Yaliyojiri kesi inayomkabili Mbowe na wenzake leo Februari 4, 2022. Kesi imeahirishwa. Shahidi wa 13 kuendelea kutoa ushahidi Februari 7, 2022

Asante. Quorum ya public opinion tunafuatilia kwa making mchongo huu.
 
HAYA NI YA CHANZO KINGINE

Soma ushahidi wote hapa

Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo Ijumaa itaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi

Mahakama inatarajia kuendelea kusikiliza ushahidi wa shahidi wa 13 upande wa Jamhuri baada ya shahidi wa 12 Luteni Urio kumaliza kutoa ushahidi wake Februari Mosi

ADVERTISEMENT

Washtakiwa wameshafikishwa mahakamani

Washtakiwa wengine katika kesi ya hiyo ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling'wenya

Tayari washtakiwa na mawakili wa pande zote pamoja na Jaji Joachim Tiganga wameshaingia mahakamani

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji kwa nafasi ya pekee naomba kumtambulisha Wakili Alute Mugwai Lissu, Pamoja Kwamba hayupo katika Quorum yetu, lakini ni mgeni wetu wa pekee leo

Wakili Arute Mugwai Lissu: Mheshimiwa Jaji Kwa nafasi ya pekee nashukuru kuwepo mahala hapa na kusikiliza shauri hili

Jaji: Karibu sana

Jaji anaita washitakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo mahakaman
i

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na leo tuna shahidi mmoja, tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Shahidi wa 13 Tumaini Sostenes Swila anaongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando

Jaji: Majina yako

Shahidi: Naitwa Tumaini Sostenes Swila

Jaji: Umri Wako

Shahidi: Miaka 46

Jaji: Kabila lako

Shahidi: Mndali

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkristo

Jaji: kazi yako

Shahidi: Askari Polisi

Shahidi: Naapa mbele ya mahakama hii Kuwa ushahidi nitakaotoa utakuwa wa kweli, kweli tupu Eehee Mwenyezi Mungu nisaidie

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shahidi unasema unaitwa nani?

Shahidi: Tumaini Sostenes Swila

Wakili Kidando: Unafanya kazi gani?

Shahidi: Ni Askari Polisi

Wakili Kidando: Una cheo gani?

Shahidi: Mkaguzi wa Polisi

Wakili Kidando: Kituo chako cha Kazi?

Shahidi: Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Temeke

Wakili Kidando: Majukumu yako ni yapi

Shahidi: Majukumu ni kuzuia kukamata na kupeleleza makosa ya jinai

Wakili Kidando: Kazi hiyo sasa umefanya Kwa muda gani?

Shahidi: Kazi hii nimefanya kwa miaka 24

Wakili Kidando: Taaluma ya Upelelezi umepataje?

Shahidi: Taaluma ya upelelezi nililipata kwa kuhudhuria kozi mbalimbali pamoja na uzoefu kazini

Wakili Kidando: Mkoa wa Kipolisi Temeke, Ofisi ya RCO. Elezea upo kwa muda gani ?

Shahidi: Nimekuwepo kwenye kituo cha RCO Temeke toka Oktoba 2015 lakini January 2020 nlipata uhamisho wa muda kwenda Makao Makuu Ndogo ya upelelezi Dar es Salaam.

Wakili Kidando: Baada ya kupata uhamishoni, Ieleze mahakama ulikaa kwa muda gani?

Shahidi: Kulikuwa na kazi mbalimbali zinazofanya pale na baada ya muda nikatakiwa kurudi kituo changu cha kazi.

Wakili Kidando: Na wakati Unapata uhamishoni wa muda, kwenda Ofisi Ndogo ya Upelelezi, ni shughuli gani ulikuwa unafanya?

Shahidi: Katika ofisi ya DCI nlikuwa nafanya kazi katika Kitengo X kinachojishughulisha na makosa yanayotishia usalama wa nchi pamoja na ustawi wa Taifa.

Jaji: Rudia Kitengo gani

Shahidi: Kitengo X

Jaji:Unaweza ku Spell

Shahidi: X ya herufi

Wakili Kidando: Hebu elezea mnamo Tarehe 14 Julai 2020 ulikuwa wapi na unafanya nini

Shahidi: Julai 14,2020 nilikuwa katika ofisi za DCI makao Makuu Ndogo Dar es Salaam nikiendelea na shughuli zangu nilipokea wito wa simu kutoka kwa katibu muktasi akinitaka nifike ofisi za DCI wakati huo alikuwa Afande Robert Boaz

Wakili Kidando: Baada ya Kupokea wito huo ulifanya nini

Shahidi: Nilienda ofisini kwa DCI Boaz na kumkuta na Ramadhani Kingai na ilikuwa saa 4 asubuhi

Wakili Kidando: Baada ya Kukutana DCI pamoja na Kingai nini kiliendelea

Shahidi: Baada ya kuwakuta pamoja, Kamishna Boaz alinitaka nipokee maelekezo kutoka kwa Afande Kingai Kamishna msaidizi wa Polisi

Shahidi: Nilitoka ofisini kwa Kamishna Boaz na kwenda kukaa pamoja alinipa maelekezo akinitaka kufungua jalada la uchunguzi akiwa ameshaandika kwenye karatasi iliyokuwa inaeleza Julai 14,2020 majira ya saa 2:30 asubuhi DCI Robert Boaz alipokea taarifa Kutoka kwa Luteni Urio za kuwepo kwa kundi linaloratibiwa na Freeman Aikael Mbowe likitaka kufanya vitendo vya kihalifu.

Shahidi: Vitendo hivyo ni kutaka kulipua vituo vya mafuta, kulipua masoko, maeneo yenye mikusanyiko ya watu, kukata miti mkubwa kwenye barabara kwa lengo la kuzuia magari yasipite.

Shahidi:kufanya maandamano nchi nzima na kudhuru viongozi wa Serikali kwa lengo la kuleta taharuki nchini na kufanya nchi isitawalike.

Shahidi: Mataendo hayo yalipangwa kufanyika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, na Kilimanjaro

Wakili Kidando: Endelea Kueleza Kilichotokea baina yako na Kingai

Shahidi: Baada ya kunipa maelezo hayo alitaka nifungu jalada na kulipeleka kwa DCI Afande Robert Boaz kisha Nilienda kwenye Ofisi wanapotunza kitabu hicho na kuweza kufungua jalada la uchunguzi lenye namba CID/HQ/PE/60/2020

Wakili Kidando: Elezea hizo taratibu za kufungua hilo jalada baada ya kuchukua hicho Kitabu

Shahdi: Unapofungua kina onyesha tarehe, muda, jina la mfunguaji na taarifa yenyewe.

Wakili Kidando: Wakati unafungua jalada hilo, mlalamikaji alikuwa nani?

Shahidi: Wakati nafungua mlalamikaji alikuwa DCI Afande Robert Boaz aliyekuwa akilalamikiwa ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili Kidando: Baada ya kufungua jalada hilo, Ulifanya nini?

Shahidi: Baada ya kufungua jalada hilo niliandika muktasari kwenda kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kuwa nimefungua jalada la uchunguzi dhidi ya Freeman Mbowe kutenda vitendo vya kihalifu kwa ajili ya uchunguzi na kulipeleka DCI.

Wakili Kidando: Baada ya Kupeleka jalada hilo nini Kilifuata

Shahidi: Julai 15,2020 majira ya saa tano nikiwa ofisini kwa DCI nilikabidhiwa jalada la uchunguzi ambalo lilikuwa limetolewa maelekezo na DCI Robert Boaz akitaka nimsaidie Afande Kingai aliyekuwa RCO Arusha.

Shahidi:Maelekezo yaliyotolewa yalikuwa ya namtaka Afande Kingai kuendelea kuwasiliana na mtoa taarifa ili aweze kumtafutia Freeman Mbowe watu waliokuwa wanahitajika kwa ajili ya kutenda vitendo vya kihalifu.

Shahidi: Pia alimtaka kuwatahadharisha watu hao kutoa taarifa ya vitendo vya kihalifu watakavyokutana navyo huko

Shahidi: Na watu watakaopatikana wakusanye taarifa na Kuzifikisha kwa Luteni Urio na yeye azifikishe kwa Afande Kingai.

Shahidi:Nilipokea maelekezo na kuwasiliana na Afande Kingai ambaye alikuwa Arusha na kunitaka nilihifadhi jalada hilo.

Shahidi:Baada ya Kuwasiliana na Afande Kingai na kumpata taarifa niliweza kukiri kupokea maelekezo na kumfahamisha kisha nikalihifadhi kwenye kabati ninalohifadhi vifaa vyangu vya kazi.

Wakili Kidando: Baada ya mawasiliano hayo na Kingai nini Kiliendelea?

Shahidi:Julai 18,2020 Nikiwa ninatekeleza majukumu yangu nilipokea simu kutoka kwa Afande Kingai akinijuilisha Denis Urio ameshapata vijana wa kuwapeleka kwa Freeman Mbowe na kunitaka nikafungue jalada la kesi kwenye kituo cha kati Dar es Salaam.

Wakili Kidando: Unamaanisha nini ukisema kufungua jalada la kesi

Shahidi: Ni Jalada ambalo linafunguliwa katika Report Book tofauti na lile jalada la upelelezi na linafunguliwa katika Vituo Vya Polisi

Shahidi: Jalada ambalo linafunguliwa katika kituo cha polisi ni tofauti na jalada la uchunguzi.

Shahidi: Baada ya kufungua niwasiliane na Mkuu wa Upelelezi Ilala ili aweze kulihamisha jalada na kulipeleka kwenye Ofisi ndogo za DCI, Dar es Salaam

Shahidi: Nilifika kituo cha polisi cha kati nikafunga kama niliyokuwa nimeelekezwa na Afande Kingai mlalamikaji akiwa DCI Robert Boazi.

Jalada hilo nililifungua kati ya Mei na Julai 2020 linalosema makundi ya watu yamepanga kufanya vitendo vya kigaidi katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo lakuleta taharuki nchini na nchi isitawalike.

Aidha nimefungua kufuatia taarifa ya Afande Kingai akinitaka nisiandike jina la mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe ili kuzuia uvujaji wa taarifa kwani kama jina lingekuwepo angeweka kujua na kusitisha mipango alivyokuwa amepanga na wenzake.

Wakili Kidando: Kitu gani Kingine kiliendelea

Baada ya kufungua jalada lenye namba CD/IR/2097/2020 Nilimjulisha Kaimu mpelelezi Fadhil Bakari. Nilimjulisha jalada hilo linataakiwa kuhamishiwa ofisi ya DCI Dar es Salaam.

Wakili Kidando: Sasa elezea baada ya siku ya Tarehe 18 July 2020, Nini Kiliendelea?

Shahidi :Julai 27,2020 Nikiwa ofisi ndogo za Makao Makuu Dar es Salaam nilipokea jalada Kosa kula njama ya kutaka kufanya vitendo vya kigaidi na lilikuwa limetolewa maelekezo na DCI Robert Boaz akitoa maelekezo kwa Afande Kingai pamoja na mimi akitaka tuendelee na upelelezi wa kosa hilo.

Wakili Kidando: Sasa kitu gani kingine kiliendelea?

Shahidi: Nilimjulisha Afande Kingai kuwa nimepokea jalada kwa niaba yako na mimi ni msaidi wako katika kupeleleza jalada hilo

Shahidi: Aliniambia anawasiliana na mtoa taarifa atanipa maelekezo nini cha kufanya.

Shahidi :Nilikiri kupokea jalada hilo na ilipofika Agosti 6,2020 nikiwa hapa Dar es Salaam saa mbili usiku Nilipokea simu kutoka kwa Afande Kingai akinijuilisha kuwa ameshapata watuhumiwa wawili yuko njiani kuwaleta Dar es Salaam kwa ajili ya upelelezi zaidi na akifika atanijulisha.

Shahidi.:Agost 7,2020 majira ya saa 11 na saa 12 nilipigiwa simu na Afande Kingai alinitaka nikutane nae kituo cha kati saa moja asubuhi.

Wakili Kidando: Samahani Mheshimiwa Jaji naomba tukutane na wenzetu kuna jambo linalohusiana na mwenendo wa kesi hii.

Jaji:Kama muda gani hivi mnaona utawatosha.

Wakili Kidando:Kama dakika 10 au 15 hivi.

Jaji anatoa

Mahakama imerejea na pande zote ziko tayari kuendelea

Shahidi:Nilifika kituo cha kati kabla ya saa moja asubuhi na kumkuta Afande Kingai akiwa na askari wawili ambao siwafahamu mmoja nliyekuwa na mfahamu ni Jumanne Malangai na askari wengine nilio kuja kuwafahamu baadae Afande Mahita na Goodluck

Wakili Kidando: Unasema ulimkuta ACP kingai na ASP Jumanne, hivi ASP Jumanne yeye ulimfahamu vipi?

Shahidi: ACP Jumanne nilimfahamu zaidi ya miaka kumi iliyopita wakati akiwa anafanya kazi Mpwapwa.

Wakili Kidando: Sasa hawa wakina ACP Kingai na ASP Jumanne uliwakuta Sehemu gani pale Kituo cha Polisi

Shahidi: Askari hao niliwakuta nje ya kituo na baadae Afande Ramadhani Kingai alitaka nipokee simu ambazo zilikamatwa Moshi kutoka kwa watuhumiwa wawili.

Shahidi:Niliweza kupokea simu mbili moja ikiwa Itel nyeusi na nyingine Tecno nyeusi.

Shahidi: Baada ya kuzipokea Ramadhani Kingai akinitaka kuzihifadhi, pia alitaka nimkabidhiwe maelezo ya mashahidi yaliyoandikwa moshi pamoja na hati za kumchukulia mali.

Shahidi: Nilichukua na kwenda kuzihifadhi katika Ofisi ndogo za DCI iliyopo Makao Makuu madongo ya Polisi Dar es Salaam.

Shahidi: Afande Kingai pia alitaka nishirikiane na Afande Mahita na Goodluck kufuatilia taarifa za watuhumiwa ambao hawajakamatwa

Shahidi: Alielekeza tufuatilie taarifa za mtuhumiwa Halfan Bwire Hassan kwa taarifa ambazo zilikuwa zimepatikana

Shahidi: Na taarifa hizo alikuwa amepewa Inspekta Mahita na mimi nikaenda kuungana nao.

Shahidi: Watuhumiwa waliokuwa wamekamatwa ni Mohamed Abdillahi Ling'wenya na Adam Hassan Kasekwa ambao nilikabidhiwa simu zao.

Shahidi: Niliwafahamu watuhumiwa baada ya kukabidhiwa hati za upekuzi pamoja na simu lakini pia alikamatwa na bastola aina ya Luger yenye namba A5340.

Wakati huo asubuhi washtakiwa sikuweza kuwaona ila walikuwa kituo cha polisi cha kati Dar es Salaam.

Shahidi: Maelekezo tuliyopewa tulifuatilia maeneo mbalimbali kulingana taarifa tuliyopewa na ilipofika saa 5 asubuhi Afande Jumaanne alinitaka nirudi kituo cha polisi cha kati ili nimkabidhiwe maelezo ya washtakiwa waliokuwa wanahojiwa pamoja na Afande Kingai.

Shahidi: Katika ufuatiliaji tulifuatilia maeneo mbalimbali ikiwemo Sinza na Osterbay Coco beach, na wakati natakiwa kurudi kituo cha Kati nilikuwa maeneo ya Sinza.

Shahidi:Maelezo ya washtakiwa nilimkabidhi nikiwa kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

Shahidi: Baada ya kupokea maelezo hayo ya watuhumiwa nilienda kwenye Ofisi ya DCI, Dar es Salaam na kuyahifadhi kwenye jalada na kuyaweka kwenye kabati ninalohifadhi vitu.

Shahidi: Nilienda kukabidhi vielelezo kituo cha polisi kati kwa kuwa watuhumiwa walifikishwa pale na shughuli zote zikawa zinafanyika pale.

Shahidi :Tuliendelea Kumtafuta mtuhumiwa Hassan Bwire eneo la Temeke hadi saa 12 jioni tukaahirisha zoezi hadi siku iliyofuata.

Shahidi: Agosti 8,2020 majira ya saa nne asubuhi nikiwa katika ofisi za DCI, Dar es Salaam nilipigiwa simu na Afande Jumanne akinitaka kufika ofisi za kituo cha polisi kati kwa ajili ya kazi.

Shahidi: Nilifika baadaa ya muda mfupi nilimkuta Inspekta Mahita na Pc Goodluck kuwa wamepewa maelekezo na Afande Kingai ya kuwahamisha watuhumiwa Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya kutoka kituo cha polisi Kati na kuwapeleka kituo cha cha polisi Mbweni.

Shahidi:Tuliwachukua watuhumiwa kutoka mahabusu ya Polisi Central na kuwasafirisha kwa gari hadi kituo cha Polisi Mbweni.

Shahidi:Tulitumia gari ya Polisi ambayo Afande Kingai alikuja nayo kutoka Arusha aina ya Fortuner.

Shahidi:Kituo cha polisi Mbweni Kipo Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Wilaya ya Kawe.

Shahidi: Zoezi la kuwaamisha watuhumiwa liliongozwa na Afande Jumanne, Inspekta Mahita na constebo wa polis Goodluck na mimi pia nikishiriki

Shahidi:Tulichukua muda usiozidi saa moja tukawa tumefika kituo cha Polisi Mbweni kisha tukawaingiza washtakiwa kwenye chumba cha mashtaka.

Shahidi:Baada ya kuwakabidhi watuhumiwa tuliendelea na zoezi la kuwatafuta watuhumiwa wengine ambapo Afande Goodluck alikuwa na taarifa za mtuhumiwa Halfan Bwire na zoezi liliendelea kwa siku nzima hadi saa moja usiku.

Shahidi: Ilipofika saa moja jioni Afande Jumanne alituambia tusitishe zoezi hadi siku inayofuata.

Shahidi: Agost 9,2020 nikiwa kwenye majukumu mengine kituo cha Kati Dar es Salaam nilipigiwa simu na Afande Kingai akinijuilisha kuwa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa Halfan Bwire Hassan akiwa na simu mbili na kunitaka nisiondoke kituo cha Kati ili wafike na kunikabidhi simu hizo.

Shahidi:Majira ya saa tatu usiku Afande Kingai alifika akiwa pamoja na Afande Jumanne, Inspekta Mahita pamoja na Constebo Goodluck.

Shahidi: Baada ya kufika alimueleza constebo wa Polisi Goodluck anikabidhi simu mbili.

Shahidi: Ya kwanza ni Simu ndogo ya gold na tekno ambayo ni smart Phone yenye rangi ya blue na ikiwa na kava jeusi na baada ya kumkabidhiwa nilienda kuzihifadhi ofisini kwangu kwenye kabati la chuma ninapo hifadhi vifaa vyangu vya kazi.

Wakili Kidando: Sasa ni shughuli gani nyingine iliendelea?

Shahidi: Afande Kingai alitaka niziandikie barua kwa ajili ya kupeleka kwenye maabara ya kisayansi ya uchunguzi wa makosa ya kimtandao.

Shahidi: Agosti 10,2020 Afande Kingai aliniambia ameshawasiliana na Luteni Denis Urio Afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuandika maelezo yake.

Shahidi: Niliwasiliana na Luteni Urio na Agost 11,2020 alifika kwenye Ofisi ya DCI na kuweza kuchukua maelezo yake.

Shahidi: Alifika majira ya asubuhi nikaweza kuandika maelezo yake kwa takribani saa zima na wakati naandika maelezo yake aliieleza kuwa alikuwa akiwasiliana na Freeman Mbowe kwa njia ya Telegram kwa namba 07199933386 na pia alinitajia namba yake aliyokuwa akifanya nayo mawasiliano ni 0787555200 na nyingine ni 0754612518 namba nyingine ya Freeman Mbowe 0784779944.

Shahidi: Nilimtaka anikabidhi simu aliyokuwa akifanya nayo mawasiliano aina ya Tecno kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kisayansi.

Shahidi: Aliniomba atoe line ya Vodacom ili anikabidhi siku inayofuata na simu nyingine alizokuwa anafanya nazo mawasiliano na Freeman Mbowe na nikamkubalia kwa kuwa mawasiliano ya Telegram hayabaki kwenye sim card bali kifaa kinachotumika kufanya mawasiliano.

Shahidi: Niliandaa hati ya makabidhiano kwa ajili ya kupokea simu ikionyesha unatoka kwa nani aina ya simu na IMEI zake.

Shahidi: Kwenye hiyo hati pia nilisaini na yeye pia kusaini.

Shahidi: Kuhusu simu nyingine alisema ziko nyumbani na kuhaidi kuzileta siku inayofuata.

Shahidi: Agost 12,2020 Luteni Urio alifika ofisi za DCI majira ya asubuhi na kunikabidhi simu tatu moja ikiwa Samsung nyeupe nyingine ni Techno C9 nyeusi, na Intel ya bluu.

Shahidi: Niliandaa hati ya makabidhiano kila hati ikionyesha aina ya simu na IMEI zake,

Shahidi: Jumla ya simu nne nilipokea kutoka kwa Denis Urio na mara baada ya kuzipokea niliziweka alama kwa kila simu kwa lengo la Kuzitofautisha ili ziwe na utambuzi.

Shahidi: Baada ya kuziweka alama nlienda kuvihifadhi katika ofisi yangu ndani ya kabati la chumba ninalotumia kuhifadhi vifaa vyangu vya kazi.

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji bado tunaendelea na maswali na ule muda wetu wa kubreaki umewadia naomba tubreaki tukirudi tutaendelea.

Wakili Kibatala:Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi.

Jaji: Basi tunabreak kwa dakika 45 hadi saa 7:45 tukirudi tutaendelea.

Mahakama imerejea kwa mara ya Pili baada ya break ya dakika 45

Jaji: Nakukumbusha shahidi upo chini ya kiapo

Shahidi: Sawa

Shahidi anaendelea kuongozwa kutoa ushahidi na wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando…..

Wakili Robert Kidando: Ulikuwa ukiieleza Mahakama jinsi gani ulivyokabidhiwa simu kati ya tarehe 12 Agosti 2020 Je, ulikuwa na idadi ya simu ngapi mpaka siku hiyo?

Shahidi: Hadi Agosti 12, 2020 nilikuwa nimeshapokea jumla ya simu nane zikiwemo simu 4 kutoka kwa Denis Urio, 2 za Bwire na simu moja kutoka kwa Adamu Kasekwa na Mohamed Ling'wenya.

Shahidi: Simu hizo nikiziona leo naweza kuzitambua kwa rangi, namba ya jalada, namba ya kesi, aina ya simu, kituo ambacho nimefungulia jalada la kesi, aina ya kosa na IMEI zake.

Shahidi: Pia zina majina ya watuhumiwa ambao ni Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa, Mohamed Ling'wenya.

Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba vielelezo ( Simu nane).

Jaji: Sawa

Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba kumuonyesha shahidi vielelezo hivyo na kama unavitambua basi uieleze Mahakama.

Shahidi anavifungua vielelezo hivyo vilivyowekwa kwenye mfuko na kutoa simu moja baada ya nyingine na kisha kuanza kukagua simu moja baada ya nyingine.

Shahidi: 7/8/2020 nilipokea simu Aina ya Itel na nimeitambua, inaonyesha namba ya jalada, jina la mtuhumiwa ni Adam Kasekwa, IMEI ipo, simu rangi yake ni nyeusi,

Shahidi: Simu nyingine niliyoipokea 7/8/2020 ni Techno rangi yeusi ambayo nimeitambua kupitia label ina kielelezo, namba ya jalada, pia imeandikwa aina ya simu, majina ya mtuhumiwa ambayo ni Mohamed Ling'wenya, IMEI namba kwenye simu hii imefutika.

