Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Bado hawakuwa smart, watu smart wenye ueledi wa kazi wangetafuta ushahidi usio na makando kando.

Simu zote za smartphone zinauwezo wa kurekodi sauti ukiwa unawasiliana huyo shahidi ambae ni komando ameenda mpaka Sudani alishindwa vipi kurekodi hata sehemu ya maongezo ambayo yangeonesha kuna element za ugaidi unapangwa.

Ni sahii zaidi tukisema shahidi alikuwa anasaka teuzi kupitia kumbambikia Mbowe kesi na kuwachoma vijana wenzie. sababu wote tunajua kipindi cha awamu ya Hayati ulikuwa unapanda cheo aidha kwa kusifia au kuumiza wapinzani sasa shahidi wakaona atoke na kubwa sijui alitegemea kuwa Meja au Kanali baada ya kazi ya usaliti na usinichi
 
Sasa maswali mnatoa makomando wangapi zinahusiana vipi na kesi hyo?
Mawakili wa utetezi wanatafuta malumbano yasiyokuwa na maana
 
Menda
Nenda katoe ushahidi Kama kweli ni smart,otherwise wewe ni mropokaji tu.
 
Serikali ifikirie sana kuhusu kesi hii na itoke na uamuzi wa win win situation. Ushahidi wa leo ni ushahidi wa kufikirika.
 
Kuhusu kukata miti barabarani kwenye mikoa mbalimbali:
Je,
1.Hao wanne wangekata miti mingapi?
2.Wangetumia muda gani kukata miti ya kutosha kuleta taharuki
3.Wangegawana mikoa?
4.Wangekata miti kwa muda gani kabla ya kukamatwa.


What is the average IQ of Tanzanians?
 
Ila mm kwa akili zangu za kiraia, ningekua jaji hii kesi ningetoa maamuzi madogo ya kesi kuu.... 😂😂😂Kwanza baada ya huu ushahidi wa Urio ningewaachia makomando wote huru, ningefuta mashitaka ya ugaidi, Kisha kesi ingeenda mahakama ya mwanzo huko Mbowe na Urio ndo wasutane huko.... 😂😂, ningeamuru posho zirudishwe nusu kwa serikali zikajenge madarasa
 
Haya toa huo ushaidi wa Mboe kutaka kumuua Sabaya
 
Wadau naomba kuuliza maana ushamba siyo ugonjwa. Huyu mleta bandiko ni njia gani huwa anaitumia kuandika taarifa ya kile kinachoendelea mahakamani?
Mimi huwa sielewi yaani mahojiano yanafanyika papo kwa papo then maelezo yanaletwa humu kama yalivyo je, ni njia gani huwa inatumika kunyakua taarifa na kuzibandika humu bila kukosewa?

Ushamba siyo ugonjwa.
 
Anyways defense wana maswali mepesi mno.
 
Kwanini Jaji asimalize kesi hii hapahapa .maana naona dhahiri ni matumizi mabaya ya hela zangu ninazokatwa kama PAye. wangezielekeza hizo hela kwenye kushughulikia changamoto zingine za msingi za nchi.Halafu hawa walioandaa huu upuuzi wote wastakiwe kwa makosa ya uhujumu uchumi.tuanze na huyu huyu urio na yule DCI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…