Habari Wakuu,
Leo
14/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3. Mawakili wa Serikali waliomba ahirisho la kesi hadi leo Februari 14, 2022 kutokana na Shahidi Tumaini Swila kushindwa kufika Mahakamani siku ya Februari 10, 2022 kutokana na ugonjwa. Awali Februari 9,2022 aliomba ahirisho kwakuwa alikuwa hajisikii vizuri.
Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3: Shahidi wa 13, Tumaini Swila ashindwa kufika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2022
Baki nami.
Updates:
Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 Kamili Asubuhi
Kesi Namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
- Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Ignasi Mwinuka Mawakili Wa Serikali Waandamizi na
- Wakili Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
- John Malya
- Faraji Mangula
- Nashon Nkungu
- Fredrick Kihwelo
- Livino Haule
- Edward Heche
- Sisty Aloyce
- Seleman Matauka
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo shahidi namba 13 ameweza Kufika Kwa ajili ya Kuendelea Kutoa Ushahidi Wake ambapo Upande Wa Utetezi Walikuwa wanahoji Maswali ya Dodoso. Tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari Kuendelea
Inspector Tumaini Sosthenes Swila anapanda Kizimbani na Kaunda Suti ya Kijivu kisha anasimama..
Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa kabla Shauri halijahairishwa ulikuwa Chini ya Kiapo na leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nakumbuka Nilipo Ishia naomba Nipewe Kielelezo Namba P4, P5 (Risasi na Maganda Yaliyo tumika)
Kibatala: Shahidi Unakumbuka Mara ya Mwisho Zoezi lilisimama Kwa sababu Ulisema unataka Kupata huduma za Afya
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Na kweli ulitoa Kauli hiyo Ukiwa kwenye Kiapo
Shahidi: Ni kweli
Kibatala: Una Daktari Wako au Una Daktari Wako Mahususi
Shahidi: Kimya
Shahidi: Nahudumiwa na Madaktari tofauti
Kibatala: Unahudumiwa kwa Muda gani
Shahidi: Zaidi ya Miaka Miwili
Kibatala: Wanaitwa nani
Shahidi: Namkumbuka Mmoja anaitwa Mohammed
Kibatala: Mohammed nani
Shahidi: Simkumbuki
Kibatala: na Amekuhudumia kwa Muda gani huyo usiyemkumbuka
Shahidi: Miaka 2
Kibatala: Je unafahamu Niliandika Barua katika Hospitali ambayo Ulisema Kwamba wanakuhudumia
Shahidi: Sijapewa
Kibatala: Kwa hiyo ujui Kwamba Hospitali imesema ipo tayari Kusema wapo tayari Kuja Kutoa Ushahidi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ni hali ya Kawaida kutomfahamu Mtu anayekuhudumia Miaka 2
Shahidi: kawaida
Kibatala: ulilazwa au ulipumzika nyumbani
Shahidi: Nilikuwa nimepumzika Nyumbani
Kibatala: Nyumbani kulikuwa na Daktari anayekuhudumia
Shahidi: Hapana
Kibatala: Tukoke hapo Nitarudi baadae
Kibatala: Unakumbuka Nilikuuliza Kwenye Viashiria Vya Ufadhili wa Ugaidi
Shahidi: Nakumbuka
Kibatala: Ni sahihi Tulikomea eneo la Fedha
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Shahidi Tulikubaliana Kwamba Mshtakiwa wa kwanza, Wapili na watatu Walitumia pesa zao Kuja Morogoro
Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Nauli ya Mohammed Ling'wenya kuja Morogoro ilitolewa na Baba Yake
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Hukupeleleza hilo eneo
Shahidi: Sikupeleleza
Kibatala: Uliona Siyo Muhimu
Shahidi: Ndiyo Siyo Muhimu
Kibatala: Je Kwa Ufahamu Wako Baba yake Mohammed Ling'wenya alishawahi Kuhojiwa Ofisi ya RCO Mtwara
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Jeshi la Polisi Kila Mtu anajifanyia kazi yake au Mnafanya Kwa Pamoja
Shahidi: Tunafanya Kazi kwa Pamoja
Kibatala: Je Uliwa Kufahamu Kwamba DCI akimuelekeza Kingai Kumuhoji Baba Yake Mohammed Ling'wenya kupitia RCO Mtwara
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Source Zako ni Maelezo Ya Denis Urio, Inspector Ndowo Kutoka Cyber Forensic na Washtakiwa Wenyewe, Je ni sahihi
Shahidi: Ni Maeneo Mawili siyo Matatu
Kibatala: yataje
Shahidi: Kutoka Kwa Denis Urio na Taarifa Iliyo andaliwa kutoka Maabara
Kibatala: Kwa hiyo Taarifa Ya Maelezo ya Watuhumiwa Kuhusu Pesa walizotumiwa siyo Sehemu ya Eneo Muhimu
Shahidi: Ni Eneo Muhimu
Kibatala: Kwa hiyo NI Eneo la Tatu
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Tukianza na Denis Urio, Fedha ambazo anasema aliwapatia Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya aliwapatia kwa Matumizi yapi
Shahidi: Kwa Lengo la Kukutana na Freeman Mbowe
Kibatala: Ni sawa sawa na Kusema Aliwapatia Fedha hizo kwa Matumizi ya Nauli
Shahidi: Ni sawasawa
Kibatala: Kwa hiyo Wakili wa Serikali Pius Hilla alipo pinga Kwamba neno nauli Je alipatia au alikosea
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Tunapinga hilo swali, Sisi tunapinga alipokuwa ana refer Kuna zile pesa zilikuwa za Nauli
Kibatala: Mheshimiwa Jaji wacha Niendelee eneo lingine, ila Mtu akisimama awe na Kitu cha Msingi
Kibatala: Shahidi Kwahiyo pesa hiyo Walipewa sababu ya nauli
Shahidi: Sahihi ya nauli na Matumizi Mengine
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Washitakiwa Wame Elezea pesa hiyo Katika Maelezo Yao
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Fedha hizo pia zime zungumzwa katika Maelezo ya Luten Denis Urio ambayo Uliandika Wewe
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unakumbuka Luteni Denis Urio alisema aliwapatia TSh ngapi
Shahidi: Ni TSh 195,000 na Kisha TSh 199,000
Kibatala: TSh 195,000 zinaonekana katika Maelezo Ya Washitakiwa Wote Ya Onyo?
