Yaliyojiri Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, kesi ya Mbowe na wenzake 3 - Kesi imeahirishwa hadi Nov. 29 2021

Aliyeisumbua mahakama ni Kingai ambaye alifungua kesi ya ugaidi, halafu akaishia kutoa ushahidi wa kuharibika kwa gari njiani na kula nyama choma.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mahakamani itanajisiwa mara ngapi? Mbona ilishakua najisi toka waanze kuteuliwa majaji wasio na vigezo?
 
Ni asilimia 20 tu ya watanzania walipendekeza vyama vingi na hawa ni waelewa. Nyerere akakubaliana nao. Wanaotaka katiba mpya ni waelewa na wanaojua ukweli na ni wachache sana. Wenye uelewa lakini hawataki ni walafi na wanafiki.
Sasa Nyerere hayupo tutawezaje kuwashinda wanafiki wanaoungwa mkono na 80% wasio na uelewa.
Hawa wachache walafi ndio wanawatengenezea mtego wanaotaka katiba mpya.
Ipo siku asubuhi kutakucha kwa walio wengi.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 

1. Hakika kabisa, hii kesi siyo ngumu. Ugumu unakuja kwa sababu Jaji analazimishwa kutoa maamuzi kwa kupinda sheria

2. Ni sawa na kusema, kutiririka kwa maji ya mto naturally ni rahisi tu. Lakini ukitaka kuyalazimisha maji ya mto yatiririke kurudi yaliko toka, utapata shida sana na automatic hutaweza. Ndivyo anavyotaka kufanya Jaji katika kesi hii, kulazimisha maji yatiririke kupandisha mlima, yarudi yalikotoka...!
Mawakili wa Serikali Kwanini Wanakataa Barua Isipokelewe? Wanaficha Nini?
KIINI CHA MAWAKILI WA JAMHURI KUKOMAA KUIZUIA BARUA HIYO ISIPOKELEWE NI:

1. Mshitakiwa Mohamed Abdilah Ling'wenya anasema alipotolewa Moshi kwanza alifikia TAZARA police station na baadae Mbweni Police Station. Hakuwahi kupitishwa Central Police DSM...

2. Wao polisi na Jamhuri wanaoshitaki wanasema SIYO KWELI washitakiwa wote 1 Adamoo na 2 Ling'wenya baada ya kutoka Moshi, straight walifikishiwa Central Polisi DSM na baadae Mbweni Police Station na kamwe hawakuwahi kuwafikisha washitakiwa hawa TAZARA Police Station kuteswa kama wanavyodai...

3. Kuthibitisha hili, Jamhuri au upande wa mashitaka umeleta shahidi polisi wanne lakini walioleta sintofahamu zaidi ni hawa wawili;

å Afande Msemwa wa Central Police DSM anayedai ndiye aliwapokea watuhumiwa na kushughulika nao ktk Selo ya C.P.D....

å Afande mmakonde na Mkuu wa Kituo cha Polisi TAZARA anayedai kuwa ktk tarehe hizo wanazotaja watuhumiwa kuwa walipelekwa kituo cha Polisi, TAZARA siyo kweli kwa sababu hakuwahi kuwapokea na hakuna kitu kama hicho ktk kumbukumbu za kituo chake wakati huo yeye akiwa ni kaimu mkuu wa kituo...!!

4. Sasa kwa kuwa polisi hawa wanabisha na ushahidi wao ni D.R za Central Police DSM na TAZARA ambazo pia zilibishaniwa sana na kuonekana ni za kughushi, ilibidi watuhumiwa watumie njia nyingine ili tu ku - prove uongo wa Polisi hawa...

5. Ndipo sasa mshitakiwa wa 2 ndugu Abdilah Ling'wenya akashauriana na mawakili wake kwa niaba yake waombe nyaraka kadhaa toka kwa RPC wa Ilala zitakazoonesha;

å Kama kweli Mkuu wa Kituo cha TAZARA amewahi kukaimu ukuu wa kituo TAZARA kwa nyakati zile alizosema ktk ushahidi..

å Kama kweli kulikuwa na movement order za watuhumiwa hao kutoka Central Police, Mbweni na maeneo mengine. Ndiyo maana wameomba OB, Station Diary, Occurrence Book nk. Nyaraka hizi ni funga kazi na zikifika mahakamani zitaufumua ushahidi Jamhuri wote na watabaki watupu...!

5. Hiyo barua bado haijulikani kama ilipokelewa na kujibiwa na RPC Ilala au la. Lakini kwa steji hii haijalishi sana kama aliipokea au la. La muhimu utetezi wanataka ikubaliwe na kuingizwa kama sehemu ya kielelezo muhimu. Na mengine yatafuata baadae. Na ikikubaliwa, obvious RPC Ilala atalazimika kuzitoa nyaraka hizo kwa mshitakiwa ili zitumike mahakamani kutolea maamuzi. Hili Polisi na Jamhuri hawataki kabisa litokee maana litafunua uongo wa Polisi na itakuwa THE END OF THE GAME...