Shahidi: Simu nyingine ya Bwire ni aina ya Techno, nimeitambua IMEI yake, namba ya kesi.

Shahidi: Tarehe 11/8/2020, nilipokea simu aina ya Techno yenye IMEI namba, kutoka kwa Luten Denis Urio, kesi namba yake ipo na jalada la kesi.

Shahidi: Tarehe 12/8/2020 na 13/8/2020 nilipokea simu 4 za Luten Urio.

Kidando: Mheshimiwa Jaji, shahidi ameweza kutambua vielelezo hivyo na tunaomba kuvirejesha mahakamani.

Vielelezo hivyo vilivyowekwa katika mfuko laini anapewa karani kwa ajili ya kuvitunza.

Shahidi: Kipindi simu hizo nakabidhiwa cheo changu kilikuwa ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi lakini kwa sasa ni Mkaguzi wa Polisi

Baada ya kuandaa hati ya makabidhiano, niliweza kuandika jina langu na cheo changu ambapo kwa kipindi hicho nilikuwa Mkaguzi Msaidizi, na Luteni Urio ambapo baada ya hapo nilisaini na yeye kusaini.

Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo(hati ya makabidhiano ya simu baina ya Swilla na Luten Urio).

Shahidi anapewa nyaraka hiyo aipitia.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji naomba mahakama ipokee kielezo hiki kiwe sehemu ya ushahidi katika kesi hii.

Nyaraka hiyo wanapewa upande wa utetezi ili waweze kuipitia.

Mawakili wa utetezi Kibatala, Mallya, Nkungu na Matata: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi juu ya nyaraka hii.

Jaji: Itakuwa kielelezo namba ngapi hiki? Jaji anauliza mawakili wa pande zote.

Kidando: Kielelezo namba 29.

Baada ya mahakama kukipokea kielelezo hicho(Hati ya makabidhiano ya simu za Denis Urio) anapewa nyaraka hiyo shahidi aisome mahakamani.

Shahidi anaanza kuisoma nyaraka hiyo

Shahidi: Nilijaza fomu hiyo kwa kuandika deshi katika hati hiyo kutokana na fomu hii, matumizi yake fomu au hati kwa ajili ya kujaza mali za watuhumiwa, lakini fomu hii nilimjaza Luten Urio ambaye alikuwa ni shahidi na sio mtuhumiwa.

Shahidi: Baada ya hapo nilivihifadhi katika kabati la chuma kwa ajili ya usalama wa vielelezo.

Shahidi: Ndani ya ofisi yangu hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwa anaitumia ofisi ile.

Shahidi: Baada ya kupokea simu tatu kutoka kwa Urio, nilimjulisha ACP Ramadhani Kingai kuwa nimeshapokea simu 8, ambapo 4 kati ya hizo ni za Luten Urio na zilizobaki zilikuwa za watuhumiwa.

Shahidi: Baada ya kumpa maelezo hayo, alinitaka niziandae simu hizo na kumkabidhi Constable wa Polisi Goodluck ili azipeleke kwa Kingai ili mimi niendelee na majukumu mengine.

Shahidi: Siku ya 13/8/2020 niliandaa barua ambayo ilisainiwa na Omari Msangi ambaye ni Kamishna Msaidizi wa Polisi aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi, ofisi ndogo ya Dar es Salaam.

Shahidi: Barua hiyo ilikuwa inaenda maabara ya uchunguzi wa Kisayansi, Kitengo cha uchunguzi wa kisayansi na Makosa ya Mtandao lengo ilikuwa ni kufanya uchunguzi wa simu 8.

Shahidi: Katika barua hiyo, simu hizo 8 nilizitambulisha kwa majina yake na IMEI yake.

Shahidi: Kwa kuwa simu hizo zilikuwa zipo kwenye flight mode ( alama ya ndege- ✈️) ilibidi niziwashe na nitumie fomula ili nipate namba ya utambuzi wa simu IMEI.

Shahidi: Nilitumia fomula ya *#06# kupiga na kupata IMEI, baada ya kuwasha simu.

Shahidi: Niliomba kupata mawasiliano yaliyotumika katika mtandao ya simu Aina ya Airtel, Tigo na Vodacom kupitia mawasiliano kwa njia ya Telegramu.

Pia niliomba nipatiwe taarifa ya mawasiliano ya miamala iliyofanyiwa kwa kupitia simu hizo.

Shahidi: Siku ya 14/8/2020 ACP Kingai alinitaka nifike chumba cha kutunzia vielelezo na niangalie kidaftari kilichokamatwa nyumbani kwa Bwire, ambacho Kingai alitaka kuangalia maeneo ya mchoro.

Shahidi: Hivyo, siku hiyo, 14/8/2020 majira ya saa 3 asubuhi nilifika Central Dsm, chumba cha kutunzia vielelezo na kumkuta mtunza vielelezo Coplo Johnstone ambaye aliweza kunionyesha vielelezo vilivyokamatwa kwa mshtakiwa Halfan Bwire Hassan vikiwa katika kitabu cha usajili Cha mwaka 2021.

Shahidi: Nilikipata kile kitabu na kuanza kukikagua

Wakati shahidi anaendelea kutoa ushahidi wake, ghafla amesimama wakili Peter Kibatala na John Mallya, ambao wamedai kuwa kidaftari hicho kilishakataliwa na mahakama hiyo kisitolewe maelezo na shahidi.

Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji, naomba shahidi azuiwe kuhusu kujadili content ambayo haipo Mahakamani, na hawezi kui- tender.

Jaji: Hapo shahidi anazungumza kile ambacho alikifanyia kazi na sidhani kama shahidi anazuiliwa kuelezea kitu ambacho amekifanyia kazi.

Jaji: Shahidi endelea.

Shahidi: Sawa, nilipopewa kile kidaftari nilienda kuangalia barabara ya Kilwa ambapo alikiita kituo cha mafuta cha GBP na Kisha nilienda kituo cha mafuta kilichopo Mivinjeni ambacho kilikuwa kinaitwa Puma.

Shahidi: Pia nilitembelea eneo la Kariakoo ambapo pembeni ya kituo cha mwendokasi kuna kituo cha mafuta, kiitwacho Big Born.

Shahidi: Pia nilitembelea eneo la Morocco ambapo kwenye barabara ya Mwenendo Kasi, katika makutano ya barabara ya Bagamoyo ambapo nilikuta kituon cha kuuzia mafuta kiitwacho Total.

Shahidi: Baada ya kujiridha kuwa maeneo hayo yanajihusisha na uuzaji wa mafuta, alinitaka siku inayofuata nichukue sampuli za maandishi za mshtakiwa.

Shahidi: Siku iliyofuatia tarehe 15/8/2020 majira ya saa tano asubuhi niliweza kumchukua mshtakiwa Halfan Bwire Hassan kutoka mahabusu ya kituo cha Polisi Chang'ombe na kumpeleka katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Kipolisi Temeke, ambapo niliweza kuchukua sampuli za maandishi kutoka kwa mshtakiwa huyo.

Shahidi: Baada ya kumfikisha ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, niliweza kuandika jumla ya karatasi nane za sampuli za maandishi, katika karatasi hizo 8 Bwire aliweza kuandika majina yake na kuweka udhibitisho huo kuwa maandishi hayo ni yake na kisha nilimrudisha Bwire kituo cha Polisi Chang'ombe.

Shahidi: Bwire aliandika sampuni hizo 8 ili kudhibitisha kama ni kweli kile kidaftari alichomatwa nacho kilikuwa cha kwake na kwamba kabla ya kuandika majina yake nilimfahamisha sababu ya kuchukua sampuli hizo na yeye alikubaliana na mimi.

Shahidi: Pia majira ya mchana nilichukua sampuli za majina ya mtuhumiwa Adam Kasekwa.



Shahidi: Kabla ya kumtoa Adamoo mahabusu, niliweza kumfahamisha kuwa Kuna kidaftari kilichokamatwa kwa Bwire kikiwa na maelezo na michoro, na kumueleza kuwa Bwire amekataa kuwa ule sio mwandiko wake.

Shahidi: Baada ya kumueleza hiyo Adam Kusekwa alikubali na kwenda kumchukua sampuli 8 kupitia katarasi nane.

Shahidi: Baada ya kurudisha Kasekwa, niliendelea na zoezi la kuchukua sampuni Mohamed Ling'wenya alikuwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Mbweni na kumueleza lengo langu na yeye alikubaliana na Kisha nikachukua sambuli zake.

Shahidi: Tarehe 16/8/2020, nilitakiwa kuandika jalada ili kulipeleka kwa DPP kwa ajili kulisoma na kuandaa mashtaka.

Shahidi: Tarehe 17/8/2020 nilifanya hivyo Kama nilivyoelekezwa na bosi wangu.

Shahidi: Tarehe 18/8/2020 nilielekezwa niandae jalada la mashtaka la Jeshi la polisi lenye mashtaka ya tuhuma za ugaidi.

Shahidi: Tarehe 19/8/2020 nilikuwepo Dar es Salaam, nilishiriki kuwapeleka mahakamani washtakiwa watatu katika Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Shahidi: Watuhumiwa hao ni Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya

Shahidi: Tarehe 19/9/2020 vielelezo hivyo nilienda kuvikabidhi kwa Koplo Hamisi.

Shahidi: 25/11/2020 nilipokea maelekezo kutoka kwa afande Ramadhani Kingai alitaka niandae barua 2.

Shahidi: Barua moja iende kwa mrajisi wa silaha ili tupata taarifa za mmiliki wa silaha kutoka kwa Adam Kasekwa ambayo ni bastola Aina ya Luger yenye namba A 5340.

Shahidi: Barua ya Pili, ilitakiwa iandikwe na kumkabidhi Ditektivu Constable Goodluck kwa ajili ya kupeleka silaha ambayo Ni bastola Aina ya Luger yenye namba A 5340 katika maabara ya uchunguzi kitendo Cha uchunguzi wa silaha na milipuko.

Shahidi: Pia barua hiyo ilikuwa inahusisha kumkabidhi risasi 3 zilizokamatwa kutoka kwa mtuhumiwa ( Adam Kasekwa).

Shahidi: Silaha hizi pamoja na risasi zilikuwa zimeandikiwa barua kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kujua kama silaha hiyo na risasi kama inafanya kazi

Shahidi: Shughuli ya kuandaa barua hizo, niliifanyia ofisi ya DCI, ofisi ndogo ya Dar es Salaam.

Shahidi: Barua zote hizo zilisainiwa na Ahmad Msangi, ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi.

Shahidi: Baada ya hapo barua na silaha hiyo na risasi zake zilipelekwa Dodoma katika Maabara uchunguzi wa silaha na milipuko kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Shahidi: Na nikiiona silaha hiyo naweza kuikumbuka kwa jina lake upande wa kushoto ambalo ni Luger na serial namba A5340.

Kidando: Mheshimiwa Jaji bado tuna maswali mengi na hapa muda umeisha, hivyo tunaomba ahirisho hadi Jumatatu, Februari 7, 2022 saa tatu asubuhi ili tuweze kuendelea na shahidi.

Jaji: Upande wa utetezi mnasemaje?

Kibatala: Hatuna pingamizi

Jaji: Kufuatia ombi lililolowasilishwa na upande wa mashtaka la kuomba kuahirisha kwa kesi hii, Mahakama inakubaliana na ombi hili na kuahirisha kesi hii hadi Jumatatu Februari 7, 2022 saa tatu asubuhi ambapo kesi hii itaendele.

Jaji: Shahidi nakuelekeza upo chini ya kiapo na unatakiwa siku hiyo uwepo mahakamani.

Jaji: Niwatakie jioni njema.








ps://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/ushahidi-wa-mkaguzi-wa-polisi-kesi-ya-kina-mbowe-huu-hapa--3705416
 
My dear friend unfortunately it does not work that way- brace for the bad new- Mbowe is going to jail.
Mkuu umejibu kiujumla,hujajibu hoja!Mimi siko kwenye hilo suala kuwa anaenda jela au vp!Mimi nazungumzia ushahidi unaohusu kielelezo kilichokataliwa na Mahakama!
 
Fanya utafiti.
Hapa hakuna haja ya utafiti wengine ni wakuwakaririsha tu maana hawaelewi

Imei namba inatolewa kwa kila SIM slot iliyopo kwenye simu, kwa maana hiyo imei namba lazima ziwe sawa na idadi ya line zinazokaa kwenye simu husika, usiulize tena kariri hivyo tu basi.
 
Upolisi ni kazi ya kijinga sana.

Hivi Serikali imekosa kupeleka huko brigadier general mmoja au hata colonel mmoja tu akawasimamie?

Wapuuzi sana
 
My dear friend unfortunately it does not work that way- brace for the bad new- Mbowe is going to jail.
Kwa kuandika hiki kiingeleza chako cha form one unajiona unajua sanaaa englsh eenh. Wewe utakuwa msukuma tu maana si kwa huu ushamba
 
Najiuliza: Kwa nini wanaleta mashahidi kama huyu? Alisema chochote kinachoweza kuthibitisha mashtaki? Nje ya kwamba aliambiwa Mbowe aliandaa Ugaidi?
 
Shahidi wa jana ilibidi aombe awe anatoka toka kwenda kwa short call na kuna wakati inaonesha aliomba tu ruhusa kabla Mh. Jaji hajamalizia kumjibu akawa ametoka mkuku!

Huyu n yule wa wakati ule hivi watakuwa na maradhi gani yanayowafanya wasiweze kustahimili kubana mkojo kizimbani mpaka wamalize. Wameshindwa kuiga mfano wa MaWakili ambao wao wakianza examination ni mpaka wanamaliza hamna kuomba ruhusa?

Lakini hata hivyo Acha ikae hivyo hivyo!
 
Kamwambie hivo aliyekutema leba sio Mimi chunga domolako fala wewe ,wanakukatikia

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Naona unazidi kupanic, ukitosheka kupanic basi ukapige mswaki maana hapo ulipo utakuwa unanuka sana, huku ukizungukwa na nzi! Pole sana punguani, taahira uliyezaliwa bila mpango!
 
Ni mlevi anakunywa mabia asubuhi ili aondoe uoga sasa kojo linakuja kila saa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…