Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Hata kwenye daladala wamo kuonesha hakatwi.
1436538768349.jpg
 
Duuh hivi kwa attention yote hii kwa wa Tz kinachojili huko Dom kuna yoyote ambaye bado anaamini Rais ajaye atatoka UKAWA? Endapo CCM watakuwa kitu kimoja baada ya mchakato huu naamini bado wana nafasi kubwa ya kutoa Rais ajaye. My opinion.

Jiulize hilo, hii ina maana moja tu, wote pamoja na mapenzi yetu lakini tunatambua ukweli huu kuwa Rais atatoka hapo Dodoma kwenye mchakato huu.
 
Leo hii CCM itarudisha heshima kwa kukata mafisadi na kusafisha chama, nguvu ya pesa si kila kitu!!
 
Hadi sasa jibu halijapatilana baada ya ubishani mkali ndani ya MCC,kikao kilichoishia saa tisa jana usiku kilikuwa kinamuomba EL awe makamu wa president ili Augustino Mwezi huu awe Rais
Hongera Lowasa

haa haa toka ugombea urais mpaka umakamu wa rais duh. kwani makamu wa rais anachukuliwa yeyote yule bila kuangalia sifa?
 
Ila chief Iyo account ya Instagram Nina mashaka nayo....

Ni kweli, hailekei kuwa yake. Ni mbinu za wapinzani wake kama zilivyo za kwake. La msingi EL OUT!

Sasa mchakato na uanze. Labda aende kwa Zitto lakini atakuwa na wasiwasi.
 
UKAWA wanakesha kufuatilia mchakato wa CCM wamesahau kabisa kama kwao wana mgombea urais.

Ritz pamoja na ubishi humu ndani,lakin kila mmoja hapa anajua Rais anatoka CCM ndio maana wote tupo hapa, na usidhani ni wapenzi tu, ata Dr Slaa hawezi kulala mpaka ajue Dodoma kumeendaje.
 
Jamani utabiri wa Maalim Hassan Hussein Yahaya, unatimia. Kuwa Rais atakuwa na mchanganyiko wa dini mbili. Had wakati huu nasema kwa herufi kubwa JAJI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.

huyo atachaguliwa zanzibar na umagambani. hatuwezi chagua rais wa tanganyika toka nchi jirani kamwe.
 
Wakuu habari,

Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.

Karibuni sana.

===================

Updates;

1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano
na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

Wewe muongo hauko kwenye kamati wala nini
 
Back
Top Bottom