Yaliyojiri Kesi ya Mbowe: RPC Kingai aeleza Mbowe alivyopanga kumdhuru Ole Sabaya. Kesi yaahirishwa hadi 27 Oktoba 2021

Naomba kuuliza swali la kijinga....

Kati ya watuhumiwa watatu na mh mbowe kwani nini wale watatu wanafungwa pingu wakiwa wanaingia na kutoka mahakamani lakin mh mbowe hafungwi?
 
Jifunze kwanza kuandika...hopeless person kabisa hovyo tu CCM ndio maana kichwani ni zero Sasa huyu anaeza hata kufrem kesi ya kubumba jinga sana
 
Weka ushahidi wa kufanya sio kutaka hata Mimi Mimi hapa nataka siro afe je nimemuua? Utanifunga vipi? Nyie Sheria mnajua
 
Hatumuoni malaika ila Mbowe ana uzoefu wa kuongoza chama kwa miaka zaidi ya 15 sidhani kma angepanga ugaidi angefanya wazi wazi hivo eti atume hela kwa namba yake ya M pesa?? Kwani hajui mitandao ingemuanika baadae??

So obviously angemtuma Mrema ama Munisi etc ndio wafanye negotiation sio yeye uso kwa uso maana in case unadakwa basi anakua hahusiki moja kwa moja, rejea kesi ya Lwakatare.

Then baada ya uchaguzi nakumbukwa alikamatwa akiwa yeye na boniface jacob kwa kesi hii hii ya kulipua vituo vya mafuta, ila ghafla wakaachiwa ila walipoita kongamano la katiba ndio kesi inafufuliwa!! Hakuna mtu mwenye akili timamu atakubali hili.

Mbowe anaweza kuwa kitu kingine ila sio gaidi. Hta Makonda alimuita ni muuza madawa ila kesi iliishia wapi? Tuache kuamini haraja maneno ya kisiasa si ndio hawa walidai JPM yupo ofisini anapekua mafaili kipindi ambacho Lissu anadai JPM ameugua?
 
 
Ndege mjaja hukamtwa na tundu bovu
 
Mbona mnahaha sana? Huyu ndiyo kwanza shahidi wa 1 upande wa serikali, kuna wengine 19 wanakuja, subirini!!
Wanakuja kutoa ushahidi au kuuza sura ili wapewe vyeo? Kingai kajikingai Tena Leo, au hujausoma muhtasari wa ushahidi wake? Hana facts Bali hisia zake ndizo anazoziwakilisha mahakamani! Hatumii vifungu vya Sheria kuthibitisha kosa Bali anatumia uzoevu wa kudhania! Leo kabanwa vibaya na Kibatala Hadi akapanic! Huyu anakwenda kukipoteza cheo chake mapema TU, yangu maskio!
 
Alikuwa shahidi wa nini hasa?
 

CCM wenzako wote Leo wako kimya maana kila mwenye hofu ya Mungu anaona uovu katika kesi hii.

Narudia tena muulize jingalao kilichompata alikuwa zaidi yako.
wanza erythrocyte
 
CCM wenzako wote Leo wako kimya maana kila mwenye hofu ya Mungu anaona uovu katika kesi hii.

Narudia tena muulize jingalao kilichompata alikuwa zaidi yako.
We vipi tena? Gaidi linaelekea kutiwa kwenye mnyororo wa chuma
 
Wenyewe wanaoifahamu vyema kesi hii wanakwambia hivi:

1. "Mbowe siyo Malaika", wakionyesha wanajuwa mengi yaliyopangwa na Mbowe na wenzake, yatakayowashangaza watu yatakapotolewa mahakamani.

2. Mwingine katangazia dunia kabisa, kwamba "washiriki wenzake tayari yalishahukumiwa na wanatumikia vifungo vyao. Mbowe pekee yake hakuhukumiwa kwa vile alikimbia na kwenda kujificha Nairobi." Kwa hiyo ni zamu yake Mbowe kupata haki yake mahakamani!

Na ushahidi wenyewe utakaomweka hatiani, ndio huo ambao umewasilishwa mahakamani na shahidi wa kwanza wa Jamhuri.

Hawa watu wote hawaoni hata haya, soni, aibu mbele za watu wengine wenye akili timamu, wenye uwezo wa kufikiri. Hivi kweli inahitaji mtu ajue sheria kama msomi wa fani hiyo kuweza kuona yanayoendelea kwenye mahakama hii?

Tukiweka pembeni uovu wa matakwa yao, tunaloweza kusema hapa ni jinsi nchi yetu ilivyoporomoka, hata katika ule uwezo wa kutunga uongo tu unaoweza angalau kuonekana kama una ukweli ndani yake.
Lakini hawa wakubwa hili siyo tatizo kwao, maadam wanao uwezo wa maguvu, kufanya lolote wanalojisikia wanaweza kulifanya.

Ikiwapendeza, Mbowe anaweza kuendelea kukaa ndani kwa muda wote wakati hawa wakiendelea kuwa madarakani kwa nguvu.

Wakati huo huo, tusiwasahau wahusika kama DCI, ambaye anaruhusu kesi kama hii kwenda mahakamani!

Nchi hii tumefika pabaya sana sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…