Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3: Shahidi wa 13, Tumaini Swila ashindwa kufika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2022

Huyo shahidi atakuwa ni slow learner ndio maana anapata shida sana kukariri hadi anaugua kwa sababu mind becomes too obsessed.

The government called the music 🎶 let her play to its tunes now.
 
Tuwape muda waendelee kujipanga. Ila siku nyingine waweke mashahidi wenye afya zinazoeleweka. Lakini wajue kuwa wajipange wajipangavyo ila wakifika kizimbani, Fimbo tunawachapa. Mpaka wakumbuke kusahau kua Tanzania siyo nchi ya wachache
 
Kwa Maana hiyo na airisha Shauri Mpaka Jumatatu Saa 3 Asubuhi na Washtakiwa Wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Siku hiyo
Tusubiri Jumatatu kama mgonjwa atakua amepona aendelee na dodoso, kama hajapona, aanze shahidi mwingine. Kesi imefika patamu.
 
Shahidi hoi. Anaenda kupangwa tena. Tuone atakuwa na yapi jumatatu
 
Na ikatokea shahidi huyu hali yake ya kiafya "ikathibitika na Daktari wa TMJ" kwamba hawezi kuendelea na ushahidi na anahitaji matibabu zaidi kwenye hospitali za rufaa (ambalo "technically" naliona linakuja). Tutaendelea kusubiri ushahidi wa huyu Swila hadi afya yake iimarike kwa huo muda?, wakati tunaendelea na mashahidi wengine kati ya hao 24?
 
Swilla ndo imetoka hiyo harudi ng'oo cross siyo mchezo jamani nilipigwa moja 2019 nilikuwa nawaza siku 5 mfululizo nashukuru Mh Hakimu alinielewa akatoa pumziko nikaenda kunolewa na wakili wangu nikarudi upya nilimwanga mtu nyaaa Ila kwa mbinde Sana jamaa akalipa faini akawa huru
 
Wataalamu wa kuanzisha Nyuzi anzisheni uzi wa kumpongeza Jaji kajitahidi sana kuanzia alipoanza Denis Urio ,kaenda bila upendeleo .
Uko sahihi kabisa. Jaji ameshaona picha nzima ya hii kesi baada ya shahidi wa muhimu kabisa, Luteni Denis Leo Urio. Huyu ndiye amebeba maamuzi ya hii kesi.
 
Kumalizana naye, una maana "kumpoteza"? Swila anaumwa, tumuombee apone aje aendelee na ushahidi wake.
 
Maswali ya kijinga yamesababisha afande nyoka kulazwa.

Taarifa za ndani zinadai kagoma kabsa kuja, na hata jumatatu kawaambia yeye hawezi.
Waende waliomtuma wakapambane na Kibatala.
Ooooh !Kimenuka.

Sema kimeumana
 
Mheshimiwa jaji, kwa niaba yangu na familia yangu, tunapenda kukujulisha kuwa tunafuatilia mwendo wa kesi hii kwa tuo. Aidha kwa mwenendo wa kesi hii mpaka Sasa hatuoni haki ikitendeka maana mawakili wa serikali wamekuwa na visingizio vingi kwa lengo la kuchelewesha kesi na kwa bahati mbaya mahakama yako imekuwa ikibariki mchezo wao. Vyovyote itakavyokuwa, tunaamini haki haijaonekana kutendeka na haitatendeka. Naomba kutoa hoja.
 
Hata hiyo jumatatu lazima atepete kizimbani plus guilty mind inamsumbua.
 
Naitwa Matereka Jayunga nafatilia kwa umakini mkubwa kutoka bariadi mkoani simiyu
Naitwa Jimbi, wewe ndugu Matereka Jayunga kwanini unatumia jina fake? Kwanini?
 
Ushahidi mkuu mbona uko tayari kwenye committal bundle na hakimu alishaona unaweza kutia mtu hatiani?
Mkuu, kwa hiyo huku mahakama kuu kinachofanyika hakina maana yoyote? Siku ukisikia Mbowe amehukumiwa kifungo jela, hutalala kwa furaha. Hawa kina Ndowo, Urio, Swila etc, wanaotoa ushahidi usiokufurahisha wanakuudhi sana.

Ni kipi kinakufanya umchukie kiasi hicho Freeman Mbowe?
 
Ule utopolo wake hauwezi kupokelewa popote.


Tumia kichwa chako vizuri na sio kuongeza uzito juu ya mebega yako
Huyu comte anapenda iwe hivyo. Angependa hawa mashahidi wa jamhuri wasiwe wanafanyiwa cross examination, ili wakileta uongo wao uchukuliwe hivyo ulivyo. Huyu jamaa anapata shida sana na hali ya hii kesi inavyoenda kwa sasa. Tukipata majaji wenye roho kama hizi za comte ni hatari sana.

Huyu jamaa nimemfuatilia kwenye nyuzi za hii kesi, anaonekana ni mtu mwenye chuki sana na Freeman Mbowe.

Siku hii kesi ikifutwa, ataugua huyu.
 
Maswali ya kijinga yamesababisha afande nyoka kulazwa.

Taarifa za ndani zinadai kagoma kabsa kuja, na hata jumatatu kawaambia yeye hawezi.
Waende waliomtuma wakapambane na Kibatala.
Safi sana. Kama mbwai na iwe mbwai. Walimtuma afungue jalada la kesi isiyokuwepo, halafu sasa yeye anateseka na maswali huku wao wamerelax. Na mbaya zaidi hii kesi inaweza kumharibia kazi yeye Swila kuliko huyo Kingai.

comte
 
Maswali ya kijinga yamesababisha afande nyoka kulazwa.

Taarifa za ndani zinadai kagoma kabsa kuja, na hata jumatatu kawaambia yeye hawezi.
Waende waliomtuma wakapambane na Kibatala.
Mkuu ongeza nyama hapo kwenye "kagoma kabisa"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…