Shahidi: Ndiyo zinaonekana
Kibatala: Katika Figure hiyo?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu hayo Kwa sababu Wewe Kama Mpelelezi Makini na Mzoefu Kwa sababu Ulitake Trouble ya Kusoma na kuelewa
Kibatala Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P4 na P 13
Kibatala: unafahamu Kwamba Adam Kasekwa alisema Kuwa Sehemu ya Fedha alizopewa alitumia Kununua Shati la Mauamaua ambalo alikuwa amelivaa Siku anahojiwa.
Shahidi: Nakumbuka Maneno Kwamba alinunua Shati lenye Maua Maua
Kibatala: Kwa Upelelezi Wako Wewe hilo Shati lenye Maua Maua linahusika Vipi na Ugaidi (Maana alitumia Fedha Kununua Shati lenye Maua Maua)
Shahidi: Ni Fedha ambazo zilitolewa na Freeman Mbowe Kwenda Kufanya Vitendo Vya Kigaidi
Kibatala: Kwa hiyo Shati ambalo alikuwa amelivaa lilikuwa ni sehemu ya Ugaidi
Shahidi: Kimyaa
Kibatala: Na Je Kipengele cha Yeye Kununua Shati Mli' rekodi Chenyewe au Hapana
Shahidi: Kilirekodiwa
Kibatala: Kwanini Sasa Unanikataza Kuuliza Kitu Kimoja kimoja
Shahidi: Ukiulizwa Kimoja Kimoja uwezi Kupata Ugaidi
Kibatala: Shika Maelezo ya Adam Kasekwa Kwanza, Katika Eneo hilo Kuna Matukio Kadhaa yalitokea, Tafuta Eneo la Luten Urio alitupa Nauli ya TSh 87,000 /=
Shahidi: Nimeona
Kibatala: Soma Kuanzia hapo tujue nauli ya Kwenda Moshi ni TSh ngapi
Shahidi: Tarehe 24 July 2020 Nilikutana na Mohammed Ling'wenya kasisitiza tuende Morogoro tukakutane Luteni Urio tuliondoka Siku hiyo hiyo na Kukutana na Luteni Denis Urio alituambia kuwa kuna Kazi ya Kulinda VIP kwa Freeman Mbowe na Kwamba Maelezo Zaidi tutayakuta huko huko, kila Mtu alipewa TSh 87,000
Kibatala: kwa hiyo Kila Mtu alipewa TSh 87,000 Ka Nauli
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Na wewe Kama Mpelelezi uliona Kuna Kosa lolote
Shahidi: Hapana
Kibatala: Na wewe Ukaona hapo Kuna Mantiki Kama Mpelelezi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Jumla Walipewa TSh ngapi wote Wawili Kama Walipewa Kila Mmoja TSh 87,000
Shahidi: Walipewa TSh 174,000/=
Kibatala: Tafuta katika Maelezo hayo pesa Iliyo Bakia katika TSh 199,000 ambayo ni TSh 25,000 kama Utaona katika Maelezo Ya Adam Kasekwa
Shahidi: haijaelezwa humu
Kibatala: na wewe Kama Mpelelezi Ulifanyia Vipi Kuhusu hiyo Tsh 25,000,je Uliandikia Maelezo ya Nyongeza
Shahidi: Ya nani
Kibatala: Kwani hapa tunamuongelea nani
Shahidi: Adam Kasekwa
Kibatala: Je wewe Kama Mpelelezi Uliandika Maelezo ya Nyongeza au Kumtaka Mtu amuhoji
Shahidi: Hapakuwa na Umuhimu huo
Kibatala: Mwambie Sasa Mheshimiwa Jaji Tunaipata Wapi hiyo Tsh 25,000
Shahidi: Hutoiona
Kibatala: Uliwahi kufundishwa Kuwa Maelezo Ya Onyo ya Mshtakiwa Yanatakiwa yabebe kila Kipengele ya Fact inayounda shtaka
Shahidi: Sijafundishwa, Siyo lazima ibebe kila kitu
Kibatala: Na wewe hiyo Tsh 25,000 siyo Muhimu kwako
Shahidi: Siyo Muhimu
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Denis Urio anasema Kwamba aliwapa TSh 199,000 kama Nauli Kwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya, Je 199,000 ya Denis Urio Inafanana na TSh 174,000
Shahidi: Zinafanana, Ni sawa na kusema 45 na Mtu Mwingine akasema ni 90 gawa kwa 2
Kibatala: Swali ni kwamba 174,000 na 199,000 zinafanama Vipi
Shahidi: Nishasema zinafanama
Kibatala: Kwa Figure zinafanama
Shahidi: Nishasema zinafanama
Kibatala: Shika na Maelezo ya Mohammed Ling'wenya, Soma Pale Baada ya Mazungumzo Luteni Denis Urio alinipa..
Kibatala: Au anzia Baada ya Kufika tulikutana na Luteni Denis Urio Bar Moja eneo la Msamvu
Shahidi: Nimeona
Kibatala: Soma Mpaka Ufike TSh ngapi walipatiwa
Shahidi: Baada ya Kufika tulikutana na Luteni Denis Urio Bar Moja eneo la Msamvu Bar hiyo Sikumbuki, Baada ya Kufika Luteni Denis Urio alitueleza Kuna Kazi ya VIP kwa Freeman Mbowe, na Siku hiyo hiyo alitutaka tusafiri Siku hiyo hiyo
Baada ya Mazungumzo Luteni Denis Urio Alini uliza huko Mtwara kwenye Kibarua chako ulikuwa unalipwa TSh ngapi, nikasema Posho ya TSh 15,000 basi akasema Nikifika huko niombe Mshahara Wa TSh 800,000 alitupatia TSh 190,000 Fedha ambazo tulinunua Nguo ilituonekane nadhifu
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Fedha hizo walinunulia Nguo
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Luteni Denis Urio aliwapa TSh 190,000
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi Yeye Denis Urio alisema Kwamba Alitumiwa TSh 199,000 na hiyo Tsh 199,000 aliwapa Mohammed Ling'wenya na Mwenzake Adam Kasekwa na Tsh 190,000 anayosema Mohammed Ling'wenya na walipatiwa na Denis Urio. Je hizo figure zote zinafanana au zinatofautiana
Shahidi: Zina fanana
Kibatala: Sawa Shahidi
Kibatala: Na Maelezo ya Kasekwa na Maelezo Ya Mohammed Ling'wenya kwenye Figure ambayo Mmoja anasema Jumla Walipewa TSh 174,000 na Mmoja anasema TSh 190,000 Je zinafanana au zinatofautiana
Shahidi: Zinafanana
Kibatala: 199,000 ukito TSh 190,000 zinabakia TSh ngapi,
Kibatala: Je Katika Maelezo ya Mohammed Ling'wenya tafuta TSh 9000 inafafanuliwa ilitumikaje
Shahidi: Haijafafanuliwa
Kibatala: Na wewe Kama Mpelelezi uliye bobea Wa Zaidi ya Miaka 20 na Ukateuliwa na DCI, Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa hiyo Tsh 9000 ulifanyiaje Kazi
Shahidi: Wote Wanakiri Kupokea Fedha kutoka kwa Denis Urio
Jaji: Sikiliza Swali vizuri Unaulizwa hiyo Tsh 9000 ulifanyiaje Kazi
Shahidi: Ndiyo nilikuwa naeleza, Wote Wanakiri Kupokea Pesa kutoka Kwa Luten Denis Urio
Kibatala: Kwahiyo hapo Ndiyo umefanyia kazi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nikiuliza kwa namna gani utarudia Maelezo ya awali
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Basi Mahakama Imesikia
Kibatala: Soma pale Baada ya Kupokea Pesa hizo kutoka Kwenye Maelezo ya Denis Urio
Shahidi: Niliwapatia TSh 195,000
Kibatala: Sasa soma Maelezo Ya Washitakiwa Wote Wawili Wanaizungumzia Wapi.. Katika Maelezo Ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya
Shahidi: Kimyaa
Kibatala: Nikisema kuwa hawajazungumzia Kuokoa Muda nitakuwa nimekosea
Shahidi: Hawajazungumzia
Kibatala: Je unakubali Kwamba Hakuna Sehemu waliyokiri Kupokea
Shahidi: Amezungumzia Denis Urio
Kibatala: Achana na Luteni Denis Urio, Nataka hiyo Refund kutoka Walipotoka Kuja Morogoro, Swali Je Washtakiwa Wali acknowledge? Simple and Clear
Shahidi: Hawajazungumzia
Kibatala: na hiyo hali wewe Kama Mpelelezi Uliona ni Hali ya Kawaida tuh
Shahidi: Siyo Mimi niliyeandika Maelezo
Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi
Shahidi: Ni hali ya Kawaida
Kibatala: Kwa hiyo hukuhangaika Kutafuta fact Ziada
Shahidi: Nilichukua Jitihada za Kutafuta Fact Ziada
Kibatala: Kwakuwa ni Hali ya Kawaida hukufanyia kazi
Shahidi: Nilifanyia kazi
Kibatala: Haya Ndiyo Utuambie Kuwa Ulifanyia Kazi vipi
Shahidi: Maelezo ya Denis Urio yalikuwa ya Uhakika
Kibatala: Na Maelezo ya Washitakiwa
Shahidi: Na yenyewe yalikuwa ya Uhakika
Kibatala: lini Ulianza Kuona au Kukufikia kati ya Maelezo ya Denis Urio au Watuhumiwa
Shahidi: Maelezo ya Washitakiwa
Kibatala: Wakati una Muhoji Denis Urio Ukiwa na Faida ya Maelezo ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Siku Nne Kabla
Shahidi: Nilikuwa sijayasoma bado
Kibatala: Na Uliyosoma lini sasa Maelezo ya Onyo ya washitakiwa
Kibatala: Baada ya Kuandika Maelezo ya Luten Denis Urio, Ulifanya zoezi la Kulinganisha
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ukaona Kila Kitu Kipo Sawa
Shahidi: Kimya
Kibatala: Sawasawa, Haya Denis Urio anasema Kwamba alitumiwa TSh 500,000 akatoa 300,000 akawapa Bwire na Lijenje na Baadae Waka patikana Vijana wawili akawapa akatoa Tsh 195,000 akawapa Jumla ni TSh ngapi
Shahidi: Jumla ni TSh 495,000
Kibatala: na Je 500,000 Ukitoa TSh 495,0000 inabakia TSh ngapi
Shahidi: Elfu 5
Kibatala: Ilienda Wapi
Shahidi: Ni Gharama za Mtandao
Kibatala: Hiyo Gharama za Mtandao ulitoa Katika Maelezo Ya Denis Urio
Shahidi: Kimya
Kibatala: Kuna Mahala Popote Katika Maelezo Ya Denis Urio ambayo umeandika wewe, Kuna Mahala Popote ameielezea
Shahidi: Hajaielezea
Kibatala: Uliambiwa Kuwa Denis Urio alifafanua hiyo Tsh 5000 hapa Mahakamani
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je hata Wakili Mwenzetu Gladys Fimbari aliwahi Kuzungumzia hapa Mahakamani hii TSh 5000
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Upo Makini na hii kesi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Kama Kuna Gharama Za TSh 5000 kama zimekatwa na Mtandao zilitakiwa tuzione katika Taarifa ya Mtandao
