Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wadau wa Warsha/Kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo
Hii ni warsha ya siku moja ambayo inawakutanisha wadau mbalimbali wa Teknolojia na mawasiliano-TEHAMA katika kujadili masuala mbali kuhusu sekta hii.
Meneja Mikakati na Uendeshaji wa Jamii Media, Bi. Asha Abinallah(Wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Warsha hiyo Carol Ndosi, Maria Sarungi(Moderator) na Catherinerose Barretto
Akiongea katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo amesisitiza kuwa tatizo kubwa katika nchi sio Jeshi la Polisi bali ni Sheria zinazosimamia Mitandao ya Kijamii.
Hivyo watu wasijikite katika kuwalaumu Polisi bali lengo kuu liwe katika kuziangalia Sheria zinazosimamia mitandao hiyo.
Mkurugenzi wa JamiiMedia, ndugu Maxence Melo akichangia wakati wa warsha hiyo
Tunahitaji kubadili namna Watu wa Serikali inafikiri wakati inapitisha Sheria zenye makosa. Raia wanapaswa kulinda.
Mdau wa Tehama akichangia
Bw. Dawson Msongaleli(CyberCrime Depertment Tanzania)
Naye Dr. Wakabi kutoka CIPESA anasema Pale watumiaji wa mtandao wanapokuwa na uoga wa kutambuliwa, inazuia utumiaji mzuri.Julieth Namfuka(CIPESA): Katiba ya Tanzania inatoa uhuru wa kujieleza bila kuingiliwa
Julieth Namfuka(CIPESA): Kuchuja taarifa kupitia miundombinu ya TEHAMA inakuwa sana katika nchi za kiafrika.
Erick Kabendera: Watu wanahisi mazungumzo yao yanasikilizwa; hii inaturudisha nyuma kama nchi
Erick Kabendera: Suala la watu kukamatwa kwa ajili ya kujieleza na kutoa maoni yao linaturusha sana nyuma.
Pascal Mayalla amelezea jinsi ambavyo amekuwa akitumia huduma ya JamiiForums kwa takribani miaka 11 hadi sasa.
Erick Kabendera: Serikali itumie mitandao ya kijamii kama JamiiForums kupata maoni ya wananchi wake.
CarolNdosi: Kumekuwa na changamoto ya kupata taarifa serikalini kwa ajili ya kushughulika matatizo ya jamii
Bi. Carol Ndosi siku ya Warsha ya Jamii Media/CIPESA jijini Dar
Wakili msomi, Jebra Kambole akiongelea changamoto zilizopo kufuatilia Sheria zilizopo na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania.
Wakili James Marenga: Sheria hutengenezwa/tungwa kwa ajili ya watawala, huo ndio ukweli wenyewe! Anasisitiza kanuni ni muhimu
Wakili Jebra: Lengo la kupitisha #CyberCrimeLaw kwa hati ya dharura halijawa wazi. Ni 2% ya watanzania wanaoijua sheria yenyewe!
Chambi Chachage kutoka @Udadisi: Watu wengi wanaandika maudhui mazuri wanapotumia utambulisho usiojulikana mtandaoni
->Kwa maudhui ya mtandaoni inabidi tujikite zaidi na ujumbe kuliko mwandishi wa huo ujumbe.
->Nimekuwa mtumiaji wa mtandao wa Jamiiforums kwa miaka kumi sasa, najua jinsi usiri ulivyo muhimu.
Wakili Jeremiah Mtobesya: Nimesimamia kesi nyingi za Makosa ya Mtandao na EPOCA na nimebaini nyingi zina msukumo wa kisiasa
Wadau wa kongamano wakichukua picha ya pamoja (selfie) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Bw. Maxence
Meneja Mikakati na Uendeshaji wa Jamii Media, Bi. Asha Abinallah(Wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Jamii Media katika Warsha ya Jamii Media/CIPESA
==========
Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania inayoendesha mitandao ya JamiiForums na FikraPevu kwa kushirikiana na CIPESA(The Collaboration on International ICT Policy in East and Southern Africa) iliyo na makao makuu yake nchini Uganda imefanya Kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini hasa wanaohusika moja kwa moja katika kulinda faragha za wateja wao ili kujadili masuala mbalimbali ya Huduma za Habari na Mawasiliano katika jukumu lao kuwa kiunganishi kati ya mteja na huduma watoazo pamoja na namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo.
Kabla ya kufanyika kwa Kongamano hilo siku ya Jumatano tarehe 12 Julai, Jamii Media ilifanya mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 10 hadi 11 Julai kwa vijana mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati na wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Mafunzo hayo yalilenga kujenga uelewa kuhusu sera zinazohusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Usalama wa Data Mtandaoni, Hali ya Uhuru Mitandaoni na Mambo yanayoathiri uhuru Mitandaoni nchini Tanzania.
Katika Kongamano hilo, Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Dawson Msongaleli kutoka kitengo cha Makosa ya Mtandaoni alifanya pia Uwasilishaji kuhusu Sheria ya Makosa Mtandaoni na kueleza kuwa Usiri na Usalama wa taarifa za watumiaji wa mtandao ni vitu viwili vinavyokanganya na kwamba inafika wakati ili kutekeleza kimoja inabidi misingi ya kingine ivunjwe.
Aidha, alibainisha kuwa kukosekana kwa kanuni za usimamizi wa Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) ni changamoto kubwa kwani inapelekea tafsri ya Sheria hiyo kubadilika kulingana na mazingira na mtu anayetafsiri kitu ambacho kinaathiri kazi yao kama watekelezaji wa Sheria na kuahidi kuwa mamlaka zinashughulikia chamgamoto hiyo.
Mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo alisema hili ni Kongamano la kwanza la aina hii kufanyika tangu kuanzishwa kwa JamiiForums miaka 11 iliyopita na limekuwa na matokeo chanya baada ya wadau kujadili kwa kina masuala mbalimbali yahusuyo usalama wa watumiaji. Aliongeza kuwa wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia huduma nzima ya matumizi ya mitandao lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma hizo.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo wamiliki wa blogu na watumiaji wa kawaida wa mitandaonya kijamii ili kuhakikisha wanakuwa na matumizi mazuri ya huduma hiyo ili kupunguza mkanganyiko kwao na kuwapa fursa adhimu ya kunufaika na uwepo wa mitandao hiyo.