inategemea ni Engineer wa nini. Kama ni wa barabara au umeme n.k itabidi awe amesomea masomo husika. Wewe hapa hukusema kuwa Magufuli ni Mhandisi yaani Engineer na matokeo yake jamaa amekurupuka akidhani kuwa Contractor ndo Mhandisi
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Anandika Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

❝
Katika Mkutano Mkuu uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma, Dk. Magufuli amechaguliwa kwa kura 1560 akifuatiwa na Asha-Rose Migiro aliyepata kura 702 huku Balozi Amina Salum Ali akipata kura 349.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Dk. Magufuli amepita kwa kura hizo kutokana na nguvu yake dhidi ya wagombea wengine.

“Hakukuwa na namna hapa kwa kuwa, wajumbe wanaamini katika mazingira haya magumu ya upinzani Dk. Magufuli anaaminika na kukubalika nje kuliko hawa wengine,” anasema mtoa taarifa na kuongeza;

“Baada ya kutemwa Membe (Bernard Membe) kwenye NEC kila mjumbe ambaye alikuwa upande wa Lowassa (Edward Lowassa) alipumua jambo lililomrahisishia Magufuli.”

Mkutano huo umehairishwa mpaka saa nne asubuhi, ambapo ndiyo muda ambao Dk. Magufuli ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na Waziri wa Ujenzi atatangazwa rasmi kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho.

Awali ndani ya ukumbi wa mkutano, kulidawa kuwepo kwa mpango wa wafuasi wa Lowassa kutaka kumpitisha Balozi Amina ili chama hicho kipate changamoto katika ‘kumuuza’ kwa wananchi ikiwa ni kulipiza kisasi kwa kukatwa mtu wao (Lowassa).

Katika Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, majina yaliyopitishwa yalikiwa ni Migiro, Magufuli, Balozi Amina, Membe na January Makamba.

Katika Halmashauri Kuu ya CCM yalipita majina matatu ya Dk. Magufuli, Dk. Migiro na Balozi Amina.

Magufuli mgombea Urais CCM | MwanaHALISI Online
big up tunaanza kufuta taratibu mifumo ya kibaguz eti rais hawez toka eneo flan au kabila fulani
 
aje magufuli aje migiro ukawa ushindi ni lazima sisi hatuangalii mtu tunaangalia na chama alichomo
kina ajenda gani??

ukawa tuna ajenda ambazo hata magufuli hawezi tia mguu hawazi kabisa kufurukuta

1. kufufua mchakato wa katiba mpya -rasimu ya warioba

2.kuimarisha muungano wa jamuhuri ya tanzania kwa muundo wa serikali tatu

3. kubana matumizi ya serikali -kusitisha ununzi wa magari na maposho yasiyo na tija

5. kufuta misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa pamoja na kufuta na kupunguza viwango vya kodi
kwenye bidhaa vifaa ya ujenzi kilimo viwanda na vyakula

6.kudhibiti matumizi ya dola na usafirishaji dola nje, pamoja na kupunguza inflation

7. kushusha kodi kwenye bidhaa za ujenzi

8. kutoa elimu bure mpaka chuo kikuu

9. kurudisha miswada yote iliyopitishwa kwa hati ya dharula ili ipite katika utaratibu wa kawaida ili ijadiliwe na bunge ipitishwe

10. kutengua mikataba17(MOU) ya kinyonyaji aliyoisani jk na wachina

11 kusitisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo ili kuimarisha bandari ya dar tanga na mtrwara

13.kupitia upya mikataba ya madini,mafuta na gesi na nakuifuta ilie isiyo na maslahi kwa nchi

14 mengine mtaongeze

kwa hayo niliyo yaainisha hapo juu sidhani kama yanaweza kuwemo kwenye ilani ya CCM ambayo kama magufuli ateuliwa kugombea uraisi itabidi ainadi,

kwa mantiki hiyo pamoja na uchapakazi wa maghufuli hizo ajenda hapo juu hawezi zigusa labda kama hajipendi,

kwa jinsi ninavyo wajua ccm kwenye ilani yao watakuja na ahadi za ulaghai, kama kuongeza mishahara, kujenga barabara, kununua meli, na vivuko

ajenda nzito zinzoweza inua uchumi wa nchi kwa miaka mitano hawawezi kuzikubali wakabaki salama
hizo ajenda zitawezekana tu tukiwapa nchi ukawa, kama mnampenda mghufuli mchukueni mkanyywe naye chai
 
Kwani magufuli lilikuwa ni Chaguo lenu kweli team Lowasa? Au nyie ndo mmeshindwa kupata mnachokitaka, Magufuli ni one of the loyal people to Kikwete, hamuwezi kusema Kikwete hajampata mtu wake, you must be Joking. Mngetoka na Amina Salum au Migiro tungejua kweli mmemnyima Kikwete Chaguo lake. Unachosema sasa ni kujitafutia faraja.
 
Mkijihusisha na Magufuli tunamkata pia...nyie mmeshapigwa chini katulieni.
Amina aliomba kura za EL hamjampa?
Team Lowasa wanangoja tu UKAWA watangaze mgombea wao. Wameapa kuwadhibitishia waliomkata EL kuwa wamefanya kosa kubwa! Bila EL hakuna CCM kushinda! Watamuunga mkono mgombea wa UKAWA kwa nguvu zote!!!!
 
ukijumlisha hizo kura zote unapata karibia 2600 na tumeambiwa wajumbe wapo 2400 na kidogo swali je mpk wenyewe wanajiibia kura?

umeonae raia wanapopata data at
a hawazchunguzz nao wanatupia tuuu kwa media
 
Kama mnavyofahamu kwa mara ya kwanza Tanzania tunaenda kupata RAISI engeneer. Iko wazi watu hawa hawana public speaking skills achilia mbali wao wenyewe kuandaa speech. hawana mbinu za kusoma audience wanayoihutubia kwa kuzielewa nyuso zao., na mengine mengi. Hivyo ni wakati muafaka kwa wahusika kumrejesha raisi huyu class akapige course ya COMMUNICATION SKILLS ili asije sababisha matatizo huko mbele. Natoa hoja.
 
Mheshimiwa Rais wa JMT Dr.John Pombe Magufuli, waziri mkuu Prof. Sospeter Muhongo, kitaeleweka tuu, kama HUTAKI acha! Haya ni majembe mawili tunayoyahitaji sasa na wakati huu!
Narudia, kama HUTAKI, acha!
 
CCM wamekwepa team Diamond na team Kiba......na ingewacost kudadadeki.
 
Kwani magufuli lilikuwa ni Chaguo lenu kweli team Lowasa? Au nyie ndo mmeshindwa kupata mnachokitaka, Magufuli ni one of the loyal people to Kikwete, hamuwezi kusema Kikwete hajampata mtu wake, you must be Joking. Mngetoka na Amina Salum au Migiro tungejua kweli mmemnyima Kikwete Chaguo lake. Unachosema sasa ni kujitafutia faraja.

Wewe humjui magufuli vizuri!
 
Magufuli sio presidential material, ni mkurupukaji. Wale wa kigamboni wajiandae kupiga mbizi
 
Back
Top Bottom