Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Sostenes Swila kuendelea kutoa ushahidi wake Februari 08/2022

Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Sostenes Swila kuendelea kutoa ushahidi wake Februari 08/2022

... shukrani sana Mkuu Nyendo kwa kazi hii njema! Nasi tuko tayari kufuatilia shauri hili muhimu kwa mustakabali wa nchi na vizazi vyake.
Mkuu ni mapema sana ngoja mpaka jioni tukiweka vyanzo vingine maana Nyendo ni editor mzuri na huongeza mipasho
 
Yaani huyu kakarishwa tu kusema sio sahihi,hata akiulizwa ulienda msalani muda mfupi uliopita atasema sio sahihi[emoji3][emoji3]
Nashon: Katika Ushahidi Wako Ulisema Uliitwa Tarehe 14 July 2020 kwa Mkurugenzi, Je ni sahihi

Shahidi: Siyo Sahihi

Nashon: Wacha nisome... Wakili anasoma

Shahidi: Ni sahihi
 
Nani anaweza kuandaa Rasimu ya Kitabu kuhusu maisha ya Freeman Aikael Mbowe.

Kitabu kichapwe mwaka 2030 kwa ajiri ya vizazi vijavyo katika vita ya kupigania demokrasia na haki za binadamu Tanzania.

Tittle : The life and times of Freeman Aikael Mbowe. A true son of the soil.

FAM ni tunu kwa wapenda haki wote,tumuweke FAB katika maandishi kwa faida ya vizazi vijavyo. Nipo tayari kutoa fedha na nyenzo kumuweka FAB katika maandishi.

Sina chama chochote lakini napenda ujenzi wa demokrasia na haki za binadamu.
 
Habari Wakuu,


Leo 07/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri kesi inayomkabili Mbowe na wenzake leo Februari 4, 2022. Kesi imeahirishwa. Shahidi wa 13 kuendelea kutoa ushahidi Februari 7, 2022

Updates:

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na
  • Wakili Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Tulimanywa Majige
  • Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

  • Wakili Nashon Nkungu
  • John Mallya
  • Dickson Matata
  • Seleman Matauka
  • Fredrick Kihwelo
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja ambaye alishaanza Kutoa Ushahidi Wake, Tupo tayari Kuendelea

Kibatala: Nasisi pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa Ijumaa Ulikula Kiapo na, Leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Shahidi: Sawa Mheshimiwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Sasa Inspector Swila, Siku ile Tulikomea Tarehe 27 October 2020 wakati unampatia DC Goodluck Bastola Baada ya hapo Ulifanya Shughuli gani Nyingine

Shahidi: Niliweza Kupokea Taarifa ya Uchunguzi na SilahaTarehe 27 November 2020 Nilipokea kutoka kwa koplo Azizi wa Kitengo Cha Silaha na Milipuko Nilipokea Silaha, Bastola aina ya Luger A5340, Risasi Moja, Maganda Mawili ya Risasi pamoja na Vichwa Viwili Vya Risasi

Wakili wa Serikali: Wakati unapokea Taarifa ya Risasi Moja pamoja na Maganda Mawawili, Ni wapi ilipokea

Shahidi: Katika Kitengo Cha Uchunguzi Wa Silaha na Milipuko

Wakili wa Serikali: Uliwezaje Kujua kama Ndiyo Silaha uliyopeleka

Shahidi: Niliweza Kuangalia Serial Namba ya Silaha, Nikakuta ni A5340 na Silaha aina ya Luger

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Risasi Zenyenwe zilikuwa na hali gani

Shahidi: Risasi niliyo pokea ilikuwa ni Moja, Ilikuwa haujatumika, Ilikuwa na Alama A3 na Risasi ambazo zimetumika Nilikuta zimepewa alama ya T1 na T2

Wakili wa Serikali: Nani aliweka alama katika Vielelezo hivyo

Shahidi: Mchunguzi Wa Vielelezo hivyo

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa umepokea Riport na Vielelezo Ulifanya nini.?

Shahidi: Vielelezo nilipeleka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na Kwenda Kuvikabidhi

Wakili wa Serikali: Kitu gani hicho ulienda Kukabidhi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Nilienda Kukabidhi Silaha, Bastola aina ya Luger A5340 na Risasi Moja, Maganda Mawili pamoja na Vichwa Vyake

Wakili wa Serikali: Na Report Ulifanyia nini

Shahidi: Report nilihifadhi na Kufungia katika Kabati langu la Chuma

Wakili wa Serikali: Baada ya Tarehe 27 November 2020, Nataka Kukurudisha Kwanza hapo ambapo unasema Ulikabidhi Risasi Moja, Maganda Mawili na Silaha, Je Ulimkabidhi nani

Shahidi: Nilimkabidhi Sarjent Nuru, ambaye Yupo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, ni Mtunza Vielelezo Katika ghala la Kutunzia Silaha

