Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa - 28/09/2021

Kama Mosses Linjenje ni marehemu - ifahamike kwa wote kuwa - "Unyama huu haukubaliki."
Ndiyo hivyo tena, kwani akina Ben Saanane na wengine "unyama" ulikubalika?

Ni hivi: Panapokuwepo na kiongozi wa nchi legelege kama Tanzania, kuwa ni "Shetani", mfumo mzima wa uongozi huo unaruhusu vishetani vyote vilivyomo ndani ya nchi hiyo kujitokeza waziwazi ili kutumika katika mfumo huo wa kishetani.

Hawa waTanzania wenzetu ambao 'ushetani' wao haukuwahi kuonekana siku za nyuma wakati ambapo hatukuwa na kiongozi mkuu akiwa shetani, wakati huu walikuwa wamepata ruhusa ya kuuonyesha ushetani wao.
 
Pole mkuu. Mshazoea waoga waoga wanaowaunga mkono kuogopa kuitwa majina ya hovyo
Wewe na huyo Numbisa wako, naona kama akili zenu wote zinafanana vile. Tuufunge huu mjadala tafadhali.
 
Kawaida wanatakiwa wawe magaidi wangapi?
 
Nimeanza kuona mbele kuna kitu kitakuja kutokea haiwezekani mpuuzi mmoja kama kingai na genge lake wajifanye wanajua ,tutanyooshana tu hata kama watakuwa wakongwe hata watoto wao watalipa maana tumeona Mahita naye amerithisha kizazi kama chake
 
Hivi hii kesi ikiisha na watuhumiwa wakaachiwa kwamba hawakuwa na kosa je hao polisi waliowatesa wanaweza kuchukuliwa hatua ?

Hapa ndo kuna changamoto, ni wazi Mbowe hana kosa ila serikali inaogopa kuumbuka hivyo wataonewa tu, ili serikali isipate fedheha, Mungu tenda miujiza haki isimame.
 

Tunakoelekea ata ya kina Ben saanane yatajulikana, Jeshi la polisi ni dhaifu sana,
 
Dah nimesoma hadi nakaribia kutoka machozi.
Yaani askar polisi anamtesa komandoo kwa sababu za kisiasa!!!

Ila hii mbegu aliyoipanda mwendazake isiporekebishwa kuna siku tutashuhudia mauaji kati ya hawa walinzi wetu.

Kwa mfano wajeda wakiambiana tusikubali udhaliliashaji na unyanyasaji waliofanyiwa wenzetu nyie polisi mutalala majumbani mwenu?

Kumbukeni hakuna maelewano mazuri kati yenu polisi na wanajeshi halafu mnaongeza majanga dah!

"Once a soldier is a soldier"
 
Huyo polisi anaepiga kelele HIGH COURT ,bora wamkamate au inakuwaje apige makelele badala ya kusema kwa sauti kuu.
 
What goes around comes around.Hao polisi hawawezi kufanya watachofanya hao wajeshi? Acha kuvichonganisha vyombo vyetu vya dola.
 
Kwasababu itakuwa haramu, siyo? [emoji3]
 
Point of correction, "once a soldier always a soldier".
 
Hii kesi inatabirika kabisa, on face of records inaonekana mashahidi wamepikwa (coaching of witnesses) ambayo ethically haitakiwi.

Pili, kwenye kesi za jinai inatakiwa mlakamikaji athibitishe shtaka lake bila kuacha shaka yoyote (beyond reasonable doubts) lakini hadi sasa hivi matokeo 3-0 huku Mawakili wa Utetezi wakiongoza kwa goli 3 dhidi ya Mawakili wa Serikali. Kuthibitisha bila kuacha shaka si jambo dogo, vijana wa DPP wanaacha mashaka sana, na ikumbukwe this is grave offence (yaani Ugaidi).

Nashauri Jamhuri wasajili "Nolle" yaani kutotaka kuendelea na kesi au Jaji ajiongeze baada ya kuwasiliana na vijana wa DPP kwamba akishafunga ushahidi wa Jamhuri aseme washtakiwa hawana kesi ya kujibu (yaani no premafacie case has been established).

Otherwise, vijana wa DPP watazidi kujidhalilisha na kuidhalilisha ofisi ya mashtaka nchini na taaluma nzima ya Sheria.

Kama sikosei ni Jaji Siyani ambaye ni Jaji incharge wa kanda ya Dodoma anayeongoza kesi hii, na kwa ninavyomjua alivyotulia na anavyojua kujiratibu, wakina Mbowe wataachiwa huru, ni swala la muda tu.

Amicus Curiae.
 
This post has been stared
 
What goes around comes around.Hao polisi hawawezi kufanya watachofanya hao wajeshi? Acha kuvichonganisha vyombo vyetu vya dola.
Hapa hachonganishwi mtu lakini kuna shida kati ya hivi vyombo vyetu vya ulinzi.

Halafu kwa nn mateso kiasi hicho wakati mahakama ilikuwa haijawatia hatiani.Au hawa polisi wako juu ya sheria😣
 
Mbowe alitakiwa ajifunze kupitia hili,, angestaafu siasa
 
Hii kesi ingekuwa inaruka "live"hewani kama Kenya.

Tungekuwa tuna archive nzuri sana na kuona jinsi mahakama na polisi zinavyopwaya .

Ingetumika kama reference nzuri sana mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…