Yaliyojiri Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwenye kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa hadi - Nov 10, 2021

Hii kesi mpaka hapa inakatisha tamaa, mahakama haipo huru haki inadhurumiwa

Sishauri mawakili wa utetezi wajitoe kwenye hii kesi, waendelee kukomaa maka mwisho ili kuithibitishia dunia kuwa kwa tanzania si lazima mpaka uwe na hatia ndio ufungwe
 
Mbona leo wakili wa serikali katumia muda mrefu sana kumwongoza mteja wake?
Kama sikosei Huyu wakili wa serikali alianza tokea jana kumwongoza kwa maswali mteja waje
 
Shahidi Mahita: Tukiwa Himo na washtakiwa gari ilipata pancha..

Shahidi Jumanne: Tukiwa Himo na washtakiwa gari ilipata hitilafu ya mfumo wa umeme..
ha ha ha kesi za kubumba hizi ni lazima ukosee kosee tu ushahidi !! Sema yote ni yote Jaji kawabeba sana kwenye hii kesi ili kuwafurahisha mabosi wa chama tawala.
 
Mpaka hapa mimi bado sijaona ushahidi wa nia na zana za kufanyia ugaidi zaidi ya maelezo tu.
 
Kibatala: OBJECTION Hakuna Mahala Shahidi amesema alifika Central

Jaji: si ndiyo anatoa Ushahidi Wake sasa, We Ulitaka Umsikie wapi?

Kibatala: Ninachosema hiyo ni Leading Question

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji labda Usome Swali la Mwisho

Jaji: Nilijaribu kumuhoji saa 6 na Dakika 51 Usiku

Kibatala: Wapi sasa kataja Central

Jaji: Hakuna


Huyu jaji ni wa mchongo
 
Jaji ni jipu
 
Fredrick Kihwelo 2. Mshtakiwa wa tatu aliteswa katika kutoa Sahihi yake, Katika Maelezo ambayo hajawahi kuandika Kwa Maelezo yake huko Kituo cha Polisi Mbweni, na Hakuruhusiwa Kusoma hayo Maelezo
kwa nini Jaji asiruhusu medical examination ifanywe ili mahakama ijiridhishe kwamba je ni kweli mshitakiwa wa tatu aliteswa na kuninginizwa kama mshikaki kabla ili kumlazimisha asaini malelezo ambayo hakuyatoa yeye.

Hizi ni tuhuma mbaya mbaya sana, Jaji aruhusu tu uchunguzi wa afya wa mshitakiwa.
 
Jaji nae ni Wakili wa Serikali
 
Huyu jumanne,atakaaa wiki nzima chini ya kiapoo
 
Mawakili wa Utetezi japo mmefaulu kuzuia maelezo ya Onyo ya Mbowe yasipokelewe lakini mna kitu muhimu cha kuchukua hapo. Angalieni anuani ya mshtakiwa upande wa Namba za simu imeeditiwa kama walivyoedit kifungu cha CPA 57(3) kwenye maelezo ya Mohamed Ling'wenya.
 
Ndiyo Maana MUNGU anachukia shahidi wa uongo.
Mithali 6-16-19

Kuna vitu sita anavyochukia Mwenyezi-Mungu; naam, vitu saba ambavyo ni chukizo kwake: Macho ya kiburi, ulimi mdanganyifu, mikono inayoua wasio na hatia, moyo unaopanga mipango miovu, miguu iliyo mbioni kutenda maovu, shahidi wa uongo abubujikaye uongo, na mtu achocheaye fitina kati ya ndugu.
 
Kumbe hili suala ninkufa na kupona. Why waedit jamani, mbona kuchoshana huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…