Wakili wa Serikali: Kabla ya kwenda Katika Shughuli Nyingine za Upelelezi, Ni wakati gani tena Ukiweza Kushughulika na Vielelezo hivyo

Shahidi: Nili shughulika tena wakati Wa Kutoa Mahakamani Kwa ajili ya Ushahidi, Ambapo Nilimkabidhi koplo Hafidh Kwa ajili ya Kuja Kutoa Ushahidi Mahakamani

Wakili wa Serikali: Turudi tena Katika Upelelezi Baada ya Tarehe 27 November 2020, kitu gani kiliendelea Wakati wa Kesi hiyo

Shahidi: Niliweza Kupokea Taarifa Kutoka kwa Mrajisi wa Silaha Siku ya Tarehe 18 March 2021

Wakili wa Serikali: Hiyo Taarifa Ilikuwa inahusu nini

Shahidi: Ilikuwa inahusu Mmiliki Wa Silaha Yenye Sirial namba A5340 aina ya Luger

Wakili wa Serikali: Na Ripoti hiyo ilisemaje

Shahidi: Report hiyo ilionyesha Kuwa Silaha hiyo, haina Usajili wowote Katika Ofisi Ya Mrajisi Wa Silaha Hapa Nchini

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kiliendelea baada ya hiyo Tarehe 18 March 2021

Shahidi: Tarehe 30 March 2021 Niliweza Kupokea Taarifa Ya Maabara ya Sayansi, Kutoka Kitengo Cha Uchunguzi Wa Maandishi, Kutoka Kwa koplo Khamis, Wa Kutengo cha Uchunguzi Wa Maandishi. Niliweza Kusoma Ripoti hiyo, Ambapo Ripoti hiyo ilionyesha Kuwa Sampuli Za Maandishi yaliyo chukuliwa Kutoka Kwa Mtuhumiwa Khalfani Bwire Hassan, Ni sawa Sawa na Maandishi Yaliyokuwepo Katika Daftari nililoambatanisha katika Uchunguzi ule

Wakili Wa Serikali: Baada ya Kuwa Umesoma, Ukafanya nini

Shahidi: Niliweza Kuhifadhi katika Jalada langu la Kesi na Kufungia Katika Kabati langu la Chuma

Wakili wa Serikali: Baada ya Tarehe hiyo Kitu gani Kingine Ulifanya Kuhusu Kesi hiyo

Shahidi: Mnamo Tarehe 10 July 2021 Niliweza Kupokea Taarifa ya Simu zile Nane Kutoka Kwenye Maabara ya kisayansi Kitengo Cha Uchunguzi Wa Makosa ya Mtandao

Wakili wa Serikali: Ulipokea Kutoka Kwa nani

Shahidi: Nilipokea Kutoka Kwa Inspector Ndowo wa Kitengo Cha Uchunguzi Wa Makosa ya Ki Mtandao Wa Maabara Ya Kisayansi

Wakili wa Serikali: Baada ya Uchunguzi Wa Taarifa hiyo nini Kilitokea

Shahidi: Alijulishwa DC Goodluck ambaye haikuwepo Dar es Salaam, alinijulisha Kwa Uchunguzi umekamilika, Ndipo nilipoenda Kuchukua Taarifa hiyo

Wakili wa Serikali: Ulimkabidhiwa Kwa Utaratibu Upi

Shahidi: Kwa Kusaini Katika Kitabu cha Kitengo Cha Uchunguzi Wa Makosa ya Mtandao

Wakili wa Serikali: Mwanzono Ulisema Kwamba Ulipeleka simu, Sasa unakabidhiwa Riport, Vipi Kuhusu Zile simu

Shahidi: Pia Nilikabidhiwa Simu Nane ambazo niliziandikia Barua

Wakili wa Serikali: Ulijuaje Kama ndiyo Simu ulizopeleka

Shahidi: Niliweza Kuzikagua Wakati na kabidhiwa Wakili wa Serikali Ulifanyia nini hiyo Riport baada ya Kukabidhiwa

Shahidi: Simu Nane nilipeleka Katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Nilimkabidhi Coplo Charles ambaye ni Mtunza Vielelezo Katika Chumba Cha Kuhifadhia Vielelezo Katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Na Ile Ripoti Ulifanyia nini

Shahidi: Ripoti Ya Uchunguzi Niliweza Kusoma. Na Kuhifadhi katika Jalada la Kesi Kisha Kuweka Katika Kabati langu la Chuma

Wakili wa Serikali: Ripoti hiyo Kwa sababu wewe Ndiye Uliyeomba Uchunguzi, Ni Vitu gani Ukiweza Kupata Kutoka Katika Ripoti hiyo

