LGE2024 Yaliyojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha - Novemba 27, 2024

LGE2024 Yaliyojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha - Novemba 27, 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Arusha.jpg

HISTORIA
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara, wenye ukubwa wa KM za mraba 34,515.5. Idadi ya watu kwa ongezeko la 2.7% kwa mwaka na inakadiriwa kufikia jumla ya watu wapatao 1,835,787 ambapo wanawake wakiwa sawa na 51.5% na wanaume 48.5%

Mkoa wa Arusha umepakana na Mkoa wa Manyara kwa upande wa Kusini, upande wa Mashariki umepakana na Mkoa wa Kilimanjaro, kwa upande wa Kaskazini umepakana na Nchi ya Kenya na kwa upande wa Magharibi umepakana na Mkoa wa Simiyu na Mara.
MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA ARUSHA
Katika Mkoa wa Arusha, kuna mgawanyo wa kiutawala ambao unahusisha mamlaka za miji na wilaya. Mamlaka hizi zimegawanywa kulingana na idadi ya kata, mitaa, vijiji, na vitongoji vinavyopatikana ndani ya maeneo yao.

Arusha Jedwali.PNG

Chanzo: TAMISEMI

Mamlaka za Miji
Jiji la Arusha linajumuisha jumla ya kata 25 na mitaa 154. Hata hivyo, hakuna vijiji wala vitongoji ndani ya Jiji la Arusha, kwani linaendeshwa zaidi kwa mfumo wa mijini. Hii inaonyesha kuwa jiji hili ni kitovu cha mijini katika mkoa huu, bila kuwa na maeneo ya vijijini.

Mamlaka za Wilaya
Kwa upande wa wilaya za Mkoa wa Arusha, kuna mgawanyo wa utawala ambao unahusisha wilaya sita;

1. Wilaya ya Arusha ina kata 27, vijiji 67, na vitongoji 259.
2. Wilaya ya Karatu ina kata 14, vijiji 57, na vitongoji 262.
3. Wilaya ya Longido ina kata 18, vijiji 51, na vitongoji 176.
4. Wilaya ya Meru ina kata 26, vijiji 90, na vitongoji 330.
5. Wilaya ya Monduli ikiwa na kata 20, vijiji 62, na vitongoji 236.
6. Wilaya ya Ngorongoro ina kata 28, vijiji 65, na vitongoji 242.

Kwa ujumla, Mkoa wa Arusha una mamlaka za wilaya tano zenye jumla ya kata 133, vijiji 392, na vitongoji 1,505.

MAJIMBO YA KIUCHAGUZI
Katika muktadha wa kisiasa, Mkoa wa Arusha umegawanyika katika majimbo saba (7) ya uchaguzi, ambayo yana jukumu muhimu katika kuwakilisha maslahi ya wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majimbo haya ni yafuatavyo: Arusha Mjini, Longido, Karatu, Ngorongoro, Arumeru Mashariki, Arumeru Magharibi, Monduli.

SOMA PIA: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

HALI YA KISIASA
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya mikoa muhimu ktoka kanda ya Kaskazini ambapo umekuwa ukitajwa kuwa ni kambi ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA ambapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 CHADEMA waliambulia majimbo sita 6 kati ya saba 7.

Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 pamoja na uchaguzi mkuu 2020 ni moja ya sababu zinazoonesha kutaka kuzorotesha nguvu ya vyama vya upinzani katika mkoa wa Arusha kama ilivyokuwa katika mikoa mingine kwani mchakato wa uchaguzi huo uliwaondoa wagombea kwa kigezo cha kukosa sifa, na kupelekea baadhi ya vyama vya siasa kujitoa katika uchaguzi huo kwa kutokuwa huru na haki huku wagombea kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM kupita bila kupingwa.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 uliwaondosha wabunge wote kutoka CHADEMA bungeni, kwani uchaguzi huo uliwapa ushindi mkubwa wabunge wa chama tawala CCM katika mkoa huo.

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mara kadhaa kimekuwa kikifanya mikutano ya hadhara katika mkoa wa Arusha ili kujiandaa kuelekea katika chaguzi hizo huku ukitegemewa kuwa uchaguzi wenye ushindani tofauti na ule wa 2019 na 2020.

YANAYOJIRI KUELEKEA NOVEMBA 27
MATOKEO YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
- LGE2024 - News Alert: - CCM yashinda 98.83% Wenyeviti Serikali za Mitaa
 
Back
Top Bottom