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ndiyo Maana Nikamuuliza Je wewe ni Mpelelezi Makini
Shahidi: Ndiyo Mpelelezi Makini
Kibatala: Wa hadhi ya Kesi ya Ugaidi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwa Ushahidi Wako na Mashahidi Wengine Wanaojenga Kesi, Baada ya Kufika Moshi Mshitakiwa Wa Pili na Watatu walikuwa Wanapita Maeneo ambayo Sabaya anapenda Frequently Kuyatembelea, Ndiyo Ulivyo sema
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: katika ile 699 000 ambayo Mnasema Mbowe alitumia Kufadhili Ugaidi, Ni TSh Ngapi Adam Kasekwa alitumia Kumtafuta Sabaya
Shahidi: Kwa Mujibu Wa Upelelezi Wangu Mbali ya TSh 699 000 Kuna Pesa zingine alikuwa anawapatia
Kibatala: Fedha hizo Zipo Katika Hati ya Mashitaka
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Kwa hiyo Fedha ambazo hazipo Katika Hati ya Mashtaka unaona zinatusaidia sisi
Shahidi: aaaahhh Zinasaidia
Kibatala: Weeeee Kweli Enheeeee
Shahidi: Anainama Chini
Kibatala: Unafahamu Kwamba Kuna Mahala unazungumzwa TSh 80,000 Mbayo Khalfani Bwire wakibafilishana Mikono na Freeman Mbowe
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: TSh ngapi
Shahidi: Ni TSh 80,000
Kibatala: Hiyo Tsh 80,000 Kuiona Katika Shughuli zako za Upelelezi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Uliona Wapi
Shahidi: Katika Taarifa Uchunguzi Wa Kisayansi
Kibatala: Kwani wao wanahusika na Kutunza Mihamala ya Fedha ya simu
Shahidi: Hapana
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe Kielelezo namba P 15,16,17,18,19 Mpaka 20
Shahidi: Ni sahihi Kwamba Taarifa iliombwa Chini ya Ofisi Yako hata Kama ni DCI
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Nakuonyesha Kielelezo Cha Barua namba P16 ya + 01 July 2020 Kutoka Forensic Beaural, Je unaitambua
Shahidi: Ndiyo Naitambua
Kibatala: Uliomba Taarifa za Lini hadi lini
Shahidi: 01 June 2020 - 31 July 2020
Kibatala: Barua Ilisainiwa kwa niaba ya nani
Shahidi: Kamishina Wa Polisi Wa Uchunguzi wa Kisayansi
Kibatala: anaitwa nani
Shahidi NAFTALI J MANTAMBA
Kibatala: Unamfahamu
Shahidi: Hapana Simfahamu
Kibatala: Wewe Kuto Mfahamu huyo ni Jambo la kawaida
Shahidi: Ni Jambo la Kawaida
Kibatala: Kwani Taarifa ya Uchunguzi Iliombwa kwa nani
Shahidi: Na DCI
Kibatala: ambaye DCI alimpa nani Mamlaka ya Upelelezi
Shahidi: Mimi
Kibatala: Kwa hiyo ni sahihi Kutomjua huyo
Shahidi: Ndiyo, Kuwajibika na hilo
Kibatala: umeona hizo Tarehe
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Hizo Tarehe Mliwapa au Walijibunia wao
Shahidi: Tuliwapa
Kibatala: Kwa kupitia Barua ya Tarehe 13 August 2020 Kumbukumbu CID/HQ/KUM/C. 8/VOL VIII/171
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Barua Ilikuwa ya Muhimu au Siyo Muhimu
Shahidi: Ilikuwa Muhimu
Kibatala Katika Ushahidi Wako Umeitoa Barua hii kama Ushahidi Wako Muhimu
Shahidi: Sikutoa
Kibatala: Ulitoa Mahakamani Sababu Ya Kwanini Hukutoa Mahakamani
Shahidi: Sikutoa Sababu
Kibatala: Uliongozwa Kuitambua hapa Mahakamani
Shahidi: Sikuongozwa hapa Mahakamani
Kibatala: Kwahiyo Barua hii Ndiyo ilipelekea Simu 8
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Ulimwambia pia Mheshimiwa Jaji kuwa Hakuna Simu hata Moja ya Mbowe Katika Simu Mlizokamata
Shahidi: Sikueleza
Kibatala: Bado tupo eneo la Fedha bado sijahama, lakini ilituzungumzie Fedha lazima Twende Maeneo Mengi
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Simu ambayo ilichukuliwa Kwa Mohammed Ling'wenya, Nilisikia Ukisema Kwa Mujibu Wa Seizure Certificate ya Mohammed Ling'wenya haikuwa na IMEI namba
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Na Ukatoa Ushahidi Namna ambavyo Ulipata IMEI namba
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ulifanya Nini Tena Ikumbushe Mahakama
Shahidi: #*06# OK
Kibatala: Ukapata IMEI namba
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Hiyo IMEI namba Uliyopata Ulimwambia Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia Mhe Jaji ni Manufacturer Directives IMEI namba Ikifutika ndiyo Ufanye hivyo
Shahidi: sikumueleza
Kibatala: Je Ulimwambia Mhe Jaji Kwamba Manufacturer au Agent Wa TECNO ndiyo Uliye Kwenda Kwake na akakupa Ushauri Wa Kitaalamu
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Unafahamu Kwamba TECHNO Wana Mawakala Wake Tanzania Wanaofanya Kazi hizo
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba ukijifunza wapi namna ya Kutafuta IMEI
Shahidi: Sikueleza
Kibatala: Hiyo IMEI namba ndiyi Uliweka Katika Barua ya Kwenda Ofisi Ya Uchunguzi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa garbage in and Garbage Out
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Kwa hiyo Wao wamenukuu IMEI namba ambayo wewe Ndiyo Ulipata
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Report ya Inspector Ndowo Wewe Uliona?
Shahidi: Niliona
Kibatala: Umemwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa hiyo IMEI namba, Kwamba Riport Uliyopata Ulilinganisha NA IMEI namba ya Mchunguzi Ukaona zinafanana
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu Maana ya authentication
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba Simu zinaweza Kuingiliwa
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba IMEI namba ni DNA ya Simu
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Mwenye Simu Mwenyewe amezungumzia Lolote Kuhusu IMEI namba ya Simu yake
Shahidi: Naomba Maelezo nijikumbushe
Shahidi: hakueleza
Kibatala: Tafuta kwanza Katika Maelezo Ya Mohammed Ling'wenya Kuna Mahala Popote ametaja Kuwa SIMU zake zote Mbili ametaja ICCID
Shahidi: Hakutaja
Kibatala: Na Kurudisha Kwenye Barua Ya Kutoka Polisi kwenda Airtel, Soma namba zote Tatu zilizoombewa Taarifa Airtel
Shahidi: 0784779944, 0782 237913 na 0787 555200
Kibatala: Nenda Katika Taarifa Ya Gladys Fimbari, Je alitoa Namba zinazo one kana Katika Mihamala alitoa Taarifa za Mihamala Ya Simu Ngapi
Shahidi: Namba Mbili za 0784779944 na 0787 555200
Kibatala: na Hapo unasoma Katika Kielelezo namba P 15
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unakubaliana na Mimi Gladys Fimbari aliombwa Miamala ya Namba 3 ila Yeye Katika Barua yake Miamala Ya Simu 0782 237913 imeachwa
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu Record ya Miamala ya Gladys Fimbari Kutoka Airtel Imetokana na Barua ya Polisi Kwenda Airtel
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nenda Katika Taarifa Ya Mihamala Kielelezo namba P 20, Mhamala Wa Mwisho kabisa wa Tarehe 31 July 2020
Shahidi: Nimeona
Kibatala: Angalia namba Iliyotuma fedha
Shahidi: 0784779944
Kibatala: Namba iliyotumiwa 0782 237913
Kibatala: Unakubaliana na Mimi namba" 0" inamiss
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Katika Barua yenu ya Kwenda Airtel, Je namba sifuri ilikwepo au Haikuwepo
Shahidi: ilikuwepo
Kibatala: Wewe Ndiyo ulimuandika Maelezo Gladys Fimbari
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Uliandika Sababu ya Kutofautiana hiyo Prefix ya "0"
Shahidi: Sikumuuliza, Kwa sababu...
Kibatala: SITAKI SABABU HAPA MIMI
Kibatala: Nenda Kwenye Barua, Ni sahihi Kwamba namba iliyotumiwa hapo Ndiyo namba ambayo ipo Kwenye Barua
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwanza imetumiwa TSh ngapi
Shahidi: 200,000
Kibatala: UNASOMA WAPI WEWE, KUWA MAKINI
Shahidi: Ni TSh 80,000
Kibatala: Je ni sahihi Kwamba namba iliyotumiwa TSh 80,000 ndiyo namba iliyokuwa Kwenye Barua Ya Polisi Kwenda Airtel
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Lakini hiyo namba katika Covering Latter ya Airtel hiyo namba Haipo
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Je unafahamu Legal Implication ya suala hilo
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Lakini Ulimuhoji Gladys Fimbari Tarehe 05 July 2021
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Je Ulifanyia Kazi hiyo tofauti
Shahidi: Sikufanyia kazi
Kibatala: Ndiyo Maana Nilikuuliza Unafahamu Maana ya legal implication
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: angalia Muamala Wa Tarehe 20 July 2020, Ukitumwa kutoka namba 0780 900174 kwenda namba 0787 555200, Je Ulisoma Taarifa za Miamala Vizuri kama Mpelelezi
Shahidi: Nilisoma na kuzielewa
Kibatala: Na ni sahihi Kwamba Moja ya Source zako za Information Mpaka Kusema Mbowe alifadhili Ugaidi Ilikuwa ni baada ya Kusoma na Kuelewa Taarifa za Miamala
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ulifahamu, Kwamba hii namba ni ya Wallet
Shahidi: Hapana Nilizingatia Covering letter ya Kutoka Uchunguzi
Kibatala: Wewe Unapeleleza Faili, Kupitia Forensic Beaural, na Yeye Kwakuwa hakuwa na Utaalamu akaomba Kutoka Airtel, Na Ndiyo Mwanzo Nilikuuliza Kwamba Unafahamu Hizo Taarifa
Shahidi: Ndiyo Nilifanyia kazi
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi amesha Jibu hilo swali Akasema hafahamu Kuhusiana na hii namba, Kwa hiyo tunaona Swali linajirudia hapa
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Hakuna Swala la Kanuni hapo, Kwa sasa Kwa sababu ni Mapema, Wacha Niendelee, ila baadae nitawahoji Kwa Sheria ipi kwa Kanuni ipi
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ilikiwa ni Maamuzi yako, Wala Siyo Sheria Wala Kanuni
Kibatala: Nishasema kuwa Kwa sasa naendelea ila wakiendelea hivyo Tutaomba Ruling sababu hili ni zoezi la Truth Findings
Kibatala: Wewe Binafsi kama Inspector Swila Ulisoma na Kuelewa au Ulisoma hukuelewa
Shahidi: Nilipitia lakini Sikuelewa
Kibatala: Kwa hiyo tuachane na hiyo Taarifa, Sababu hujaielewa
Shahidi: Anayeweza Kufafanua hiyo ni Mtu wa Airtel
Kibatala: Sawasawa Nimekuelewa
Kibatala: Haya Kuhusu KYC unazijua
Shahidi: Kwa kiasi Chake
Kibatala: lakini ulizo fanyia kazi KYC za Denis Urio na Mbowe, Mohammed Ling'wenya
Kibatala: Kwa hiyo ulizielewa au hukuzielewa
Shahidi: Nafahamu Vitu baadhi
Kibatala: Unafahamu Kwamba KYC inayo Purport namba ya Mbowe, Denis Urio na Mohamed Ling'wenya zote Zina namba ya NIDA
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba NIDA ndiyo Primary Source
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba Wewe Kama Mpelelezi Ulipokea Taarifa ili Uchunguze na Kuthibitisha Kwamba kweli I alikuwa na Makosa ya Ugaidi
Shahidi: Sikuwahi
Kibatala: Kwani nani alikuwa Mpelelezi Kati yako wewe na Airtel
Shahidi: Mimi pamoja na Wapelelezi Wengine
Kibatala: Kwa hiyo wewe hukufanya lolote la Kwenda NIDA Kuona Kama Kweli zilikuwa Taarifa zao
Shahidi: Si Kufanya
Kibatala: Je unafahamu Kwamba hiyo pesa iloyotumwa kwenda namba ya Tigo ilitumwa kutoka namba 0719933386
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Mliomba TIGO Taarifa Ya Namba hiyo
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu namba ya Faili ya Mbowe, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Khalfani Hassan Bwire ni CD /IR /2097 /2020
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Ndiyo Ulisema Wewe Ulifungua Faili hilo Tarehe 18 July 2020
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Na wewe Ndiyo Uliandika Maelezo Ya Frank Kapala
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi Pia Ulisema katika Ushahidi Wako Kuwa Ulifanyia Kazi Taarifa za Tigo
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Na wewe Ulisema ni Mpelelezi Makini
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Haya Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Jalada Walilojibu Tigo ni lipi..?
Shahidi: ni CD/IR/ 2097/ 2021
Kibatala: tukumbushe Kuwa Jalada lako ulilofungua ni la Mwaka Gani?
Shahidi: Ni Mwaka 2020
Kibatala: Je Tigo Walijibu Jalada lako kwa Kunukuu Mwaka gani
Shahidi: Mwaka 2021
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulifanya Juhudi gani za Kiupelelezi Ku Reconcile Utofauti Wa Mwaka 2020 na Mwaka 2021
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: na Mhamala unaobebwa na Barua hiyo ni wa TSh 500,000 ambao unasemekana Kwamba Mbowe alimtumia Denis Urio
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unajua Author Wa hiyo Barua
Shahidi: Hapana
Kibatala: Angalia aliyeandika hiyo Barua pale Chini ni nani
Shahidi: Imeandikwa Mwanasheria ila Jina halija andikwa
Kibatala: na wewe Tarehe 08 July 2021 ulimuhoji Mtu anaitwa Kapala
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Sasa Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulijuaje Kwamba Aliyeandika Barua ile ni Frank Kapala
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Nikisema Kwamba Ushahidi Ulikuwa wa Kupangwa kwa fact hizo Nakosea
Shahidi: Siyo Sahihi
Kibatala: Je unafahamu Kuhusu Mihamala ya Tigo ambayo Mnasema Kwamba ilikuwa Mihamala ya Freeman Mbowe
Shahidi: anafahamu Mtu Mwingine
Kibatala: Kwa hiyo Ukiacha Miamala Ya Tigo hii Hakuna Kitu Kingine Unachokifahamu
Shahidi: Kuhusu Miamala anafahamu Denis Urio
Kibatala: Bado tupo Kwenye pesa, Umetaja Mara Kadhaa Kuhusu Taarifa Ya Cyber Kama Moja ya Kitendea kazi chako
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Tutaona nini na nini
Shahidi: Taarifa za Mawasiliano na Usajili Wa Namba za Simu
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P 23 na P 26 Na P22 ya Covering letter
Kibatala: Sasa Shahidi Nakuonyesha Barua Kutoka Uchunguzi Wa Kisayansi Kielelezo namba P22
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Barua Imeelekezwa Kwa nani
Shahidi: Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai
Kibatala: Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai ambaye ndiyo Mlalamikaji
Shahidi: Inaenda Kwenye Ofisi
Kibatala: Kwani Imesema "Kurugenzi " au "Mkurugenzi "
Shahidi: Mkurugenzi
Kibatala: Soma namba ya Jalada iliyobeba Barua
Shahidi: Ni CD/IR/ 2097/2020
Kibatala: Na Barua Iliyo rejewa ni Kumbukumbu namba Ngapi
Shahidi: CID/HQ/C8/9/Vol viii/171/ ya 13 August 2020
Kibatala: Barua ambayo ujaitoa Mahakamani Kama Kielelezo
Shahidi: Sijaitoa Mahakamani
Shahidi: Mheshimiwa Jaji naomba niende chooni
Mahakama ipo Kimya kusubiri Shahidi arudi
Na Sasa Shahidi amerejea Kizimbani
Kibatala: Tunaweza Kuendelea Shahidi
Shahidi: Tuendelee
Kibatala: Je Barua ambayo Haipo Mahakamani Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Kwenda Ofisi ya Cyber Imeandikwa lini
Shahidi: Tarehe 13 July 2020
Kibatala: Na Majibu yamekuja lini
Shahidi: Tarehe 09 July 2021
Kibatala: Kama Kipindi Cha Mwaka sasa
Shahidi: Miezi 11
Kibatala: Walikwambia kwanini Kufanya Extraction tuh Kesi Kubwa kama hii Vielelezo Vinakaa Miezi 11
Shahidi: Walisema Kuna Vielelezo Vingi
Kibatala: Unafahamu Kwamba Tarehe hizo ndiyo zilikuwa za Vuguvugu za Maswala ya Katiba
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Kwenu Kesi hii ya Ugaidi Ilikuwa ni Priority au Mlianza hata Kuchunguza Maswala ya Mapenzi Kwanza
Shahidi: Nisha Jibu
Kibatala: Wakati Nyie Mnasubiri Kwa Speed Ya Kawaida Mlikuwa mnatambua Kuna Watu wapo Ndani
Shahidi: Tulikuwa tunatambua
Kibatala: Wakati kwa Ushahidi Wako Mwenyewe, Ulisema Kwamba Wakina Gabriel Mhina na Khalid Walikaa Mwaka Mzima, Je Mnafahamu Madhara Ya Kukaa Mwaka Mzima
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Madhara Waliyo Pata Washitakiwa Wa Kwanza, Wapili na Watatu Kama Vijana Kwa Kukaa Ndani Muda Mrefu
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Maana ya Polisi Impunity
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ulifanyia Kazi Extraction Reports
Shahidi: Nilifanyia kazi Kwa Ufahamu Wangu
Kibatala: Unafahamu zilikuwa ngapi
Shahidi: Nne
Kibatala: Unafahamu Kwamba Kuna Extraction Report Siku ambayo Covering Latter Imeandikwa
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Walifanya Extraction Tarehe 09 July 2021 Saa 11 na Dakika 29 Jioni
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba Walikuwa Wanakimbizana na nini, hizo Siku Mbili za Mwisho
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Baada ya Kukimbiza Extraction Report kwa Siku Mbili ndiyo Baada ya Siku 12 Mbowe akakamatwa
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Na Unafahamu a baada ya Extraction Report kukamilika na Mbowe Kukamatwa ndiyo Elia Kaaya akaachiwa na Baadae akaja kuwa Shahidi Kwenye kesi hii
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Haya nipeleke hayo Maeneo ambayo yalokuingiza Kufikiria Kwamba Freeman Mbowe alifadhili Ugaidi
Shahidi: Ukurasa wa Nne, Bullet ya Pili
Kibatala: Unasema nini
Shahidi: Kwa Mujibu wa Report ya Tigo ya Tarehe 20 July 2020, Namba Ya Simu 0719933386 ilituma namba Kwemda 0787 555200
Kibatala: Ni sahihi Kwamba hapo amekopi Kutoka Tigo
Shahidi: Siyo Sahihi
Kibatala: Tuambie Sasa Inspector Ndowo alifanya nini
Shahidi: Hapo bullet ya Chini inaposema Kwamba Kwa Mujibu Wa Report kutoka Tigo...
Kibatala: Nitafutie Mahala ambapo Inspector Ndowo Ali Originate Uchunguzi kutoka kwake, Zaidi ya Taarifa Ya Tigo (Mbali na Primary Source kutoka Tigo)
Shahidi: Alifanyia Kazi Taarifa Kutoka Tigo akaanda Taarifa hii
Kibatala: Hiyo kazi ambayo alifanya yeye Inspector Ndowo nauona katika Bullet ipi
Shahidi: Ndiyo ungemuuliza yeye Inspector Ndowo
Kibatala: Kwa Mdomo tena
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Report inatakiwa Kuiongelea Yenyewe
Shahidi: Ndiyo Ungemuuliza Yeye Sasa
Kibatala: Nisionekane na Kuharass, Je Unakubaliana na Mimi Taarifa inayo Tajwa hapo ni ileile ya Tigo ambayo Kwenye Barua ya Tigo ni CD/IR 2097 /2021
Shahidi: Hapana ni CD /IR/ 2097 /2020
Kibatala: Kwani Barua Kutoka Tigo imeandika jalada gani
Shahidi: CD /IR 2097 /2021
Kibatala: Siyo Kuuliza tena hapo.
Kibatala: Haya bullet gani Nyingine inayo zungumzia Kuwa Mbowe akiwatumia pesa
Shahidi: Ya Pili Kutoka Mwisho, 0784779944 imesajiliwa kwa Majina Freeman Mbowe ilituma Pesa Kwemda namba 0782 237913 ilituma Kiasi cha TSh 80,000
Kibatala: Je unafahamu Unachosema hapo Hakipo katika Hati ya Mashitaka
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Sasa Lengo la Kuleta Mahakamani Kitu Hakipo katika Hati ya Mashtaka ni nini
Shahidi: Hizo ni fedha ambazo hazikuweza Kutolewa Maelezo na Denis Urio
Kibatala: Lengo la Kuleta pesa hizo hapa Mahakamani na nini, Zilikuwa ni Mahaba au Ufadhili wa Ugaidi
Kibatala: Ni sahihi Katika Maelezo Yako uliyo andika wewe Unaandika hivi, Vilevile Uchunguzi Wa Cyber Ulikuwa Unaonyesha Mshitakiwa Mbowe akiwatumia Pesa wenzake na Kutoa Maelekezo nini cha Kufanya
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Hiyo Taarifa Wewe Ulipata Wapi Kwamba Mbowe alikuwa anatuma pesa na Kutoa Maelekezo nini cha Kufanya
Shahidi: Kwenye report
Kibatala: Haya nitafutie Kwenye Riport Mahala inaposema Kwamba Mshtakiwa Freeman Mbowe alikuwa anatuma Pesa na Kuelekeza Wenzake nini cha Kufanya (Vitendo Vya Ugaidi)
Shahidi: anapekua Report
Shahidi: Kwenye Report Hakuna
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa katika Report Hakuna Mahala ambapo Mbowe anatoa Maelekezo nini cha Kufanyia Fedha hiyo
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Katika Report Hakuna Maelezo hayo
