Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye mahojiano kati ya Chief Odemba na Peter Msigwa kwenye kipindi cha Medani za Siasa

Pre GE2025 Yaliyojiri kwenye mahojiano kati ya Chief Odemba na Peter Msigwa kwenye kipindi cha Medani za Siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Mikutano ya Makatibu Wakuu wanakimbia ila hii ya roporopo anayoenda kuchamba chama chake cha zamani ahhhh, sababu inawachafua wengine na kuwapaisha wao.

Ngoje tuona Msigwa atakuja na jipya gani leo.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa: Nchimbi kaingia mitini, wengine wagoma kushiriki!

IMG_20240907_171316_050.jpg



Baadhi ya Maswali Odemba na Majibu Mchungaji Msigwa yaliyojitokeza kwenye mahojiano

Msigwa kupinga matokeo ya Uenyekiti Kanda ya Nyasa

Odemba:
Tulipoketi hapa wakati wa Mdahalo baina yako na sugu uliahidi Watanzania kuwa utakubaliana na matokeo mara baada ya uchaguzi na utamuunga mkono yule ambaye atashinda na kutangazwa, umekuja kuwashangaza walio wengi kwa kukataa na kupinga yale ambayo uliahidi. Kwanini uliwadanganya Watanzania na kwanini umekuwa kiongozi kigeugeu kwa kiwango hicho?

Msigwa: Ni kweli tulivyokuwa kwenye Mdahalo nilizunguza hayo maneno na baada mara ya uchaguzi nilisimama kukubaliana na yale yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi. Lakini nimeulizwa na watu wengi na nimesema hata mahakamani kunakuwaga na Mawakili wa pande mbili, jaji anapotoa hukumu mawakili wa pande zote mbili wanasimama kwamba wanakubaliana na ile hukumu kwa mujibu wa taratibu lakini wakitoka nje upande ulioshindwa, na Jaji anapomaliza ile kesi anasema upande ulioshindwa unayo haki ya kukata rufaa. Mawakili wakitoka nje husema hukumu hii hatujatendewa haki tunakata rufaa. Kwahiyo nilikubaliana lakini baadaye kulikuwa na ilegularity nyingi sana zilizokiukwa na wizi wa hali ya juu, uvurugaji wa hali ya juu ambazo baadaye nilizikatia rufaa kama moja ya demokrasia na moja ya haki yangu. Kwahiyo sikufanya makosa nilifuata utaratibua.

Sababu za Msigwa kutokubali Mrema kusimamia Uchaguzi Kanda ya Nyasa
Odemba:
Baada ya Uchaguzi ulipeleka lawama zako kwa Mrema. Kwanini ulihisi Mrema ameharibu uchaguzi?

Msigwa: Kwanza kabla ya Uchaguzi siku mbili au tatu nilimandikia barua Katibu Mkuu kwamba Bwana Mrema mliyemtuma kusimamia uchaguzi huu ametake sides nikatoa malalamio yangu lakini Katibu Mkuu hakunijibu barua yangu. Nimetoa malalamiko yangu kwa nguvu sana sikujibiwa wala hatua hazikuchukuliwa (Lalamiko hilo limehifadhiwa hapa). Mrema alionekana kula na kunywa rushwa aliyopewa na Mgombea mwenzangu kinyume na utaratibu

Odemba: Wasimamizi walipewa rushwa na Mgombea mwenzako, ushahidi upi ulio nao? Na rushwa ilikuwa ya nini na kwa kiwango gani?

Msigwa: Suala la Rushwa ni triki lakini kimoja wapo ni kwamba rushwa ya pombe, rushwa ya chakula. Na wewe kama hakimu hauwezi kukaa mpaka usiku na hasimu wangu ambaye tunashtakiana naye huku utegemee kwamba utatenda haki haiwezekani.

Odemba: Hivyo Mrema na Kigaila walipewa rushwa

Msigwa: Mrema akiwa Iringa pale kabla hajaondoka muda wote alikuwa na Mgombea Mwenzangu. Muda wote chakula na pombe na sio siri na baadaye tulipomuulizia alisema na wewe ukitaka ninunulie pombe.

Odemba: Kuna Ubaya wowote?