6. Kwa hiyo, hii barua ya Ling'wenya ikikubaliwa tu iingie kama kielelezo cha ushahidi wa Mohammed Abdilah Ling'wenya inaweza kuwa na athari zifuatazo kwa upande wa mashitaka;

å Kumlazimisha RPC wa Ilala kuwapatia washitakiwa nyaraka hizo walizoomba kitu ambacho kitakuwa hatari sana kwao, maana. huo ndiyo unaweza kuwa mwisho wa uongo wao...

å Inaweza kuukosesha thamani ushahidi wote wa Afande Msemwa wa Central Police DSM na ule wa mkuu wa kituo cha Polisi TAZARA...

Hii ndiyo inayowafanya mawakili wa Jamhuri wapambane kuhakikisha hiyo nyaraka haipokelewi kabisa...!!
Walikatisha Ushahidi Ghafla Ili mawakili wa utetezi wasipate muda wa kuandaa chochote lakini Ukweli Daima Husimama na Shahidi anaye Jitetea ameweka Wazi na ameonesha anajua anacho kisema na Kufanya.

Kukatisha ushahidi wa ghafla ni ili kuwapoteza maboya mawakili wa utetezi kwa sababu ni wazi kuwa mmawakili wa Jamhuri walishaelewa hatari iliyoko mbele yao juu ya hili wanalobishana nalo sasa...

Kwa hiyo kujaribu kuwachanganya, waliamka asb, wakafika mahakamani na kutangaza kuufunga ushahidi wao na lengo likiwa ni kuwasitukiza upande wa utetezi wasimwandae shahidi...

Very unfortunately kwao, kumbe shahidi yuko vizuri na mawakili wa utetezi nao wakawa wako sharp...

Kwa hiyo upande wa Jamhuri hawakudhani kuwa shahidi angeweza kuwa na akili Wa kuja na "counter attack" hatari na matata kiasi hicho kwa kuleta ushahidi wa nyaraka strong kiasi hicho hata kutaka kuimaliza kesi hii mapema hivi. Waingereza husema, THEY WERE CAUGHT BY SURPRISE...

Ni mpaka J'3 tarehe 29/11/2021. Hatujui watacheza vipi na Jaji wao. Lakini it's obvious that, Jaji ana wakati mgumu kwelikweli kuamua. It's either awabebe kwa kupinda sheria au asimame kwenye sheria...
Hivi TUNDU LISSU hawezi Kuja Kujiunga na Hii Kesi?
Hiyo ni GEAR KUBWA. Hii kesi haina uzito wa kumhitaji TL. Kibatala na wwnzake wameshamaliza kazi. Hakuna kesi hapo...!

By the way, kumbuka kuwa, baadhi ya wanaoitafuta roho yake bado wapo. Mmoja mkubwa wao a.k.a JIWE alishakufa. Subiri nao wafe KIROHO na KIMWILI, kisha ndipo aje...
 
Akafungwe mama yako ndioo utafurahiaaa
 
umchambua vyema msomi sizan kama Lay man anaweza hili👏
 
Kiongozi naimani uko salama, naomba niulize maana nimefwatilia hii kesi leo japo kwa twitter ila kuna jambo sijaelewa...

Kwann mawakili (hasa wakili wa shahidi mr kiwelo) baada ya kujua kwamba hii ni very critical issue kwann hakusaini mwenyewe barua? Au ni nini alikwepa kusaini mwenye mpaka akamuachia mr kibatala?

Maana nikijaribu angalia mawakili wa serikali wanakomaa na hii issue!

Naomba nieleweshi mkuu!

NB: naona leo mawakili wa serikali walikua wanatumia kila ku provoke mawakili wa utetezi kisaikolojia...
 
Mawakili wa Serikali kwa nini wanaogopa barua hii isipokelewe?
Akili kichwani mwako, tukutane Monday!!
 
Naungana na wewe jamaa walipaniki kiasi kwamba wakaanza ku attack watu aiseee!! Kazi kweli kweli! Ila nahisi walitumia kama mechanism ya kuvuruga mahakama na kuwatoa mawakili wa utetezi kwenye reli japo hawajafanikiwa!
 
Mkuu umedadavua vizur sana, hongera uko vizur upstairs!! Nimesoma as if nilikuwa naangalia game ya juzi Man city v/s PSG yaan burudani kabisa.Kiufupi hao mawakili wa serikali wameamua leo wapaki bus tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…