Shahidi: Katika Report hiyo Niliweza Kugundua Vitu vifuatavyo, Niliweza Kugundua Kuwa palikuwa na Mawasiliano kati ya Shahidi Luteni Denis Urio na Mtuhumiwa Freeman Mbowe ambayo Yalifanyika Katika Mtandao Wa Telegram Pia Kupitia Maelezo Ya Shahidi Luten Denis Urio, aliweza Kusema Kuwa alitumiwa pesa Kutoka Kwa Mtuhumiwa Freeman Mbowe

Ambapo Tarehe 20 July 2020 Namba 0719933386 ambayo ni Ya Mtuhumiwa Freeman Mbowe ilituma Kiasi cha TSh 500,000 Kwenda Kwa namba ya shahidi Luteni Denis Leo Urio ambayo ni 0787 555200.

Pia Tarehe 22 Mwezi huo huo wa July 2020 ilionyesha Kuwa Shahidi Luten Denis Urio Kupitia namba yake ya 0787 555200 ulipokea Kiasi cha TSh 199,000 kutoka Kwenye namba ya Wakala Kama alivyo eleza Luten Denis Urio.

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini Kiliendelea

Shahidi: Tuliendelea Kuandika Taarifa Mbalimbali na Kupitia Ripoti hiyo Niliweza Kujiridhisha kuwa ni kweli Mtuhumiwa Freeman Mbowe aliweza Kutuma hizo Fedha Kwa Luten Denis Urio

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea baada ya hapo

Shahidi: Siku ya Tarehe 27 July 2021 Watuhumiwa Justin Kaaya, Khalid na Gabriel Muhina Walifutiwa Shitaka Lao baada ya Kugundulika hawahusiki na chochote

Wakili wa Serikali: Turudi Baada ya Kupokea Ripoti Ya Uchunguzi Wa Kisayansi Kuhusu Simu, Baada ya Hapo Ulifanya nini

Shahidi: Mnamo Tarehe 18 July 2021 Niliandika Taarifa Kwenda Kwa Afande Mkurugenzi Wa Upelelezi wa Makosa Ya Jinai Nchini, Kuwa Kuna Ushahidi Wa Uhusika wa Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe, nakuwezesha Kumkamata

Wakili wa Serikali: Mwanzoni Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulizungumzia Kuhusu Kufungua Majalada Mawili, Je ni Jalada lipi ambalo wewe Uliandikia Taarifa

Shahidi: Ni lile Jalada la Kesi tulilo fungulia Polisi, ambalo ni CD/IR /2097 /2020 lenye Chama za Kutaka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali: Wakati Wa Kufungua Jalada la Kesi hili CD /IR /2097 /2020 Ulisema Kwamba Usiandike Jina la Freeman Mbowe Kwa sababu Kama Ungeandika Jina Taarifa zingeweza Kuvunja, na akasitisha Mpango Wake, Je Ulikuwa Unamaanisha Nini

Shahidi: Nilikuwa namaanisha kuwa angeweza Kusitisha Kumtumia Mtoa Taarifa, angeweza Kutumia Watu wengine ambapo Jeshi la Polisi lisingejua Mahali wala Muda, Kitu ambacho. Lingesababisha Jeshi la Polisi Kushindwa Kuzuia Uhalifu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuandika Taarifa Kwenda Kwa DCI Nini Kiliendelea

Shahidi: Nilipokea Taarifa Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi alinitaka nitunze Jalada hilo na Kwamba Yeye anafanya Jitihada za Kumkamata Mshitakiwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Baada ya DCI Kukwambia Hatua ambazo angechukua nini Kilitokea sasa

Shahidi: Mnamo Tarehe 22 July 2021 Nilipokea Karatasi Ya Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe Kutoka Kwa Afande Jumanne Malangahe Mrakibu Wa Polisi, Kimsingi Nilipokea Maelezo hayo Ikionyesha Mtuhumiwa amekataa Kutoa Maelezo Yake Polisi

Wakili wa Serikali: Kwa Kipindi hicho Ulifahamu huyo Mtuhumiwa Freeman Mbowe amepatikanaje

Shahidi: Nilifahamu Kwamba amekamatwa Mwanza na Kusafirishwa Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Umekuwa Ukizungumza Majina Ya Watu Kadhaa Hapa Mahakamani akiwepo, Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe. Hebu ieleze Mahakama Kama Watu hao wapo hapa Mahakamani

Shahidi: Ndiyo Watu hawa wapo hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Hebu onyesha sasa

Shahidi: Mtuhumiwa Wa Kwanza, Kutoka Upande Wa Kulia ni Khalfani Bwire Hassan, Wapili kutoka Kulia Kwangu ni Adam Hassan Kasekwa, Watatu Kutoka Kulia Kwangu ni Mohammed Abdilah Ling'wenya na Wanne Kutoka Kulia Kwangu ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Sasa Mwanzoni Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulizungumzia