Habari Wakuu,
Leo
04/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.
Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri kesi ya Mbowe 01/02/2022. Luteni Denis Urio amaliza kutoa ushahidi wake. Shahidi wa 13 kuanza 04/02/2022
Updates:
Jaji ameingia Mahakamani
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili:
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Ignasi Mwinuka
- Mawakili Wa Serikali Waandamizi na,
- Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili:
- Michael Mwangasa
- Gaston Garubindi
- Michael Lugina
- Sisty Aloyce
- Iddi Msawanga
- Maria Mushi
- Evaresta Kisanga
- Khadija Aaron
- Dickson Matata
- John Mallya
- Nashon Nkungu
Kibatala: Kwa nafasi ya pekee naomba kumtambulisha Wakili Alute Mughwai Lissu, Pamoja Kwamba hayupo katika Quorum yetu, lakini ni mgeni wetu wa pekee leo.
Wakili Alute Mughwai Lissu: Mheshimiwa Jaji Kwa nafasi ya pekee nashukuru kuwepo mahala hapa na kusikiliza shauri hili
Jaji: karibu sana
Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja, Tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea
Jaji: shahidi wa ngapi
Wakili wa Serikali: Mh Jaji Shahidi Wa 13
Shahidi: NAITWA Tumaini Sostenes Swila, miaka 46, Kabila mndali, dini mkiristo, kazi ni Askari Polisi
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii Kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, kweli tupu Eehee Mwenyezi Mungu Nisaidie
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shahidi Unasema Unaitwa nani
Shahidi: Tumaini Sostenes Swila
Wakili wa Serikali: Robert Kidando Unafanya kazi gani
Shahidi: Ni Askari Polisi
Wakili wa Serikali: Una Cheo gani
Shahidi: Ni Mkaguzi wa Polisi
Wakili wa Serikali: Kituo Chako Cha Kazi?
Shahidi: Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Temeke
Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni yapi
Shahidi: Ni Kuzuia, Kukamata, na Kupeleleza Makosa ya Jinai
Wakili wa Serikali: Kazi hiyo sasa umefanya Kwa Muda gani
Shahidi: Miaka 24
Wakili wa Serikali: Katika Shughuli hiyo ya Upelelezi, Kitu gani hasa unafanya
Shahidi: Shughuli Mbalimbali Katika Upelelezi, ikiwemo Kukagua Eneo la Tukio, Kuchora eneo la Tukio, Kuku Sanya Vielelezo, Kuhoji Mashahidi, Kukamata Watuhumiwa, kuwahoji Watuhumiwa, Kuandaa Barua Mbalimbali za Kuomba Uchunguzi wa Vielelezo, Kupeleka Vielelezo Maabara, Kuchukua Maandishi ya Sampuli za Watuhumiwa, Kuandaa Taarifa za Wapelelezi, Kusimamia Gwaride la Utambuzi wa Watuhumiwa, Kuwafikisha Watuhumiwa Mahakamani ikiwa ni pamoja na Kutoa Ushahidi Mahakamani
Wakili wa Serikali: Umesema Umekuwa Katika Upelelezi Kwa Miaka Mingapi
Shahidi: 24
Wakili wa Serikali: Taaluma ya Upelelezi Umepataje
Shahidi: Kwa kuhudhuria Kozi Mbalimbali pamoja na uzoefu Kazini
Wakili wa Serikali: Unasema huko Mkoa Wa Kipolisi Temeke, Ofisi ya RCO, Elezea upo Kwa Muda gani Katika Kituo hicho cha kazi
Shahidi: Nipo tangu OCTOBER 2015, Lakini Ulipofika Mwezi January Mwaka 2020 nilipata Uhamishoni wa Muda Kwenda Makao Makuu Ndogo ya Upelelezi, Jijini Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupata uhamishoni huo wa Muda, Ieleze Mahakama Ulikaa Kwa Muda gani
Shahidi: Nilianza Kufanya Kazi Ofisi ya Makao Mkuu ya Upelelezi toka January 2020 Mpaka August 2021 nikarudi Kituo Changu Cha kazi
Wakili wa Serikali: Na wakati Unapata uhamishoni Wa Muda, kwenda Ofisi Ndogo ya Upelelezi, Ni Shughuli gani ulikuwa unafanya
Shahidi: Nilikuwa Nafanya kazi Katika Kitengo X
Jaji: Rudia Kitengo gani
Shahidi: Kitengo X
Jaji: Unaweza Ku-spell
Shahidi: X ya herufi Wakili wa Serikali: Kitengo X kinajishughulisha na nini
Shahidi: Makosa yanayotishia Usalama wa nchi pamoja na Ustawi wa Taifa
Wakili wa Serikali: Katika Makosa yanayotishia Usalama na Ustawi wa Nchi, Kitu gani Kina fanyika haswa
Shahidi: Kina husika na Makosa yanayotishia Usalama Wa Nchi, Nchi Nzima
Wakili wa Serikali: Sasa Ukiwa hapo ulikuwa na nafasi gani?
