Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

naona pia wanamkingia shahidi kifua,hawataki aulizwe maswali .kwa nini wamemleta mahakamani?
Sheria ya ushahidi ina masharti yake na imetoa mwongozo ni swali gani linafaa kuulizwa na kujibiwa, ni wajibu wa mahakama kusimamia kuwa yale maswali yanayokubaliwa na sheria ndio yanaulizwa, sasa huyu wakili anajiulizia tuu maswali ya hovyo kama lileswali waliokuwa wa namuuliza shahihidi habari za baba yake aliyekuwa IGP
 
HJawa Mawakili wa serikali waoga sana.Na wanapenda kupoteza ladha ya hadithi yetu
 
1. Mamalaka inayaamua kutengeneza kesi za michongo ni CCM
2. Sio swali
3. Hakuna hatua zitakazochukuliwa kwa sababu CCM enjoys inflicting pain to innocents
 
Aise huyu wakili Nashon Nkungu ni hatari na nusu. Anatiririka kama kameza vifungu vyote kichwani.

Hapo bado Peter Kibatala ndo mziki mnene. Huyo afande Urio atatema bungo kwa maswali atakayochapwa. Hapo tuombe Jaji aje na hitimisho kwamba shahidi ajibu maswali yote atakayoulizwa na mawakili wa utetezi.
 
Leo Naahon amenifurahisha;
1. Shahidi unajua baada ya kesi hii utaibuka shujaa au kituko?
2. Mheshimiwa Jaji naomba mahakama hii kwa wivu mkubwa....
 
Homeboy aliekuja kutoa ushahidi pengine sio Homeboy Original.

Mawakili wa utetezi wana haki ya kumdodosa ili kujua weledi wake kikazi ndio watagundua kuwa huyu ni Urio wa ukweli sio pandikizi la mtu mwingine kwa lengo kutoa ushahidi wanaoutaka wao.
 
Homeboy aliekuja kutoa ushahidi pengine sio Homeboy Original.

Mawakili wa utetezi wana haki ya kumdodosa ili kujua weledi wake kikazi ndio watagundua kuwa huyu ni Urio wa ukweli sio pandikizi la mtu mwingine kwa lengo kutoa ushahidi wanaoutaka wao.
Sitashangaa kama Jaji akiailisha kutoa uamuazi mpaka kesho ili wapate muda wa kumcoach Urio ....!!
 
Shahidi Urio ameeleza mahakama kwamba alikabidhi simu zake kama vielelezo kwa ajili ya investigation.Lkn kumbuka kuna shahidi mtaalamu wa forensic ambaye alikwishatoa ushahidi wake kwamba ktk investigation hakupata text wala video kwenye vile vielelezo alivyofanyia kazi.
Leo shadidi anaeleza mahakamani kuwa kuna txt za telegram za mawasiliano kati yake na Mbowe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…