Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

umenena mkuu chama kikongwe kama hiki ili kianguke ni lazima wakologane ila bado uwezo wa kutengeneza unafki bado wanao ,yaani ule unafki wa kusifiana kwenye majukwaa
Nchimbi , sophia na kimbisa warudishe pesa za fisadi la sivyo ......
 
Akiwa anahojiwa na Charles Hilali Kingunge amesema mazingira ya kuwakata baadhi ya wagombea yalijengwa mapema,na viongozi waliopo serikarini mapema kabisa.

Sasa maamuzi yanayo tokea na yatakayo tokea,yatatokana na kile ambacho kiliandaliwa toka mwanzo.

ni watu wajinga,wapumbavu na washenzi ambao wanaweza kuwaonea akina kingunge na lowasa HURUMA kwa sababu wote ni wana ccm ambao wameshiriki katika kuvunja sheria za nchi na katiba.

watu wa mashirika binahsi,NGO,na vyama vya upinzani wamekuwa wakilalamika juu ya huu uhuni wa kutofuata sheria na taratibu za nchi LAKINI akina kingunge,nchimbi,kimbisa na msindai, na wengineo wengi wamekuwa wakiunga mkono upumbavu wa aina hii

Ni kwa nini kingunge na wenzake hawajawahi kutoka hadhalani na kupinga kwa mfano ushenzi unaofanywa bungeni? au ni kwa vile maslahi yao yameingiliwa ndio maana leo wamekuwa wapinzani?

bunge la katiba walipindisha kanuni za bunge,miswada ya gesi na mafuta, na mikataba mingi iliyo iingiza nchi katika umaskini ilipitishwa na akina kingunge ,lowasa and company.

LOWASA +KINGUNGE+MGEJA,NCHIMBI SOFIA mkae mkijua kwamba ukisikia jilani yako ameingiliwa na vibaka ukakaa kimya ukidhani ni yeye tu aliumbwa kuingiliwa na vibaka ujua zamu inayokuja ni kwako.

Na hii ni PICHA kamili ya jinsi ccm inavyoendesha hii nchi ujanja ujanja

kazi kwenu maana mirija ya maziwa imekatwa
 
Wakuu habari,

Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.

Karibuni sana.

=================

Updates;

1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano
na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

😛7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.

9. Update 22:55
CC bado inaendelea, sasa hivi watu wa catering wanawapelekea vyakula na vinywaji (Pengine ni daku ya leo kwa waliofunga?)

Julai 11, 2015:

1. Update 01:00
CC imemaliza kikao chake; Nape kakutana na waandishi na kuna tetesi kuwa kuna kundi lilikuwa linajipanga kufanya mapinduzi ya Mwenyekiti wa CCM. Aidha, Nchimbi na wenzake wawili wameondoka wakiwa wamejaa jazba na wameonekana kutokubaliana na maamuzi ya CC. Updates zaidi zinafuata...

2. UPDATE 01:20

Hatimaye 5 Bora imejulikana, ni:

1) Bernard Membe

2) John Magufuli

3) Asha Rose Migiro

4) January Makamba

5) Amina S. Ali

View attachment 267181


3: Update 12:00

Nchimbi, Mkono na Kibajaji wamezuiwa getini wasiingie mkutanoni kisa hawana vitambulisho. Baada ya tafrani ya takribani robo saa wajumbe hao wameruhusiwa kuingia.

4: Update 12:15
Mwenyekiti wa CCM Taifa, mh. Kikwete amefungua kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (NEC) cha kuchuja majina matano nafasi ya kugombea Urais.

5: Update 12:51
NEC imemaliza kikao cha kupiga kura, Tatu bora inatangazwa hivi punde (Kama itatokea)


6: Update 13:05
Kikao cha Halmashauri Kuu kimepitisha jina la Dr. Shein kuwa mgombea wa Urais Zanzibar.

7.Update 13:25
Wanec wametoka nje, hawana imani na CC, wanahoji kwanini Membe apite 5 bora, Lowassa aachwe?. Wametishia kuifuta CC. Ngoma imeachwa wazee kina Mwinyi na Mkapa wamebaki wakishauriana na viongozi nini cha kufanya.

8. Update 13:33
Hali ni tete Dodoma, Wapambe wa Lowassa, Wametishia Amani, Wamejikusanya kwenye bustani ya Nyerere Squre Wanaimba. Tunamtaka Lowassa tunamtaka Lowassa...!!

9:Update 14:00
Mkutano umefunguliwa na Mwenyekiti wa chama Rais Kikwete na kuahirishwa baada ya Dakika saba kwa kile wanachodai ni kuruhusu watu wakapate Chakula cha mchana. Wakati Mwenyekiti wa Chama anaingia, Wajumbe wa NEC walimpokea kwa wimbo wa "Tuna imani na Lowassa" hadi rais anakaa wameendelea kuimba
.


10: Update 17:30
Mkutano wa NEC, wajumbe wanapiga kura hivi sasa kupata wagombea tatu (3) BORA. Mkutano mkuu wa Taifa Utaanza saa TATU usiku.

11: Update 20:00

Matokeo Top 3 ya Urais CCM (Jina/Kura):
Magufuli 290
Amina 284
Migiro 280
Makamba 124
Membe 120
naona muhindi na team nan c walikutana hapo jana
 
Mimi ningekuwa Lowasa, huu ni wakati mwafaka wa kulipiza kisasi. Nitafanya hivyo kwa kuhamia chama kingine. Sijui kama anajitambua kwamba ana majority ya kura ukilinganisha na hao vilaza waliobaki. Ahamie chama kingine kukimaliza chama kilichomaliza ndoto yake aliyoishi nayo au niseme malengo yake ya kisiasa yameyeyuka. Alijiudhuru uwaziri mkuu kumstahi mshikaji wake mnafiki. Hadi mtoto wa huyo mnafiki anafanya party ndani ya mfungo.
Lowasa, CCM si mamako, babako,mwanao au nduguyo wa damu. Wengi wamefaidi fadhila zako na wema wako lakini sasa wewe ni fisadi. Toka CCM, watanzania kwanza hawakitaki chama hiki!
 
Ni magufuri migilo name Amina Salem eee mungu mbariki john pombe magufuri aipeperushe bend era ya ccm
 
Magufuri ataitaji nguvu bungeni ili serikali ipelekwe puta
 
Back
Top Bottom