Shahidi: Nilikuwa naendelea na Upelelezi pamoja na Makosa Mengine
Wakili wa Serikali: Hebu Elezea Mnamo Tarehe 14 July 2020 ulikuwa wapi na unafanya nini
Shahidi: Nilikuwa Katika ofisi Za Mkurugenzi Wa Makosa ya Jinai Nchini, Ofisi Ndogo za Dar es Salaam, Nikiendelea na Majukumu yangu Ndipo nilipopokea Simu Kutoka Kwa Katibu muhtasi Kutoka Kwa Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai Nchini, akitaka ni file katika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Nchini Wakati huo alikuwa Afande Robert Boaz
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Wito huo Ulifanya nini
Shahidi: Nilienda Moja kwa Moja Mpaka Ofisi ya Mkurugenzi Wa Makosa ya Jinai Nchini, Nikawakuta Afande Robert Boaz na Ramadhan Kingai
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Muda gani
Shahidi: Majira ya Saa 4 Asubuhi
Wakili wa Serikali: Ulichukua Muda gani Kufika
Shahidi: Ilikuwa kama Dakika 15 Kufika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukuta DCI pamoja na Kingai nini kiliendelea
Shahidi: Baada ya Kuwakuta Pamoja Kamishina ROBERT BOAZ wakati huo akiwa DCI alinitaka Kupokea Maelekezo Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai ambaye ni Kamishina Msaidizi wa Polisi
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa DCI Kukwambia Upokee Maelekezo hayo nini kiliendelea
Shahidi: Baada ya Kupokea Maelekezo hayo tukitoka Pamoja na Afande Ramadhan Kingai Kamishina wa Polisi, Ofisini Kwangu, Akanipa Maelekezo Ya Kufungua Jalada la Uchunguzi Maelekezo hayo alinipa takiwa tayari yameandikwa katika Karatasi
Yalikuwa yanaeleza kuwa Mnamo tarehe 14 July 2020 Majira ya Saa 2 na Nusu Asubuhi, Mkurugenzi Wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ROBERT BOAZ Kamishina Msaidizi Wa Polisi alipokea Taarifa Kutoka Kwa Luten Denis Urio, Juu ya Uwepo wa Kundi linaloratibiwa na Freeman Aikael Mbowe la Kutaka Kufanya Vitendo Vya Uhalifu.. Ambavyo ni Kulipua Vituo Vya Kuuzia Mafuta, Kuchoma Masoko Moto pamoja na Maeneo yanye Mikusanyiko wa Watu wengi, Kukata Miti Mikubwa katika Barabara Kuu kwa Lengo la Kuzuia Magari yasipite, Kufanya Maandamano Nchi Nzima yasiyokuwa na Ukomo, Na Kuwadhuru Viongozi Mbalimbali Wa Serikali.. Kwa Lengo la Kuleta Taharuki Nchini kufanya Nchi isitawalike..
Wakili wa Serikali: Elezea Kuilezea hiyo Taarifa
Shahidi: Na Matendo hayo yalipamgwa Kufanyika Katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro
Wakili wa Serikali: Endelea Kueleza Kilichotokea Baina yako na Kingai
Shahidi: Baada ya Kupokea Maelekezo hayo alinitaka nifungie Jalada Kisha nipeleke Ofisi Ya DCI, Nilienda Moja kwa Moja katika Ofisi Inayohusika na Kitabu cha Kufungua Majalada, Ofisi Ya Mnadhimu, Ambapo Nilienda na Kuchukua Kitabu hicho na Kufungua Jalada la Uchunguzi lenye Kumbukumbu namba CD HQ/PE/60/2020
Wakili wa Serikali: Elezea hizo Taratibu za Kufungua hilo Jalada baada ya Kuchukua hichi Kitabu
Shahidi: Kitabu Kile Kina onyesha Tarehe ya Kifungua, Muda, Jina la Mlalamikaji na Taarifa Yenyewe
Wakili wa Serikali: Wakati unafungua Jalada hilo, Mlalamikaji alikuwa nani
Shahidi: Mlalamikaji alikuwa Afande Robert Boaz Kamishina Wa Polisi na Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Nchini
Wakili wa Serikali: Nani alikuwa analalamikiwa
Shahidi: Mlalamikiwa katika Jalada hilo alikuwa ni Freeman Aikael Mbowe
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umefungua Jalada hilo, Ulifanya nini?
Shahidi: Baada ya Kufungua Jalada hilo, niliweza Kuandika Minutes Kwenda Kwa Mkurugenzi Wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, nikimkulisha Kuwa nimefungua Jalada la Uchunguzi dhidi ya Freeman Mbowe, Kwa Kutaka Kufanya Vitendo Vya Uhalifu, Kama ambavyo nimevitaja hapo Juu, nikaandika, Naleta Jalada Kwako Kwa Maelekezo zaidi
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umeandika hiyo Minute's Ulifanya nini sasa na hilo Jalada
Shahidi: Nilienda Moja kwa Moja Mpaka Ofisini Kwa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupeleka Jalada hilo nini Kilifuata
Shahidi: Siku ya Tarehe 15 July 2020 Saa 5 Asubuhi nikiwa Katika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai, Nilikabidhiwa Jalada hilo la Uchunguzi ambalo Kumbukumbu namba zake nilizitaja ambalo lilikuwa limetolewa Maelekezo na Robert Boaz Kamishina Wa Polisi na DCI Akinitaka nimsaidie Kamishina Msaidizi Wa Polisi Ramadhan Kingai Kufanya Upelelezi, ambaye wakati huo alikuwa ni RCO wa Arusha
Wakili wa Serikali: Maelekezo yaliyolewa kwenda kwa nani
Shahidi: Maelekezo Yakitolewa Kwemda Kwa Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi Pamoja na Mimi Kumsaidia Upelelezi
Wakili wa Serikali: Hayo Maelekezo ya Kumsaidia ACP Kingai Yalikuwa ni Maelekezo gani
Shahidi: Yalikuwa ni Maelekezo Ya Kutaka ACP kingai Kuendelea Kuwasiliana na Mtoa Taarifa ili aweze Kumtafutia Watu ambao Walikuwa Wanahitajika na Freeman Mbowe Katika Kutenda Vitendo hivyo Maelekezo Yalikuwa pia Kuwa Alikutana nao Watu hao, awape tahadhari ya Vitendo ambavyo wataenda Kukutana navyo huko
Wakili wa Serikali: Dhumuni hasa la Maelekezo hayo yalikuwa ni nini
Shahidi: kupata Taarifa na Kuwajua Watu Wanaoshirikiana na Freeman Mbowe, Na Pia Watu ambao Watakuwa wamepatikana Kutoka kwa Luten Denis Urio afikishwe kwa ACP Ramadhan Kingai Kisha na Yeye afikishe kwa DCI
Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kuwa Umepewa Jalada na Maelekezo hayo Ulifanya nini
Shahidi: Miliwasiliana kwa al Simu na ACP Ramadhan Kingai ambaye kwa wakati huo alikuwa Arusha, Baada ya Kumjulisha alisema lihifadhi Jalada hilo nitakupa Maelekezo
Wakili wa Serikali: Baada ya Sasa Kuwa Umemjulisha ACP Kingai, Nini Kiliendelea Katika Ushauri huo Shahidi Baada ya Kuwasiliana na ACP kingai na Kumjulisha Maelekezo ambayo yapo Katika Jalada na Yeye Kuniambia Kuwa ni hifadhi, Niliweza Kuandika Taarifa ya Kukiri Kupokea, KishaNika hifadhi Jalada hilo katika kabati langu la Chuma ambapo natumia Kuhifadhi Vifaa Vyangu Vya kazi..
Wakili wa Serikali: Baada ya Mawasiliano hayo na Kingai nini Kiliendelea
Shahidi: Mnamo Tarehe 18 July 2020 nikiwa naendelea na Majukumu Yangu katika Ofisi Ndogo ya DCI Nilipokea Simu Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi, akinijulisha kuwa Luteni Denis Urio tayari amepata Vijana Wa Kuwapeleka Kwa Freeman Aikael Mbowe Na akanitaka niende Kufungua Jalada la Kesi katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Ukisema Kufungua Jalada la kesi
Shahidi: Ni Jalada ambalo linafunguliwa katika Report Book tofauti na lile Jalada la Upelelezi na Linafunguliwa katika Vituo Vya Polisi Pia alini elekeza baada ya Kufungua Jalada hilo niongee na Mkuu Upelelezi Mkoa wa Polisi Wa Ilala aweze Kuhamisha Jalada hilo Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Nchini
Wakili wa Serikali: Wewe Ukafanya nini
Shahidi: Niliweza kwenda Kufungua Jalada hilo Kama nilivyo elekezwa na ACP kingai, Nika Fungua Jalada la Kutaka Kula Njama Kutenda Vitendo Vya Kigaidi
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Maelekezo hayo Shughuli hiyo Uliweza Kutekelezaje
Shahidi: Niliweza Kufika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Nika Fungua Jalada hilo, Mlalamikaji Robert Boaz Kamishina Wa Polisi, Jalada hilo alinielekeza Kufungua Kuwa Mnamo Mwezi kati ya May na July 2020 Kuna Kundi la Watu Wamepanga Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Katika Mikoa Mbalimbali Nchini, Kwa Lengo la Kuleta Taharuki, Na Nchi isitawalike Aidha nilifungua Taarifa hiyo Kufuatia Maelezo Ya ACP kingai ambaye alitaka nisiandike Jina la Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe Katika Taarifa hiyo, Ili kuepusha uvujaji wa Taarifa Kwani kama Jina lake lingekwepo katika Taarifa hiyo angeweza Kujua na Kusitisha Utekelezaji wa alilokuwa amepanga pamoja na Wenzake..
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kiliendelea Shahidi: Baada ya Jalada Kufunguliwa ambapo lilikuwa na Kumbukumbu namba CD/IR /2097 /2020 Nilimjulisha ambaye alikuwa kaimu Mkuu Wa Upelelezi Mkoa wa Ilala ambapo wakati huo alikuwa FADHIL BAKARI
Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kumjulisha ACP FADHIL BAKARI nini kiliendelea
Shahidi: Niliondoka na Kuendelea na Kazi Zingine
Wakili wa Serikali: Sasa Elezea baada ya Siku ya Tarehe 18 July 2020, Nini Kiliendelea
Shahidi: Mnamo Tarehe 27 July 2020 nikiwa Ofisi Ndogo ya Upelelezi Dar es Salaam Nilipokea Jalada lenye Kumbukumbu namba CD /IR/2097 /2020 Kosa Kula Njama za Kutaka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi
Jalada hilo lilikuwa limetolewa Maelekezo na Afande Robert Boaz Kamishina Wa Polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa Ya Jinai Nchini akitoa Maelekezo Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi Pamoja na Mimi akitutaka tuendelee na Upelelezi Wa Kosa hilo
Wakili wa Serikali: Sasa Kitu gani Kingine kiliendelea Shahidi: Niliweza Kumjulisha Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi, kuwa nimepokea kwa niaba yako Jalada Na mimi ni Msaidizi Wako katika Upelelezi Wa Jalada hilo
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumjulisha Kingai nini hasa kiliendelea
Shahidi: aliniambia Kuwa yeye anaendelea na Ufutailiaji na Mtoa Taarifa, atanipa Maelekezo ya Nini cha Kufanya
Wakili wa Serikali: Baada ya hapo sasa, Kitu gani hasa kiliendelea katika Jalada hili
Shahidi: Nilikiri Kupokea Jalada hilo Kisha nikalitumza katika Kabati langu la Chuma, Ilipo fika Tarehe 06 August 2020 Mimi nikiwa hapa Dar Es Salaam Majira ya Saa 2 Usiku, Nilipokea Simu Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akinijulisha Kwamba Tayari Wamekamatwa Watuhumiwa Wawili na Wapo Njiani Kuja nao Dar es Salaam kwa ajili ya Kuendelea na Upelelezi zaidi Akaniambia akifika atanijulisha..
Wakili wa Serikali: Baada sasa ya Kukupa Taarifa hiyo, Elezea Kama alilufamisha Kuhusu Watuhumiwa hao Wamekamatwa wapi na wakina nani
Shahidi: Alichokisema ni kwamba amekamata Watuhumiwa Wawili Katika Mji wa Moshi hakuniambia Majina
Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya ACP Kingai Kukupa Taarifa hiyo Shahidi: Ilipo fika Tarehe 07 August 2020 Majira kati ya Saa 11 na Saa 12 Alfajiri nilipigiwa Simu na Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akinitaka nikutane naye Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Mapema Saa 1 Asubuhi
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji samahani kabla ya kuendelea Kuna jambo moja naomba tukutane faragha na wenzetu kuhusu mwenendo wa kesi hii..
Wakili Peter Kibatala: Sawa mheshimiwa Jaji
Jaji: Kwa muda gani
Wakili wa Serikali: Kwa dakika 10 mpaka 15
Jaji anatoka Mahakamani (11:27 AM)
Jaji amerejea Mahakamani (11:37 AM)
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wa Jamhuri tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi tupo tayari Kuendelea
Jaji: sehemu ya Mwishoni alisema alieleza Kufika Kituo cha kati Kati ya Saa 11 na 12 Asubuhi
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Maelekezo Hayo wewe Ulifanya nini
Shahidi: Nilijiandaa Kwenda Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam ambapo Nilifika kabla ya Saa 1 Asubuhi
Wakili wa Serikali: Ulipofika hapo Ulifanya nini
Shahidi: Niliweza Kumkuta Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akiwa pamoja na Askari Wawili ambao siwafahamu na Mmoja nilikuwa Namfahamu ambaye ni ASP Jumanne Malangahe, Wale wawili Nilikuja kuwafahamu baadae ambao ni Inspector Mahita na Constable Goodluck
Wakili wa Serikali: Na unasema Ulimkuta ACP kingai na ASP Jumanne, hivi ASP Jumanne yeye Ulimfahamu vipi
Shahidi: ASP Jumanne nilimfahamu zaidi Ya Miaka 10 Wakati akiwa anafanya Kazi Mkoa wa Pwani
Wakili wa Serikali: Sasa hawa wakina ACP Kingai na ASP Jumanne uliwakuta Sehemu gani pale Kituo cha Polisi
Shahidi: Niliwakuta Nje ya Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Ambapo Afande Kingai alinitaka nipokee Simu Mbili Kutoka Kwa Goodluck ambapo zilikatwa Kutoka Moshi Kwa Watuhumiwa. Nilipokea Simu Mbili, Moja aina ya Itel Nyeusi na Nyingine ni Tecno Nyeusi pia
Wakili wa Serikali: Baada ya akuzipokea ikafuata nini baada ya Kukabidhiwa
Shahidi: Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi alinitaka pia Nikabidhiwe Maelezo Ya Mashahidi yaliyo andikwa huko Moshi pamoja na Hati za Kuchukulia Mali
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umemkabidhiwa Vitu hivyo Ulifanya nini
Shahidi: Nilichukua na Kwenda kuvihifadhi katika Kabati langu la Chuma lilipo katika Ofisi ambayo nilikuwa natumia katika Makao Makuu Madogo Ya Upelelezi Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Kwa Siku hiyo Kitu gani kiliendelea
Shahidi: Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi alinitaka nishirikiane na Inspector Mahita na DC Goodluck Kuhusu Watuhumiwa Wengine Kwa Lengo La kuwakamata
Wakili wa Serikali: Hebu fafanua katika Eneo la Ufutailiaji
Shahidi: Siku hiyo alituelekeza tumfuatilie Mtuhumiwa Khalfani Bwire Katika Maeneo ambayo Taarifa Zimeelekeza
Wakili wa Serikali: Maelekezo hayo walikuwa Wamepewa akina nani
Shahidi: Inspector Mahita, na Mimi Mwenyewe
Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kukwambia Kuwa kuna Watuhumiwa ambao walikuwa wamekamatwa, Hebu elezea ni Watuhumiwa gani walikuwa Wamekamatwa
Shahidi: Ni Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdilah Ling'wenya ambapo Watuhumiwa hao nilikuwa nimekabidhiwa simu zao
Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Ulifahamu Kuwa Watuhumiwa hawa walikamatwa
Shahidi: Ni baada ya Kukabidhiwa Simu. Adam Mbali na Kuwa na Simu aina ya Itel, Kwenye hati ya Kukamatia Mali pia ilionyesha amekamatwa na Bastola aina ya Luger yenye namba 5340
Wakili wa Serikali: Rudia tena namba
Shahidi: 5340
Wakili wa Serikali: Kwa Ling'wenya Alikamatwa na nini
Shahidi: Simu aina ya Tecno ambayo ilikuwa na Rangi Nyeusi
Wakili wa Serikali: Umezungumzia Kuhusu Kuchukua Simu Mbili na Hati za Kukamatia Mali, Elezea Watuhumiwa hao wakati Unamkabidhi wa Walikuwa Wapi
Shahidi: Wakati huo Asubuhi Sikuweza Kuwaona, ila walikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Hebu Elezea sasa Maelekezo ya Kufuatilia Taarifa za Khalfani Bwire mliyatekelezaje
Shahidi: Tulifutilia Maeneo Mbalimbali Kulingana na Taarifa zilizokwepo, Ilipo +fika Majira ya Saa 5 Asubuhi, nilipigiwa Simu na Afande Jumanne Malangahe wakati huo akiwa Mrakibu wa Polisi walitaka nirudi iliniweze Kukabidhiwa Maelezo Ya Watuhumiwa ambao Walikuwa wamemaliza Kuwahoji yeye na Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi
Wakili wa Serikali: Elezea Sasa Mkiwa Na Mahita na Goodluck ni Maeneo gani Mlifuatilia hizo Taarifa
Shahidi: Tulifutilia Maeneo ya Sinza, Oysterbay na Coco beach na Baadae Temeke
Wakili wa Serikali: Wakati Unapigiwa Simu na ASP Jumanne ulikuwa wapi
Shahidi: Wakati huo nilikuwa Maeneo ya Sinza
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Simu Ulifanya nini
Shahidi: Mimi na Wenzangu Tulirudi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam ambapo ASP Jumanne aliweza Kunikabidhi Maelezo ya Mohammed Ling'wenya wakati huo ACP kingai aliweza Kunikabidhi Maelezo Ya Adam Kasekwa
Wakili wa Serikali: Sasa Maelezo haya Ulikabidhiwa Ukiwa wapi
Shahidi: Nilikabidhiwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa umepokea Maelezo hayo ya Watuhumiwa Wawili Wewe Ulifanya nini
Shahidi: Niliyachukua na Kuyapeleka katika Ofisi niliyokuwa natumia katika Makao Makuu Ndogo ya Upelelezi Dar es Salaam na Kuhifadhi katika Jalada Kisha katika Kabati la chuma
Wakili wa Serikali: Ulisema Wakati huo ulikuwa Ofisi ya DCI Makao Makuu Ndogo Dar es Salaam, na Umekuwa Ulielezea hapa Kufuata Maelezo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na Vielelezo Vingine, Kwanini ilikuwa hivyo
Shahidi: Kwa sababu pale Ndipo Jalada lilipo kuwa limefumguliwa na Watuhumiwa walipokuwa wamefilishwa kwahiyo Shughuli Nyingi zilikuwa zinafanyikia pale
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa umechukua Maelezo ya ASP Jumanne na ACP kingai nini Kiliendelea
Shahidi: Mimi na Wenzangu Inspector Mahita, DC Goodluck Tuliendelea na Zoezi la Kumtafuta Khalfani Bwire Kwa Kurudi Eneo la Sinza
Wakili wa Serikali: Maeneo gani ambayo Mlienda.
Shahidi: Temeke tulifika Saa 12 Jioni
Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini sasa kiliendelea
Shahidi: Tulihairisha Kuendelea na Zoezi hilo mpaka Siku inayofuatia
Wakili wa Serikali: Siku inayofuatia ni Siku gani
Shahidi: Ni Siku ya Tarehe 08 August 2020 Majira ya Saa nne Asubuhi, Nikiwa Katika Ofisi Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai, nilipigiwa Su na Afande Jumanne Malangahe Mrakibu Msaidizi Wa Polisi, Alinitaka nifike Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam kwa ajili ya kazi
Wakili wa Serikali: Elezea Kama Ulifanya Maelekezo aliyokupa
Shahidi: Nilifika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Muda Mfupi Nikakuta yupo a Inspector Mahita na DC Goodluck akanijuliisha kuwa amepewa Maelekezo na Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi ya kuhamisha Watuhumiwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na kuwapeleka Kituo cha Polisi Mbweni
Wakili wa Serikali: Baada sasa ya hapo Nini sasa kiliendelea
Shahidi: Tukiwa chukua Watuhumiwa hao kutoka Mahabusu ya Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na Kuwasafirisha kwa kutumia Gari na Kwenda nao Kituo cha Polisi Mbwe
Wakili wa Serikali: Na Ulisema Maelezo hayo ya kuhamisha Watuhumiwa yalikuwa yanahusu Watuhumiwa gani
Shahidi: Ni Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Ling'wenya
Wakili wa Serikali: Mlitumia Gari gani
Shahidi: Gari ya Polisi ambayo alikuja nayo Ramadhan Kingai Kutoka Mkoa wa Arusha, Gari aina ya Fortuner
Wakili wa Serikali: Kituo cha Polisi Mbweni Kipo wapi
Shahidi: Kanda Maalum Ya Dar es Salaam, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni na Wilaya ya Kipolisi Kawe
Wakili wa Serikali: Akina nani wengine Walishiriki zoezi hilo
Shahidi: zoezi liliongozwa na ASP Jumanne Malangahe, Inspector Mahita na Constable Goodluck
Wakili wa Serikali: Na wewe Ulishiriki Vipi
Shahidi: Na Mimi pia nilishiriki
Wakili wa Serikali: Iliwachukia Muda gani Kufika Kituo cha Polisi Mbweni
Shahidi: ilichukua Muda Usiozidi Saa 1
Shahidi: Leo anaongea taratibu Kuliko Mashahidi wote ambao waliwahi Kufika Katika kesi hii, Kila Muda Jaji na Mawakili wa Serikali Wanamkemea na Kuomba aongeze Sauti
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kiliendelea Kule Kituo cha Polisi Mbweni
Shahidi: ASP Jumanne alimuagiza Inspector Mahita Kuwakabidhi Watuhumiwa katika Chumba Cha Mashtaka
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwakabidhi Watuhumiwa katika Chumba Cha Mashitaka nini kiliendelea
Shahidi: Baada ya Kuwakabidhi Watuhumiwa hao Tuliendeleana zoezi la Kutafuta Watuhumiwa Wengine, liliongozwa na ASP Jumanne ambapo alikuwa anaendelea Kupokea Taarifa, akiwepo Mtuhumiwa Khalfani Bwire
Wakili wa Serikali: zoezi kiliendelea kwa namna gani
Shahidi: Tuliendelea Kuwatafuta Watuhumiwa hao Mpaka Saa 1 Usiku
Wakili wa Serikali: Saa 1 Usiku nini Kilitokea
Shahidi: Samahani Mheshimiwa Jaji nilikuwa naomba Kwenda Short call Kuna Dawa nazo tumia Kwahiyo naomba Mahakama inivumilie nitakuwa naenda Mara kwa Mara
Shahidi anatoka kwa kusindikizwa na Askari Magereza Mmoja
Shahidi amerejea
Wakili wa Serikali: Shahidi Ulisema Kwamba Zoezi la Kufuatilia Taarifa liliendelea Mpaka Saa 1 Jioni, Nini kiliendelea
Shahidi: Ilipofika Jioni Saa 1, ASP Jumanne alituambia tusitishe zoezi Mpaka Siku inayofuatia
Wakili wa Serikali: Ili inayofuata ni Siku gani
Shahidi: Tarehe 09 August 2020
Wakili wa Serikali: Tarehe 09 August 2020 Nini kiliendelea
Shahidi: Ilipofika Tarehe 09 August 2020 Jioni nikiwa Katika Majukumu Mengine, nilipigiwa Simu na Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi akinijulisha Kuwa amefanikiwa Kumkamata Khalfani Bwire akiwa na Simu Mbili na aKanitaka nisiondoke katika
Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam ili anikabidhi Simu za Khalfani Bwire..
Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea
Shahidi: Majira ya Saa 3 na Nusu Nikiwa kwenye Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Afande Ramadhan Kingai alifika akiwa pamoja na Afande ASP Jumanne Malangahe, Inspector Mahita na Constable Goodluck Baada ya Kufika alimuagiza Constable Goodluck anikabidhi simu Mbili zilizo kamatwa Kwa Khalfani Bwire. Simu hizo nilizo kabidhiwa Simu Moja aina ya Bundy yenye Rangi Nyeusi, Simu Nyingine aina ya Techno ambayo ni Smart phone yenye Rangi ya blue, Na ilikuwa na Cover Jeusi
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukabidhiwa Simu hizo Ulifanya nini
Shahidi: Nilienda Kuhifadhi Simu hizo Ofisini Kwangu Ndani ya Kabati
Wakili wa Serikali: Sasa ni Shughuli gani Nyingine ili endelea
Shahidi: Wakati na kabidhiwa Simu hizo, Afande Kingai alinitaka pia niziandikie Barua Kwenda Ofisi Ya Uchunguzi ya Makosa ya Mtandao
Wakili wa Serikali: Baada ya Maelekezo hayo sasa nini hasa Kiliendelea
Shahidi: Siku inayofuatia Tarehe 10 August 2020, Afande Ramadhan Kingai alinijulisha kuwa tayari amewasiliana na Shahidi Luten Denis Urio, Wa JWTZ ili afike Siku inayofuatia kwa ajili ya Kuandika Maelezo Yake
Wakili wa Serikali: Baada ya ACP Kingai Kukupa Taarifa hiyo Kuhusu Tarehe 10 August 2020, Nini Kiliendelea
Shahidi: Niliweza Kuwasiliana na Luten Denis Urio Kwa Njia ya Simu, ili aweze Kufika Kwa ajili ya kuandika Maelezo yake
Wakili wa Serikali: alifika Muda gani Katika hiyo Tarehe 11 August 2020
Shahidi: Alifika Majira ya Asubuhi
Wakili wa Serikali: Baada ya Luteni Denis Urio nini Kiliendelea
Shahidi: Niliweza Kuandika Maelezo Yake na Aliweza Kueleza Jinsi alivyo Pata Taarifa
Wakili wa Serikali: Ongeza sauti
Shahidi: Niliweza Kushuka naye na Kwenda Katika Ofisi ni iliyokuwa natumia, na Niliweza Kuchukua Maelezo yake
Wakili wa Serikali: Ulichukua Muda gani Kuandika Maelezo yake
Shahidi: Ilikuwa Asubuhi, Ulichukua Saa Nzima
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kiliendelea
Shahidi: Wakati naandika Maelezo Yake alieleza Kuwa alikuwa akifanya Mawasiliano na Freeman Mbowe kwa kutumia Mtandao Wa Telegram, na alisema Kwamba Alikuwa ana wasiliana na Freeman a Mbowe Kwa namba yake ya 0719 933386
Namba ya Freeman Mbowe, pia alinitajia namba zake aliyokuwa anatumia 0787555200 Ya Mtoa Taarifa Denis Urio, na pia 0754612518 namba ya Denis Leo Urio, Pia alinitajia namba Nyingine Ya Mtuhumiwa Freeman Mbowe 0784779944
Wakili wa Serikali: Wewe Ulichukua Hatua gani sasa
Shahidi: nilimtaka anikabidhi Simu ambazo amekuwa alifanya naye Mawasiliano, Ambapo aliridhia Kunipa Simu aina Ya Techno
Wakili wa Serikali: Kwanini Wewe Uliaka akukabidhi Simu
Shahidi: Ilikuwa ni Kwa ajili ya kwenda Kufanya Uchunguzi Wa Kisayansi, ambapo Urio alisema ni Kwa Telegram
Wakili wa Serikali: Wewe ulipo taka yeye akukabidhi Simu hiyo, alikwambia nini
Shahidi: aliridhia lakini akaomba atoe line ambayo alikuwa alifanyia Mawasiliano na Freeman Mbowe ambapo angeiwasilisha Siku inayofuatia
Wakili wa Serikali: Baada ya yeye Kusema ameridhia na akaomba atoe Card ya Vodacom, wewe Ulijibu nini
Shahidi: Milimkubalia, Huku nikijua Mawasiliano ambayo yanafanyika Kwenye Telegram Yanabakia Kwenye Kifaa na siyo Sim Card
Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea baada ya Kumkubalia Kutoa ile su Card
Shahidi: Niliandika Hati ya Makabidhiano, Huku nikiandika IMEI namba, Kwa ajili ya Kupokea hiyo Simu
Wakili wa Serikali: Hati hiyo ya Makabidhiano Ilikuwa na nini
Shahidi: Hati ilikuwa inaonyesha Simu nimepokea kwa nani, Jina. Lake, Mtu anaye Mkabidhi Pamoja na Kuandika IMEI namba zake kwa kuanzia namba 35 na Kuishia 040 na IMEI Nyingine inaanza namba 35 na Kuishia namba 057
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa Umerekodi Vitu hivyo, gani Kitu gani Kingine Ulifanya katika hiyo Hati
Shahidi: Hiyo Hati Nilisaini na Niliye Mkabidhi naye alisaini Wakili wa Serikali: Baada ya Kusema alikukabidhi Simu aina Techno, Je zile simu Nyingine alikwambia zipo wapi
Shahidi: alisema zipo Nyumbani Morogoro na. Akahaidi kuleta Siku inayo fuatia
Wakili wa Serikali: Siku inayofuatia ilikuwa lini Shahidi: Ilikuwa Tarehe 12 August 2020 katika Ofisi Ndogo ya Upelelezi Dar es Salaam, allifika Majira ya Asubuhi
Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea
Shahidi: aliweza Kunikabidhi Simu Tatu Samsung Duos yenye Rangi Nyeupe, simu Nyingine ni simu aina ya Techno C9 yenye Rangi Nyeusi, Simu Nyingine aina ya Itel yenye Rangi Nyekundu
Wakili wa Serikali: Haya Makabidhiano wewe Ulifanya nini
Shahidi: Niliandaa Hati ya Makabidhiano Ya kila Simu, nikamsainisha na Mimi nikasaini
Wakili wa Serikali: Hebu Elezea Mahakama ni simu ngapi ulipokea Kutoka Kwa Luten Denis Urio
Shahidi: Simu ambazo Nilipokea zilikuwa ni Jumla ya Simu Nne
Wakili wa Serikali: Mara baada ya kuzipokea Ulifanyia nini
Shahidi: Niliweka Exhibit Label PF 143 Kwenye kila Simu
Wakili wa Serikali: Kwanini uliziwekea Exhibit Label Kwa Kila simu
Shahidi: Kwa Lengo la Kuzitofautisha, Ili zisiweze Kuchanganyika
Wakili wa Serikali: Na Hiyo PF 143 ilikuwa na nini
Shahidi: Kituo cha Kesi ilipofunguliwa, Namba ya Jalada, Tarehe ya Kuweka hiyo Lebel, Jina la Mmiliki (Kielelezo) kosa, aina ya Kielelezo na Utambulisho Wake
Wakili wa Serikali: Baada ya KuViwekwa Exhibit Lebel PF 145 Ulifanya nini
Shahidi: Nilichukua na Kwenda Kuvihifadhi katika Ofisi ninayo tumia na Kuhifadhi ndani ya Kabati la Chuma, ambalo Mimi nalitumia
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Bado tunaendelea na Cross Examination, Kwa Ruhusa Yako tunaomba Break fupi ili tukirejea tuweze Kuendelea
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Hatuna Pingamizi
Jaji: Basi tuta break Mpaka Saa 7 na Dakika 45, tutarudi kuja Kuendelea
Jaji anatoka (1:10 PM)