Yaliyojiri Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, kesi ya Mbowe na wenzake 3 - Kesi imeahirishwa hadi Nov. 29 2021

Jaji ana jifunga mwenyewe kwenye maamuzi yake. Kuna barua utetezi ulikataa isipokelewe, yeye kwa mapenzi yake kwa hii kesi akaipokea ili kuwafurahisha mawakili wa mashtaka. Bila kujua kita tokea nini baadae. Sasa mawakili wa utetezi wana mwambia kwa sheria ile ile uliyo tumia kuikubali ile kile kielelezo cha mashtaka, itumie hiyo hiyo kupokea hiki kielelezo. Hapo ni pale stering ana kufa kabla cinema haija isha.

Atachomokaje hapo?
Na akikataa hiki kielelezo naona ndio mwisho wake kuendelea na hii kesi. Washtakiwa hawata kubali maaana ataonekana ameegemea upande mmoja.

Mungu tunae mwabudu hutenda kwa wakati. Serikali ya Ccm na mapolisi wake wana kwenda kuaibika soon.
Ndio maana unaona mawakili wamejisahau hadi wana mgombeza jaji wao.
 
Uko sahihi sana...

Lakini yote ya yote, NI GHARAMA KUBWA SANA KUIGEUZA HAKI YA MTU KUWA HATIA na FAIDA NA THAWABU kuu KUIACHA HAKI KUFUATA MKONDO WAKE....

Just imagine...

Eti mawakili wa serikali au Jamhuri wanataka mshitakiwa asitumie njia yoyote possible kisheria ku - prove his/her innocence..!

Wameng'aka na kupaniki kwelikweli kuona mshitakiwa akitaka nyaraka hizo muhimu toka kwa RPC Ilala kuletwa mahakamani ili zitumike kuthibitisha UONGO au UKWELI wa mapolisi hawa wanaojaribu kuthibitisha makosa ya washitakiwa hawa mahakamani....!

Na hii ndiyo shida ya kesi za kutengenezwa/kubumba ili kukomoana...

Jaji Tiganga ana wakati mgumu sana...

It's either aamue kunyoa au kusuka...
 
Kama alivyo pokea kielelezo cha mashtaka kimagumashi ndivyo atakavyo kikataa jumatatu.

Hapa ni lazima utetezi wajiandae kwa mahakama ya rufaa.
 
mkuu hii comment yako imeniuhudhunisha sana ni kweli kabisa jamaa wamekonda sana na nyuso zao zimepoteza nuru kabisa ila kwa vile ni makomandoo wanajitahidi kujikaza tu kiume,wanateseka kwa hila za watu wachache wenye roho za kishetani wanaohisi dunia hii wataishi milele ila wajue tu hakuna marefu yasiyokuwa na ncha na pia what goes around always come around.
 
Mkuu, au mwingine yeyote anayejua haya mambo: hizo SD,OB nk hawa waovu wanaweza kuzichakachua pia au?! Isijekuwa hii weekend yote wataitumia kutengeneza feki za kuleta mahakamani!
 
Mkuu, au mwingine yeyote anayejua haya mambo: hizo SD,OB nk hawa waovu wanaweza kuzichakachua pia au?! Isijekuwa hii weekend yote wataitumia kutengeneza feki za kuleta mahakamani!
Sio laisi ki hivyo, ndio maana Kuna moja waliileta mahakamani Ina pages zimegolewa na pages nyingine zimeongezwa kwa kuwekewa pini. Na video ya cctv camera zitahitajika ya vituo vyote vya polisi vilivyotajwa mahakamani
 
Mkuu, au mwingine yeyote anayejua haya mambo: hizo SD,OB nk hawa waovu wanaweza kuzichakachua pia au?! Isijekuwa hii weekend yote wataitumia kutengeneza feki za kuleta mahakamani!
1. Mosi, kwa upande mmoja inawezekana kabisa iwapo tu mfumo mzima wa utendaji wa serikali kupitia polisi, CID na DPP unaohusika na udanganyifu huu ktk kesi hii inayoendelea unakuwa umehusishwa kila hatua kuandaa uongo huu...

2. Pili, upande wa pili hili ni gumu sana iwapo jambo hili haliuhusishi mfumo mzima wa polisi na serikali kupitia idara za CID & DPP & mahakama...

Na mpaka hapa kila mtu mwerevu na mwenye akili amekwisha kujua kuwa, mpango huu ni wa kikundi fulani kidogo tu cha wanasiasa ndani ya CCM walafi wa madaraka wakiwatumia baadhi ya maafisa wa polisi, idara za CID, DPP na Majaji & mahakimu wachache wasio waadilifu ndani ya mahakama....

Hawa wanadhani adui na kikwazo chao ili kufikia malengo yao maovu ni Freeman Mbowe & CHADEMA kwa ujumla...

SASA, kama ni kikundi kidogo tu ndani ya serikali na polisi ndo kinahusika kuandaa au kutengeneza kesi hii ya uongo, basi ni obvious kabisa hawawezi kuharibu mfumo wote wa utunzaji kumbukumbu na nyaraka ili tu ku - suit evil ambitions zao. Wapo watakaokataa kushiriki ujinga na uovu huu. Na kwa maana hii mtu asidhani kuwa ndani ya serikali hii hii ya CCM hakuna watu wema na waadilifu. Hapana, wapo wengi sana huko polisi, mahakamani, jeshini, TISS etc...

Na dalili za uongo wao kuanikwa wazi, ziko wazi sana.....

Na kwa kifupi kabisa, tunaweza kusema kuwa hawawezi ku - maintain consistency ya UONGO wao before they got caught...!!

You just wait and see..
 
Kiongozi naimani uko salama,

Yes, niko ok
naomba niulize maana nimefwatilia hii kesi leo japo kwa twitter ila kuna jambo sijaelewa...

Bila shaka, nitakujibu kwa kadiri ya uelewa wangu...
Kwann mawakili (hasa wakili wa shahidi mr kiwelo) baada ya kujua kwamba hii ni very critical issue kwann hakusaini mwenyewe barua? Au ni nini alikwepa kusaini mwenye mpaka akamuachia mr kibatala?

Kama unakumbuka, Adv. Kihwelu ameshalitetea hili kwa kusema;

1. Toka mwanzo kule mahakama ya Kisutu wakati wa committal proceedings, Kibatala ndiye alikuwa wakili wa washitakiwa wote watatu

2. Hata sasa katika steji hii, mkuu wa jopo la mawakili wa utetezi ni Peter Kibatala na si kosa barua hiyo kusainiwa na yeye..

3. By the way, wameombwa sheria inayokataza hilo, wameshindwa kuitoa ama japo kunukuu kifungu cha sheria..
Maana nikijaribu angalia mawakili wa serikali wanakomaa na hii issue!

Ofcoz, ni lazima wakomae na hilo kwa sababu kama nilivyosema mwanzo, that, THEY WERE CAUGHT BY SURPRISE....

Hawakutegemea "counter attack" hatari na matata kwao kama hii ambayo inaweza kugeuza mambo mengi kuwa against them...!

And you know what?

Hiyo barua ikikubaliwa na kupokelewa tu kuwa kielelezo cha ushahidi upande wa utetezi, tutashuhudia bonge la U - TURN ktk kesi hii...!
Naomba nieleweshi mkuu!

Nadhani maelezo hayo juu, yanaweza kukupa ufahamu kiasi fulani...
NB: naona leo mawakili wa serikali walikua wanatumia kila ku provoke mawakili wa utetezi kisaikolojia...
Yes, na provocation dhidi ya wenzao ni kwa sababu hizi;

1. Just, ku - panic kwa sababu hatua waliyoichukua upande wa utetezi kupitia kwa mshitakiwa wa pili Mohamedi Abdilah Ling'wenya baada ya kupendelewa ktk mapingamizi yaliyokwisha kutolewa maamuzi, hawakuitegemea na ina threaten kuwatupa nje na kudhihirisha hila na uongo wa ushahidi wao na mashitaka kwa ujumla...

2. "Umafia" wanaoutumia kujipatia nyaraka fulani fulani bila kufuata sheria tena zingine mahakama ikiwa ndiyo custodian wake, imewashitua na kuwashangaza na kuleta panic upande wa Jamhuri hata kujiuliza wamewezaje kupata akili hii...

Hili hata Judge linampa wakati mgumu. Ameingia ktk mtego ambao ili ajinasue ni lazima ajichanganye tu. Na akijichanganya tu atawapa upenyo upande Wa utetezi kupiga nyundo....!!!

3. Wala usiwe na shaka, mtu yeyote anayeshindwa kutetea hoja na akaanza kum - provoke mwenzake, basi tambua kuwa ameshashindwa...

Hawa Jamhuri na Polisi wao, UONGO wao utawekwa wazi zaidi na zaidi very soon...
 
Mkuu asante sana kwa ufafanuzi huu.....I wish watu wema walio kwenye nafasi za kufichua hila chafu zinazofanywa na waovu hawa wafanye hivyo kwa wingi....wapuuzi hawa ni wa kukomeshwa kabisa.
 
La 'kubumba' halina ubani. Litasambaratika vilevile kama zilivyo kazi nyingine za shetani. AMEN
 
Hii kesi ni biashara ya kutakasia kodi zetu,
 
Mkuu umedadavua vizur sana, hongera uko vizur upstairs!! Nimesoma as if nilikuwa naangalia game ya juzi Man city v/s PSG yaan burudani kabisa.Kiufupi hao mawakili wa serikali wameamua leo wapaki bus tu.
Safi
 
Usiwe na matumaini kwenye hii kesi, judge, mawakili wa serikali, na mashahidi wao wote ni timu moja, wanafanya kazi kwa kusaidiana kila mmoja kati yao kwa nafasi yake.

Kilichobaki sasa ni kusubiri kukata rufaa tu mahakama ya rufaa.
 
Mkuu The Palm Tree ,umemaliza kila kitu kwa lugha nyepesi.
Kongole.
Mungu akubariki sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…