Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi Februari 01, 2022

Hapo ndo patamu zaidi
 
Ushahidi wa mashahidi wote unazungumzia kukamatwa kwa cc washitakiwa, kuharibika kwa gari njiani, kuandika maelezo, miamala ya pesa, detention register kula nyama choma, kunywa MO energy n.k. hakuna anayetoa ushahidi wa ugaidi. Bure kabisa, ugaidi Sasa nani atatoa ushahidi?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
PILATO yalipomchachia akawaambia WAYAHUDI: Sioni kosa kwa huyu(Yesu)linalostahili kifo, Kuna desturi moja, nimwachie Nani, Yesu au Baraba (naye Baraba alikuwa mwizi), WAYAHUDI wakajibu "Mwachie Baraba!".PILATO akanawa maji (Kama ishara kuwa yeye hahusiki na hukumu ya kifo Cha Yesu!). Huyu Jaji mwishoni atanawa maji Kama Pilato mambo yatakavyomuwia vigumu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kuna maswali yanadsi majibu: -

1. Kwanini akina Bwire, Adamoo na Ling'wenya ni washitakiwa badala ya kuwa mashahidi upande wa jamuhuri? Au soon watabadilishiwa status?

2. Kwanini Denis Urio hayuko pamoja na akina Adamoo kama mshitakiwa (tena namba moja) wakati yeye ndiye aliyechonga mpango mzima wa ugaidi bila magaidi wenyewe kujua au hata kuambiwa kwamba ni magaidi? Kwa nini yuko upande wa Jamuhuri peke yake akitoa ushahidi dhidi ya magaidi aliowatengeneza kwenye fikra zake bila kumshirikusha Free na magaidi wenzake? Je, ni lini atabadilishiwa mashitaka ili aunganishwe na magaidi wenzake?

Kibatala cheza naye huyo jamaa hadi ijumaa kitaeleweka. Lazima atafunguka tu!

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Huyu shahidi abandikwe maswali mpaka wiki ijayo,atasema tu!
 
Huyu Jaji mwishoni atanawa maji Kama Pilato mambo yatakavyomuwia vigumu.
hakuna Jaji duniani anaweza kumtia hatiani mbowe na wenzake, ushahidi una mapengo mengi mno. Na kama akifanya hivyo basi Jaji ataingia kwenye vitabu vya kumbukumbu ya maajabu kupata kutokea katika ulimwengu huu tunaoishi.

Kifupi kina Kigai na genge lake hawasaidiki - Jaji kawabebaa wee ila kaona hawabebeki.
 
Nikweli haibadiliki kulingana na maelezo ya LT urio majibu ya maswali yaliyokushinda kuyajibu ni haya.

1. Mbowe alimtafuta LT urio kwajili ya kumtafutia vijana watakao ambatana nae (walinzi)

2. Mbowe alihitaji vijana mahili wa kufanya kazi ya ulinzi kwake ambao ndo hao alio watafuta Lt denis.

3. Mbowe alimtumia Lt urio pesa za nauli na kuwakusanya hao walinzi aliotafutiwa na urio.

4.;nikweli kabisa mpaka sasa hakuna shahidi hata mmoja aliedhibitisha mahali popote kwa evidence ya kuonekana kuwa mbowe na wenzake ni Magaidi zaidi ya kwenda kuongelea kizimbani baada ya kula makande nyumbani kwao.

Kama mimi ndo ningekuwa jaji ningeamuru Lt urio apigwe bakora 100 za mguvu hadharani kwa kosa la uongo na kuwauza makomando wasio kuwa na hatia kwa tamaa zake za pesa.

#Adamo, Bwire, Ling'wenya, Lijenje siyo magaidi bali ni makomando wazalendo walio uzwa na urio kwa watesi wake kina kingai kwa mgongo wa ugaidi.
 
Kumbuka Pilato pia hakuona kosa la Yesu, ila kwa shinikizo la Wayahudi ikabidi anawe mikono na kusema "Mchukueni wenyewe mkamsulubishe". Huyu Jaji anaweza asione kosa la Mbowe, lakini kwa cc shinikizo la CCM ataishia kunawa mikono Kama Pilato.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza ameulizwa:
Kibatala: Ulisema Kwamba Mohammed Ling'wenya baada ya Kufika Kwa Mbowe Tarehe 24 hujawahi Kuzungumza naye

Shahidi: Hapana, Nilimtafuta bila Mafanikio

Kibatala: Je unasema Kwamba Mbowe aliacha Kuwasiliana na wewe Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 24 July 2020

Kibatala: Kwa hiyo Kwenye Kielelezo namba P 34 Kuna Meseji ambazo Ulimtumia Mbowe Hakujibu?

Shahidi: Zipo

Kibatala: Meseji hizo Ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji ambazo hazikujibiwa na Mbowe Kwa Kuongozwa na Mawakili wa Serikali

Shahidi: Sikuonyesha

Kibatala: Vipi Kuhusu Calls, Ulimuonyesha Mheshimiwa Jaji

Halafu akaja kuuliwa kiujanja:
Kibatala: Ulipo surrender Simu zako zote toka Tarehe 12 August 2020, Ulifafanua Kwa Jaji Kuwa Ulikuwa unatumia Simu gani
Shahidi: Hapana Siku fafanua

Simu alikabidhi tarehe 12.8.2020 halafu akaendelea kuzitumia tena tarehe 24.8.2020. Huyu jamaa anastahili kuwa mshtakiwa wa kwanza halafu wenzake waliokuwa anashirikiana nao kuchonga mashtaka waunganishwe kama washtakiwa
 
Jambo la maana kuliko yote leo kutoka kwenye dodoso za Mh. Kibatala

Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Asubuhi.
 
Siyo kwamba alikuwa "kama" double agent bali ni hakika "alikuwa". Hii hufanywa hivi kwa masnichi wote duniani. Ila tu hatari yake ni pale anaposhtukiwa/anapogunduliwa huwa anakosa upande wa kuegemea maana mzigo wote humlemea na walio wengi wanapogundulika hujinyonga kwa kuwa kila upande humkana.

Ktk uchambuzi wa maelezo ya Urio anadhihirsha kuwa Mbowe hakuwahi kuwa na nia ya kutafuta vijana wa kufanya vitendo vya taharuki bali aliyekuwa na wazo hilo ni Urio pamoja na Kingai "kimtego" wakijiegesha katika hitaji sahihi la Mbowe la kutaka vijana wa ulinzi.
 
Tuwekee provision(s) ya sheria hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…