Msigwa: Ubaya Mkubwa sana kwa sababu wewe unayekwenda kusimamia haki, haki inatakiwa ionekane na itendeke. Chama chetu kimekuwa kinara kwamba Tume ya Uchaguzi hawatendi haki wanapendelea kwahiyo wewe kama Msimamizi wa Uchaguzi kwa Mfano wakati unafanya kusajili watu, kuna watu wanaitwa mazoku. Huyu Dada Catherine Ruge anasimamia nyanda ya Nyasa na nilimlalamikia kwamba ametake side from the begining kuanzia mwezi wa kwanza wa pili alivyokujaga kule, Yeye aliyekuwa anatakiwa atende haki alikuwa analala Desderia kwenye Hotel ya Sugu. Kwa muda wote analala Desderia ndo anakuja kufanya kazi. Nimelalamika kwa barua kwa chama kwamba huyu anayekuja kusimamia haki. Kwamba aliletwa kimkakati wale wanaoniunga mkono kwenye majimbo yote wasipite lakini hayo yalishindikana. Nimelalamika kwa barua, nimelalamika kwenye vikao haikutendeka. Kwahiyo hata huyu Mrema aliambiwa kwamba unachokifanya sio sawa sababu wewe ni hakimu.

Odema: Hiyo pombe ambayo unaisema una uhakika kwa mba alitoa Sugu

Msigwa: Ndiyo, nina uhakika kabisa, hivyo vitu nina uhakika kabisa haya mambo sio nimesema leo, nililalamika mapema kabisa imeandikwa kabisa na sikujibiwa barua na Katibu Mkuu wa Chama. Nilitoa malalamiko ya wazi kwa mfano Peter Baleku aliyepaswa kuwa mshindi alizuiwa kupiga kura, makatibu hawakupiga kura, uchaguzi wa Njombe ulivurugwa kwa makusudi na amri iliyokuwa inatokwa kwa Mwenyekiti wa chama kwamba hakikisheni Msigwa hapiti. Kulikuwa na vikolombwezo vingi sana ambavyo kulikuwa hakuna uchaguzi huru na haki. Hivi ni vitu ambavyo vinatoa uhalali wa sisi kuikosoa tume ya uchaguzi.

Odema: Hiyo kauli ya hakikisheni Msigwa hashindi alikwambia wewe?

Msigwa: Nimeipata kwenye vyanzo tofauti vingi na nimemchallenge kwenye Kamati Kuu kwamba wewe unapita kwenye Kanda yangu unasema lazima mimi nishindwe. Nilimchallenge tukiwa kwenye Ziara Rukwa na nilipomuuliza maswali hayo hata Lema anajua. Nilipokaa nao nilisema hawa watu wanapita alikuwa anapita Boni, anapita Toby kwamba hawa watu wanapita wanasema Msigwa asinshinde, Nilikaa naMwenyekiti nikamuuliza kwamba hawa watu umewatuma alishindwa kunijibu, Nimeenda Kamati Kuu nikamchallenge kuwa nilikuuliza tukiwa Rukwa kwenye Ziara nimekuuliza Kamati Kuu Mwenyekiti alikuwa hana majibu. Kwahiyo sio vitu ambavyo nimetunga kutoka hewani. Kwanza nilimface Mwenyekiti Mwenyewe, nililalamika ndani ya chama, nikakata rufaa kwa sababu watu wengi wanaomzunguka wanategemea teuzi zake kwahiyo hawawezi kumkabili.

Odema: Kwanini uliamua kuondoka CHADEMA ilihali rufaa yako ilikuwa bado inasikilizwa? Ulikata rufaa ya nini ikiwa unajua unaondoka?

