Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Lazima ana kundi ila halijawa open
Mkuu,
Ninaposema hana kundi haina maana hata familia yake haiko nyuma yake.

Ninapongelea makundi ndani ya CCM ninatoa kioo cha hali halisi ambayo imeigawa CCM.

Ukubwa wa kikundi chake utaongezeka watakapoenda kwenye NEC kwa sababu wale ambao walikuwa kwenye vikundi vya wagombea waliokatwa wataanza kutafuta sehemu ya 'kujikunyata'.

By the way, ulimuona wakati anatafuta wadhamini ndani ya CCM?
 
Mkuu Nimechoka Wewe Acha Tu Na Huwezi Amini NINAUMWA Na JINO Pamoja Na FIZI Lakini Nimejikaza Tokea Asubuhi Hadi Sasa Saa 9 Kasoro 20 Hii. Naomba Ruhusa Yako / Yenu Nipumzike Sasa. Nawapongeza Wale Wote Tulioanza Kuchangia Uzi Huu Tokea Kukuche Hadi Sasa Kwani Wote Mmeonyesha UKOMAVU Na UVUMILIVU Bila Kusahau UZALENDO Wa Hali Ya Juu Sana Na Wale Pro Lowassa Poleni Sana Hii Ndiyo Siasa ( Leadership Hazards ) Hivyo TUVUMILIANE Tu Na TUSINUNIANE Humu Jamvini. Binafsi Nawapendeni Nyote Japo Najua Kuna Niliowakwaza Hapa Na Pale Hivyo NAWAOMBENI Radhi Sana Kama Siyo Msamaha. Alamsiki Guys!

Ok poa Mkuu pole sana kwa jino,pumzika salama.
 
na mwambie tu kuwa kuna kila dalili asha rose migiro akapata political advantage hapa na kuibuka mgombea rasmi wa ccm na kuna kila uwezekano tukaongozwa na mwanamke this time. Why? Team lowassa hawawezi kukubali kumpa nchi magufuli kwani wanajua akichukua nchi atawatesa hivyo hawamwamini totally na hawamtaki kabisa isipokuwa system, wazee wote wa ccm kuanzia mwinyi, mkapa, jk ( japo kidogo ), mangula, msekwa na mawaziri wakuu wastaafu karibia wote wanamtaka dr. John pombe magufuli na team lowassa hawawezi kukubali kumpa nchi mbaya wao bernard membe ( ambaye kwa kiasi kikubwa sana anasapotiwa na jk pamoja na familia yake nzima ili aje kulinda maslahi ya jk binafsi na wanafamilia wake ) kwani wanajua kuwa atawamaliza kwa visasi hivyo watatumia ushawishi wao wote ili wampigie kura mama dr. Asha rose migiro na watasaidiwa mno na katibu mkuu wa ccm abdularhman kinana. Hivyo basi kwa mazingira hayo na labda nguvu ya ziada itumike tu ili magufuli awe rais ila naiona njia ni nyeupe kwa mama asha rose migiro kuwa mgombea rasmi wa ccm isipokuwa huyu mama nje ya ccm hauziki vilivyo na mapungufu haya ndiyo yatafanya upepo baadae ubadilike na magufuli apitishwe kwani kiuhalisia ndiye mtu pekee si tu anakubalika bali anaogopwa na anaheshimiwa sana hata na wapinzani japo wawili hao kama binadamu hawakosi mapungufu yao na kwa uzuri ni kwamba yanarekebishika. 60% dr. Magufuli na 40% dr. Migiro. Huo ndiyo mtazamo wangu mdogo na alamsiki nyote.
membe ndiye atapitiashwa na chama na si vinginevyo!
-mark my words.
 
Ni Rasmi Sasa Kuwa Lowassa Amekatwa. Mtakao Niamini Vizuri Na Mtakaoona Natania Shauri Yenu Na Nyie Watu Wa Team Membe Hata Yeye Pia Hayupo Na Amekatwa. Taarifa Kamili Ni Kuanzia Saa 7 au Saa 8 Usiku Na Wanafanya Hivi Kwakuwa Kutakuwa Hakuna Watu Wengi Pale Maeneo Na Ulinzi Usiku Huu Umeimarishwa Maradufu Kupambana Na Wale Wahuni Wa Lowassa Waliopanga Kufanya Vurugu. Sasa Kikao Cha Kuwatafuta 3 Bora Kinaendelea Na Wakimaliza Tu Kuwapata Nape Atazungumza Na Waandishi Wa Habari Ambao Wameweka Kambi Hapo Hapo Ukumbini. Narudia Tena Kusema Si Lowassa Wala Membe Aliopita 5 Bora Na Timu Ya Lowassa Inataka Kufanya UMAFIA Kwa Kuhakikisha Kuwa Asha Rose Migiro Anapeta Katika 3 Bora Ili Wapige Kura Za Maruhani ( Za Kukomoana ) Ili Mwanamke Achukue Nchi Ila Wazee Wanajitahidi Kuhakikisha Nchi Anakabidhiwa Magufuli au Mwandosya au Sitta Na Katika Umakamu Imeshaamriwa Awe Jaji Ramadhan. So Far Hii Ndiyo Latest Yangu Kwenu Na Nina Uhakika Nayo 100%.

