Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Lile kongamano la jana lilikuwa tamu sana, Nkrumah ilitema mpaka nje. Watu tumesimama toka saa 4 hadi hadi saa 8 bila kuchoka maana sehemu kubwa ya waliozungumza walikufanya ujue what next.

Ukiangalia wachangiaji wengi hapa na wa jana tunakubaliana jambo moja kwamba KATIBA IANDIKWE UPYA.
Tatizo lililopo ni namna gani itaandikwa na tusipoangalia tutabishana kwenye hili ghafla 2015 hiyooo.
Kuna mchangiaji mmoja jana aliuliza "Wananchi tufanye nini ili kuipata hii katiba mpya???"

Pengine pamoja na mashaka yetu juu ya tume ya rais pengine tuipe a benefit of doubt kwamba inaweza kuja na mawazo ya mchakato gani utumike kuifikia hiyo katiba maana rais ameahidi tume itaongozwa na mtaalam wa sheria aliyebobea ( of coz sio Werema).Otherwise mijadala kama ya jana inafaa iendelee, natamani wale wasomi wa makanisa na miskiti waliotengeneza manifesto zao mwaka 2010 kabla ya uchaguzi waje na mjadala pia. Wasiongelee dini zao bali msitakbali wa nchi kwa jicho la dini. TUCTA nao wafanye hivyo upade wa wafanyakazi wakati NGOs ziangalie namna ya kuwaunganisha wakulima na wafugaji ili wajue katiba ndio pembejeo, maji, malisho ya mifugo yao n.k
 
(1)Tutumie msamiati sahihi: Hatutaki kuandika katiba upya; tunataka kuandika katiba mpya. Kuandika katiba yetu upya maana yake ni kuisahihisha iliyopo hapa na pale. Tunataka kubadilisha hata utangulizi wake, na kuweka vipengele vingine.

(2) Kutakuwepo na conflict of interest kama Rais atachagua tume ya kuratibu uandishi wa katiba. Tume iundwe na Bunge ili iajibike kwa wawakilishi wa wananchi. Mpango wa Mnyika wa kutaka Bunge lipitishe sheria ya kurasimu uandishi wa katiba mpya ni sahihi.

(3) We need not re-invent the wheel. Mchakato uliotumika kwa ufanisi na wenzetu wa nchi jirani una masomo ambayo yanatufaa.

(4) Tutakuwa tumeanza vibaya sana kama tutakubali ushauri wa Shivji wa kuandika katiba kwa kutumia mfumo wa kamati ya Rais. Shivji amechemsha, big time.
 
Tundu Lissu.....kashangiliwa kweli!!!!
Watoa mada wamezungumza masaa mawili na nusu, anaomba muda wa uchangiaji uongezwe!!!
anatofautiana na Shivji, tunahitaji katiba mpya ili kubadili utaratibu uliotufikisha hapa ambao umetufikisha pabaya.
Nchi hii haiwezi kutawalika tena kwa katiba hii.......rais mfalme, chama kimoja, muungano wa serikali mbili.
Point noted
Prof Shivji ktk mdahalo wa leo ulioandaliwa na UDASA ameuma maneno kuhusu uhalali wa JK kuwa madarakani KIKATIBA kwa kuwa katiba yenyewe haikutokana na matakwa ya wananchi lakini amemshambulia Rais wa kwanza Nyerere kwamba eti hakuwa kihalali KIKATIBA! Lilipokuja suala la uhalali wa JK na marais waliofuata baada ya Nyerere akajifanya amesahau kulijibu na alipokumbushwa akadai unahitajika ufanyike utafiti kwanza! Kwa hili simwelewi Shivji!
Aha-ha-hah!
Shivji ameaibika. Siku zote nimekuwa nikimuona wa maana, kumbe kenge tu!
 
Hivi wadau mna habari TBC walipotosha umma juu ya hili kongamano? Waliwanukuu Shivji, Ulimwengu na Lissu wakikataa katiba mpya ila marekebisho. TBC1 NI JANGA LA TAIFA. Mlioangalia news zao jana mtakubaliana na mimi.
 
tunapenda kuwataarifu wananchi ambao hawataweza kufika ckd kuwa kongamano la katiba kesho litaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha itv. Tunawashukuru sana itv kwa moyo wa uzalendo.

Karibuni

kitila

mkuu tumeuona mchango wa udasa hapo ndio tunajua kweli tuna wasomi nchi hii-vipi tunaweza kupata dvd za mjadala???
 
Tafadhari kama kuna mtu an video za mdahalo wa katiba Nkuruma inisaidie sikuona kabisa.
 
Back
Top Bottom