Msigwa: Rufaa zote za nyuma zilikuwa zinasikilizwa ndani ya wiki moja, zingine siku tatu zinasikilizwa Ya kwangu imeendelea kuwa inachezewa tu hawataki kuisikiliza kwa sababu kimsingi walikuwa hawana majibu kwahiyo wanasema waliamua kuchutama, walikuwa wanadilidali hawana majibu, walikuwa wanatafuta mahali pa kuchomoka. Lakini kila mwanadamu ana point of elasticity. Mwanadamu anakuwaga na uvumilivu unafikaga mwisho. Kuna mtu aliniuliza uliamua lini kutoka CHADEMA, kutokuridhishwa na mambo ya CHADEMA hakujaanza juzi nilivyotoka CHADEMA kwenda CCM. Kumekuwa Gradual kuna mambo mengi ya maudhi yameendelea kuwepo. Kwa mfano, tulivyokuwa bungeni Mwenyekiti wa Chama alikuwa haoneshi Leadership kabisa yeye kamakiongozi wa kambi ya upinzani alikuwa haoneshi leadership kabisa.

Alikuwa haudhurii vikao vya bunge matokeo yake wakati fulani alikuwa anafanya maamuzi ambayo wakati fulani yalituathiri mfano yale maamuzi ya Corona. Lakini muda mwingi aliochukua leadership pale sababu alikuwa na ombwe la uongozi alichukua Zitto au Mbatia, yeye kama kiongozi alikuwa nanajificha, Hayo mambo ambayo sisi wenye akili bungeni tuliwahi kulalamika kwamba huyu mtu anaitwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani lakini hatuioni leadership. Kwahiyo mambo yameendelea kupile up mpaka inafika mahali kwamba enough is enough.

Odemba: Iwapo ungeshinda kwenye uchaguzi wa Nyanda ya Nyasa ungeen CCM?

Msigwa: Mfumo wa Vyama Vingi ulipoanza na watu walipoanza kudai katiba, walianza kudai katiba baada ya kuwa na experience, katiba na tume huru ya uchaguzi baada ya kupata experience walivyoingia kwenye uchaguzi. Swali hilo ni sawa na kusema kama wapinzani wangeshinda wangedai katiba?

Kama Msigwa angeshinda Uchaguzi Kanda ya Nyasa

Odemba:
Swali la msingi ni je kama ungeshinda ungeenda CCM?

Msigwa: Inategemeana na mazingira ambayo ningekutana nayo kwa sababu kubaki CHADEMA au kutokubaki hakutegemeani na cheo isipokuwa inategemeana na misingi ya chama lakini mambo mengine unaamua kuchukua hatu sababu ya experience unayoipata

Odemba: Umenieleza kuwa haya mambo uliyaona mapea sana, hii ina maana kuwa wakati unaenda kwenye uchaguzi maana yake tayari ulikuwa na wazo la kwenda CCM maana yake kivyovyote vile haiwezekani mawazo ya kwenda CCM yalianza baada tu ya Uchaguzi.

Msigwa: Nimetoa mfano kama kwenye ndoa, ukiona watu wameachana kwenye ndoa hawaachani siku moja huwa kuna mambo yaanza upandana, wanakaa wanagombana wanasuluishana. Mpaka watu wanasema wanataka talaka maana yake kunakuwa kumefika mwisho. Mimi mambo ya CHADEMA yapo mengi na naomba Wananchi mnielewe. Mimi sio mgeni na Freeman Mbowe. Tumesafiri wote kwenye Helikopta, tumesafiri kwenye magari, tumekula wote, tumefanya kazi ya siasa wote, tumekuwa Bungeni wote kwa miaka kumi.

Kwahiyo mimi sio kichaa ninze tu from no where nigeuke. Kuna mambo mengine siwezi kuyasema nayoyajua kwa sababu hamtanielewa, kwahiyo inabidi nikae nayo moyoni. Nachotaka kusema kufeli kwa leadership yake haya mambo hayanisumbui mimi tu, kuna watu wengi yanawasumbua, wengine hawana guts za kutoka na kusema wengine wanagugumia tu kwa sababu za ukabila, wengine wanagugumia sababu ya urafiki hawataki kutoka hadharani kusema vitu havipo sawa. Watu wengine wameifanya chadema kama ni dini kama ni Ukristo utasikia hata wana wa Israel walipotoka Misri walipata mateso thats rubbish hakuna wana wa Israel hapa hiki ni chama cha siasa. Ndani ya Chama chochote kuna watu wabaya na wazuri.