Hv mnatoaga wapi ujasiri wakuandika uwongo namna hii ilhali ukijua kwamba ukweli utajulikana muda mfupi mbeleni??? We need to change
 
na mwambie tu kuwa kuna kila dalili asha rose migiro akapata political advantage hapa na kuibuka mgombea rasmi wa ccm na kuna kila uwezekano tukaongozwa na mwanamke this time. Why? Team lowassa hawawezi kukubali kumpa nchi magufuli kwani wanajua akichukua nchi atawatesa hivyo hawamwamini totally na hawamtaki kabisa isipokuwa system, wazee wote wa ccm kuanzia mwinyi, mkapa, jk ( japo kidogo ), mangula, msekwa na mawaziri wakuu wastaafu karibia wote wanamtaka dr. John pombe magufuli na team lowassa hawawezi kukubali kumpa nchi mbaya wao bernard membe ( ambaye kwa kiasi kikubwa sana anasapotiwa na jk pamoja na familia yake nzima ili aje kulinda maslahi ya jk binafsi na wanafamilia wake ) kwani wanajua kuwa atawamaliza kwa visasi hivyo watatumia ushawishi wao wote ili wampigie kura mama dr. Asha rose migiro na watasaidiwa mno na katibu mkuu wa ccm abdularhman kinana. Hivyo basi kwa mazingira hayo na labda nguvu ya ziada itumike tu ili magufuli awe rais ila naiona njia ni nyeupe kwa mama asha rose migiro kuwa mgombea rasmi wa ccm isipokuwa huyu mama nje ya ccm hauziki vilivyo na mapungufu haya ndiyo yatafanya upepo baadae ubadilike na magufuli apitishwe kwani kiuhalisia ndiye mtu pekee si tu anakubalika bali anaogopwa na anaheshimiwa sana hata na wapinzani japo wawili hao kama binadamu hawakosi mapungufu yao na kwa uzuri ni kwamba yanarekebishika. 60% dr. Magufuli na 40% dr. Migiro. Huo ndiyo mtazamo wangu mdogo na alamsiki nyote.
bernard membe ndiye atapitiashwa na chama na si vinginevyo!
-mark my words.
 
Sipati picha Wananchi wanapelekewa mtu wasie mtaka wampigie kura.

Wasiyemtaka kwani lini tuliwauliza wanamtaka nani?Lowassa alikamata television na magazeti, wananchi mtu pekee waliyekuwa wanamsikia ni Lowassa,wengine walikuwa wanaelezwa kwa ubaya sasa ulitegemea nin?

Sasa game tofauti kabisa, mgombea wa CCM atapata hiyo coverage ya chama tawala akienda na slogan ya Makongoro, tumewatimua vibaka...tumekirudisha chama chetu.Makongoro anapaswa awe kwenye timu ya kampeni,atafaa sana.
 
Wakuu habari,

Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.

Karibuni sana.

===================

Updates;

1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.

6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano
na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.

9. Update 22:55
CC bado inaendelea, sasa hivi watu wa catering wanawapelekea vyakula na vinywaji (Pengine ni daku ya leo kwa waliofunga?)

Julai 11, 2015:

1. Update 01:00
CC imemaliza kikao chake; Nape kakutana na waandishi na kuna tetesi kuwa kuna kundi lilikuwa linajipanga kufanya mapinduzi ya Mwenyekiti wa CCM. Aidha, Nchimbi na wenzake wawili wameondoka wakiwa wamejaa jazba na wameonekana kutokubaliana na maamuzi ya CC. Updates zaidi zinafuata...

2. UPDATE 01:20

Hatimaye 5 Bora imejulikana, ni:

1) Bernard Membe 2) John Magufuli 3) Asha Rose Migiro 4) January Makamba 5) Amina S. Ali

View attachment 267181

=> Kikao cha HALMASHAURI KUU YA TAIFA kimeahirishwa hadi kesho tarehe 11 Julai 2015 saa 4 asubuhi

-------

good Lowasa out
 
Nakumbuka kibonde alipaza sauti akasema SAFARI YA MATUMAINI!!!!! watu wenye shibe ya pesa wakajibu IMEANZA!!!
Nasikitia 4U movement.. yaani majungu yote yale..mapesa yote,.mafuriko ya wadhamini..lakini AMEKATWA! da CCM Wabaya wangemwambia mapema..naomba kujua kama ameshaenda ICU au bado. MUSSA ALLAN Mwalimu Julius OcampoR FOUR NA MR PRESIDENT jikaze ndio maisha
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom