Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Mbowe na Wenzake: Shahidi Afred Kapala wa tiGO atoa Ushahidi, Kesi kuendelea, Nov 03, 2021

Lissu alichofanyiwa sio ugaidi..
Azori sio ugaidi..
Saanane sio ugaidi..
Akwelina sio ugaidi..

Mbowe kuhoji katiba--- GaiDiiii kubwa la maadui...

Hivi unajisikia rahaaaaa!! wakati moyoni unajua ukweli ila unajichetua tu...

Inahusiana nini na kuwaombea Watoto wadogo wasiokuwa na hatia Vifo? Hata Mbowe mwenyewe hawezi kubaliana na huu upuuzi
 
Lissu alichofanyiwa sio ugaidi..
Azori sio ugaidi..
Saanane sio ugaidi..
Akwelina sio ugaidi..

Mbowe kuhoji katiba--- GaiDiiii kubwa la maadui...

Hivi unajisikia rahaaaaa!! wakati moyoni unajua ukweli ila unajichetua tu...
CCM wapo sahihi kumpa KAMANDA WA ANGA hii kesi.
 
Huyu wakili wa tiGO hakuna kitu anajua, naona Matata na Kibatala ndio wameweza kumuanika wazi...

Data/Information security kwenye makampuni ya simu ni kitu namba moja na sio kuwa ni takwa la kampuni bali ni takwa la kimataifa kupitia ISO...(na kuna hati huwa inatolewa kila mwaka kama sehemu ya compliance)

Huyo bwana mdogo sijui wamemuokota wapi kuwa shahidi anayeshindwa kujua kuwa taarifa za mteja ni za kulinda kwa gharama yoyote
 
Haya wateja mmesikia!! ukigombana na polisi mtaani au ukimchukulia demu ana uwezo wa kwenda tigo kuchukua taarifa zako ikibidi kuzipika kidogo ili akufunge... Kazi kwenu na Tigo yeny
 
Halafu kila kitu kafanya yeye. kupokea maombi, processing na kutoa taarifa. Sasa hiyo ni kampuni au ujinga
 
Lazima wateja walindiwe faragha zao kwa sheria madhubuti kama tunataka kuonekana watu wanaojiwelewa huko duniani.
 
Haya wateja mmesikia!! ukigombana na polisi mtaani au ukimchukulia demu ana uwezo wa kwenda tigo kuchukua taarifa zako ikibidi kuzipika kidogo ili akufunge... Kazi kwenu na Tigo yeny
Tigo wameshemka sana kwenye hili, Police wa uchunguzi akitaka kujua info ni lazima atafute cort order na si police yeye kwenda kupewa print out - hii kitu ni mbaya mbaya mno.

Kesi itatusaidia kujua namna mifumo ilivyo mibovu.
 
kama hujaelewa lengo la kung'ang'ania usiri na hatua zingine za utoaji taarifa za mteja ni kuionyesha mahakama kwamba huu ushaihidi ni wakupika hauna ukweli ndani yake.
 
Mkuu huna akili za kujua umuhimu wa hayo maswali. hukumu zingine ni za maelekezo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…