Kibatala: Infact Ukisoma hiyo Riport anaye Omba Pesa ni Denis Urio
Kibatala: pale Kwenye Wamekwambia Wanataka nini.? Na wa Umri gani (Katika Kielelezo G) page 3 Mpaka page ya 4
Shahidi: Nimeona,
Kibatala: Ni nani anayesema naomba Nitumie nauli kwa ajili ya Kuwa Mobilise nikutane nao Morogoro Kwa Mujibu wa Riport ya Inspector Ndowo
Shahidi: Imetumwa na Denis Leo Urio
Kibatala: Ni sahihi Meseji hiyo inaonyesha na Matumizi ya hiyo pesa
Shahidi: Ukisoma Moja Moja huwezi Kupata Maana halisi
Kibatala: Sijakubishia, Ila tunazumgumzia Kuhusu Report ambayo wewe ndiyo Umesema Kwamba Ni Source ya Conclusion Yako
Kibatala: Sasa Kwa Mujibu Wa Inspector Ndowo, Ni sahihi Kwamba Lengo lipo katika Meseji ni Kuwa Mobilise
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Na Kwa Mujibu wa Riport hiyo nani Kasema "No Problem kaka ni Kwa namba Ipi na Kwa kiasi Kipi"
Shahidi: Ni Freeman Mbowe
Kibatala: Na Kwa Mujibu wa Report hiyo nani Kasema Usiwe unatumia namba yako Kaka
Shahidi: Denis Leo Urio
Kibatala: Katika Maelezo Uliyokuwa Unamuandika, Ulimuhoji Denis Urio kwanini Yeye Kama Mtu wa Kumtoa gaidi pangoni aje aonekane Ushahidi Wake badala yake ndiyo anamfucha gaidi pangoni
Shahidi: Ndiyo alieleza
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Maelezo Ya Luten Denis Urio
Kibatala: Haya Tafuta Mahala ambapo Luteni Denis Urio alifafanua katika Maelezo Yake kwanini anamwambia Mbowe atumie namba ya Wakala au Wasaidizi Wake
Shahidi: Wakati Wa Maongezi Yetu Afande DCI alifanya Mawasiliano, na Baada ya Muda Mfupi aliingia Afande Mwingine
DCI aliniambia ili tuweze Kukusanya Ushahidi Niendelee Kuwatafuta Watu hao, Ili kumweka Karibu
Kibatala: Nitafutie Mahala ambapo Denis Urio anasema alimwambia asitumie namba yake atumie namba ya Wakala au Wasaidizi Wake ilikumweka Karibu
Shahidi: Ili asiweze Kumtilia Mashaka
Kibatala: Hayo Maneno Yapo au hayapo, wewe Umesoma Kielelezo namba P23 Meseji inasema Usiwe unatumia Namba yako, Tumia namba ya Wakala au Wasaidizi Wako, Sasa nataka Sehemu Katika Maelezo ya Denis Urio sehemu ambayo amesema nilifanya hivi ili Ku gain Confidence
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Tunapinga hilo swali, Sababu limeshajibiwa
Kibatala: Naomba Mwenzangu unisomee Nione Kama limejibiwa
JAJI: ulikuwa Umeulizaje Mr. KIBATALA
Kibatala: Nataka Kwa Maelezo Ya Denis Urio Kwamba anitajie sehemu ambayo amesema Kwamba Ile Meseji ya Kumshauri Mbowe Kuwa Usitumie Namba yako, Tumia ya Wasaidizi Wako au Wakala, Je Katika Maelezo hayo Kuna sehemu ambayo amesema?
Shahidi: Maneno hayo kwenye Maelezo Hayapo
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kutoa Hoja, Naomba uridhie tupate Break Kidogo Kama Ilivyo Utamaduni Wetu, Kisha turejee Saa 8 Kasorobo
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi
Jaji na airisha Kwa Muda Wa Dakika 45, tutarudi tena Saa 7 na Dakika 45
Jaji anatoka, saa 7:00
***************************
Jaji amerejea Mahakamani Muda huu 02:18
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani tena
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wa Jamhuri Quorum ipo Kama Awali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia kwa Upande wet Quorum ipo Kama Ilivyo kuwa awali na tupo tayari Kuendelea
Shahidi Karejea Kizimbani
Mwenyekiti Freeman Aikael Mbowe amenyoosha mkono wake wa kulia hapa
Freeman Mbowe: Mheshimiwa Jaji naomba kuleta Kwenye Mahakama yako kuwa tumekosa haki ya kula chakula mchana kwa Miezi 5, Wakati nyie Mna' break kwenda kula sisi hatupati chakula wala maji kwa miezi Yote 5
Pale mwanzo tuliambiwa kuwa kama chakula tuchukue Kutoka Jela, tutoke nacho Jela tuje nacho Mahakamani, tkitoka hapa tunakutana Magereza Wameshakula tunakwenda kulala na njaa siku zote.. Hawa vijana wanakonda kila Siku hata kusikiliza kesi ni geresha.. Ni hayo tu.
Jaji: sasa nyie Kibatala mnatoa uwakilishi gani hapa Mahakamani kama wateja wenu hawali miezi mitano?
Kibatala: sisi tulifkisha kwa Officer wa Magereza, Suluhu aliyotoa ndiyo hiyo Asubuhi Watoke na Chakula Kutoka Jela Kitu ambacho tulibishana na hatukufikia Muafaka kwa sababu haiwezekani.. Nafikiri hata Msajili Wa Mahakama analijua hilo, sutaki kumsemea.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Mujibu Wa Jambo lililo letwa naomba Tubreak Kidogo tuweze Kuishauri Vyema Mahakama.. Imekuwa ghafla sana..
Jaji: basi nawaita Mawakili Kuwakilisha Watu wote Ofisini Kwangu, Tuweze Kujadili
Jaji anatoka 02:27
Askari magereza wamemfuata Freeman Mbowe, anahitajika ofisini kwa Jaji katika kikao cha pamoja na mawakili wa pande zote (serikali na utetezi), Washtakiwa wengine watatu bado wamebakia kizimbani.