Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi Februari 01, 2022

Kibatala Leo kakomaa na shahidi siku nzima na Bado hajamaliza!
Kwa sababu huyu ndiye central character wa story nzima...

Akiharibikiwa huyu (na tayari imeshathibitika kaharibu), basi kesi nzima inaishia kwake...

Huyu ndiye mchoraji wa ramani nzima ya ugaidi. Ndiyo maana anaenda kuweka rekodi ya kuwa cross examined na utetezi kwa muda mrefu zaidi kuliko mashahidi wengine wote...

Akivunjwa vunjwa huyu, kesi yote inakuwa imekwisha. Narudia tena kuandika, Denis Urio ameshaimaliza kesi hii kwa faida ya watuhumiwa/washitakiwa..!
 
Jambo la maana kuliko yote leo kutoka kwenye dodoso za Mh. Kibatala

Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Asubuhi.
Kibatala: Mhe Jaji Nauliza Swali la Mwisho halafu nitatoa hoja

Kibatala: Ulisema Bwire Alikwambia Wapo katika Utekelezaji Wa Mpango

Shahidi: Siyo Mpango, alisema Samahani Bro tumeshakengeuka, Tumeshawishiwa na Freeman Mbowe, Na Vijana Wapo Kilimanjaro Katika Utejelezaji
 
Jambo la maana kuliko yote leo kutoka kwenye dodoso za Mh. Kibatala

Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Asubuhi.
Watu mtakesha na kupoteza muda na rasilimali fedha mkifuatilia kesi hii huku muda wa maandalizi au hoja za kupata Time huru na Katiba Mpya ukipita. Kumbukeni muda wa mwanadamu haufidiwi. Ukipita hakuna kuurudisha. Mh Mbowe anapotezewa muda wake ambao angeutumia kukijenga Chama chake; CHADEMA, kuandaa mazingira ya Watanzania kutambua umuhimu wa Tume Huru ya uchaguzi na madai ya Katiba Mpya. Mara vuuup, uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu huu hapa
 
Tuwekee provision(s) ya sheria hiyo.
PROHIBITION FOR ACTS OF TERRORISM
4(1) No person in the United Republic and no citizen of Tanzania outside the United Republic shall commit terrorist act and a person who does an act constituting terrorism, commits an offence, unincorporated association or organisation;

(2) A person commits terrorist act if, with terrorist intention, does an act or omission which;
(a) may seriously damage a country or an international organization; or

(b) is intended or can reasonably be regarded as having been intended to;

(i) seriously intimidate a population;

(ii) unduly compel a Government or perform or abstain from performing any act;

(iii) seriously destabilise or destroy the fundamental political, constitutional, economic or social structures of country or an international organization; or

(iv) otherwise influence such Government, or international organization; or

(c) involves or causes, as the case may be

(i) attacks upon a person's life which may cause death;

(ii) attacks upon the physical integrity of a person; (iii) kidnapping of a person,
 
Mkuu point- halafu imeweka watu pale Mh. Kibatala na Genge lake wanauliza maswali hayana maana siku 3
 
Niseme tu lugha ya kiingereza ndiyo kitu kihumu zaidi katika maisha yako. Mbona hapa imetumika lugha nyepesi kabisa ya kisheria kwamba kusudio la kutenda kosa lenye kuhatarisha taifa ama taasisi. Maana yake kuna ingredients zinatakiwa kuwepo kwenye hiyo act or omission.

Sasa unadhani mawakili waandamizi wa serikali hawajui kwamba hiyo provision ipo hadi leo wasiitumie?

Wanajua vizuri ila haiendani na case at hand maana hakuna hata ingredient moja iliyopo kwenye mashitaka haya.
 
Yaani ni full kujichanganya...

Hebu fikiri hivi;

1. Simu zinakadhiwa na kushikiliwa polisi tangu tarehe 12/8/2020...

2. Shahidi anakutana nazo mahakamani Januari, 2022...!

3. Lakini cha ajabu simu hizo zinaonekana kutumika hapa katikati. Zimetokaje polisi? Wao wabumba kesi bila shaka wanajua..