Ndani ya CCM kuna watu wazalendo na wanaoipenda nchi na ndani ya CHADEMA ipo hivyo hivyo. Sasa watu wanaona kwamba ukiwa CHADEMA wao ndiyo Wachamungu na wale wa CCM ndiyo mashetani very wrong.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Peter Msigwa afichua madudu ya CHADEMA: Chama kimekuwa kama SACCOS, Mbowe anakimbiwa na kila mtu
 
Leo ni leo mchungaji Peter Msigwa mwanachama mpya mchanga wa CCM kapatikana, baada ya bosi wake katibu mkuu wa chama dola kongwe CCM ndugu Dr. Emmanuel Nchimbi kukimbia interview.

Chama dola kongwe kutumia mamluki mpya akiseme chama chenye utitiri wa makada waliolelewa toka TANU Youth League hadi UVCCM wakazeekea chamani, hakika CCM imekata pumzi in Kingunge Ngombale Mwiru voice
 
Msigwa hakomi tu kwa Kikeke nusu akimbie leo tena anarudia ? Msigwa inatakiwa afanye mahojiano na kina Kitenge sio hawa wa kina Odemba
 
Odemba anatafuta stress tena. Msigwa ataingia mitini halafu Odemba aanze kulia.
Nadhani ameshafanya kipindi tayari, kinachorushwa usiku ni recorded. Hata hivyo sioni kama atakuwa na jipya zaidi ya nongwa kwa cdm, na chuki yake dhidi ya Mbowe.
 
Good,
CCM tunafanya tactics, na kwa ujinga chadema wanakuwa busy kweli, muda ni mfupi nawaamusha ma chadema kaamsheni matawi vijijini, msipumbazike na kesi zisizo na kichwa wala miguu, nawafumbuwa rudini vijijini muda ni mfupi sana. (Tusije laumiana) CCM Tunawapenda sana chadema.
 
Wote tunakumbuka jinsi mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama Vya Siasa ulivyoshindikana kufanyika

Kumbe inawezekana Washiriki wa Mdahalo baada ya kuridhia wakashiriki kuutangaza Mdahalo Kwa Umma

Nimeona kwa Kamala Harris na Trump kuhusiana na Mdahalo wao wa Jumanne

Ahsanteni Sana 😂😂
 
Hakuna kichwa ndani ya ccm kwa sasa chenye uwezo wa kufanya mdahalo.

Safu yote ya juu ya ccm naona vichwa vyao havina ubongo.

Mangula na Kinana wangekuwepo hao wangeweza.
 
Shida haiko kwa mtagazaji Odemba au kituo kinachoandaa na kurusha midahalo hiyo yaani StarTV....

Shida iko kwa viongozi wanasiasa hawa wanaoalikwa kushiriki hususani wa CCM kuwa waoga kushiriki mijadala huru na ya wazi kama hii ya USA....

CCM ni waoga kwa sababu ya tabia yao ya UONGO, UNAFIKI na KUPATA nafasi hizo za uongozi wa watu kiujanja ujanja na wizi wa kura....

Watu wa tabia na mwenendo huo usitegemee washiriki mijadala huru na ya wazi. Wao hujiandalia midahalo yao yenye maswali wanayopanga wao waulizwe na mtangazaji au mwendesha mdahalo wanayemtaka wao na kituo cha TV au radio wanachokitaka wao....

Odemba na StarTV hawana cha kujifunza toka USA bali CCM ndiyo wajifunze siasa na demokrasia ya nchi kama hiyo na MUACHE WOGA kukabiliana na wananchi.....!!
 
Viongozi wa ccm hawatakagi midahalo
Umuite kuingozi mkuu kwenye mdahalo,utaambiwa hawezi kuja maana yeye ni mtu mzito sana

Ova
 
Wote tunakumbuka jinsi mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama Vya Siasa ulivyoshindikana kufanyika

Kumbe inawezekana Washiriki wa Mdahalo baada ya kuridhia wakashiriki kuutangaza Mdahalo Kwa Umma

Nimeona kwa Kamala Harris na Trump kuhusiana na Mdahalo wao wa Jumanne

Ahsanteni Sana 😂😂
Odemba sio wa kumpa hizi habari

He won’t understand
 
Back
Top Bottom