4. After all kuna hili very interesting, kuwa, hakuna uthinitisho/risiti ya makabidhiano iliyopelekwa mahakamani kuonesha kuwa hizo ni mali za Urio na zilikuwa polisi kwa uchunguzi...

5. Tuwape kongole jamani mawakili wa upande Wa utetezi kwa sababu wanafanya kazi kubwa na ngumu sana kumwokoa M/Kiti toka ktk midomo ya hawa simba wala watu...

Wanaendelea kuthibitisha pasipo shaka kuwa, mashtaka hayana ukweli wa uhalisia kwa sababu ni ya uongo wa kutungwa na watu wakiwa wamekaa ofisini...!!
 
Du!
 

Kwahiyo unashauri nini kifanyike mkuu?
 
Ndiyo maana mahakama husikiliza pande zote na kupima nguvu ya ushahidi.

Ushahidi wa Urio umejaa story tu, lakini pia una tofauti nyingi Sana na kubwa, juu ya maelezo yake mwenyewe aliyoyawasilisha mahakamani hapo awali, lakini pia bado anatofautina na haohao wenzake akina kingai kwa kiwango kikubwa.

Matobo haya yanaufanya ushahidi wake kuwa wa mashaka sana juu ya ukweli wa kile anachoki "hadithia".

Pamoja na kasoro zake hizo bado hakuna hata sehemu moja ya maelezo yake alipofanikiwa kuithibitishia mahakama kuwa Mbowe alikuwa na nia ya kutenda au palipo na viashiria vya nia hiyo.

Kinyume chake aliyekuwa na nia ya kutenda ugaidi ni Urio aliyekuwa akitaka "kuiegesha"nia hiyo kwa Mbowe kupitia hitaji sahihi la Mbowe la kutafuta ulinzi.

Comte kubali kuwa Urio na Kingai walishindwa Sana ktk dhamira yao ya kishetani na vyeo walivyo tunukiwa kutokana na kazi hii ya uovu wavuliwe maana wamepoteza fedha nyingi Sana za serikali bila mafanikio, zaidi tu ni aibu kubwa kwa serikali na kuiongezea chuki kutoka kwa Wananchi.
 
Draft la Kingai na genge lake lishagoma - Mashahidi wote hadi leo hakuna aliyethibitisha pasi na shaka kosa la Ugaidi la Mbowe na wenzake !! Huyu URIO ndiyo kabisaa kaithibitishia mahakama kwamba Kina Adamoo ni watu wazuri.
Ila Yale Maelezo ya kina Adamoo ya kukiri Kutenda Ugaidi. Walikataa kuwatambua walitoa chini ya Mateso kwenye ile Kesi Mdogo.
 
shikamoo Kibatala! Alimkona vizuri sana!
 
Kaulizwa swali zuri kwamba kwanini Simu za Mbowe hazijakamatwa kuthibitisha mawasiliano baina yao!????? Wanajua hayo mawasiliano wameyachonga ndo maana wana simu za urio ila za Mbowe hawakuzikamata maana ni mchongo
 
Jambo la maana kuliko yote leo kutoka kwenye dodoso za Mh. Kibatala

Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Asubuhi.
Hilo sio jipya kwani Iko wazi mashtaka waliyo nayo hayana dhamana!Wala hakuna anayetegemea baada ya kuahirisha kesi Jaji aseme wastakiwa wataenda nyumbani!
Grow up,achana na hizi petty issues zisizo na maana!
 
Leo Lumumba wamekuwezesha bando kubwa mpaka unageuka bush lawyer.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hilo sio jipya kwani Iko wazi mashtaka waliyo nayo hayana dhamana!Wala hakuna anayetegemea baada ya kuahirisha kesi Jaji aseme wastakiwa wataenda nyumbani!
Grow up,achana na hizi petty issues zisizo na maana!
ZINA MAANA MKUU SANA KULIKO LILE SWALI NA KIREFU CHA DCI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…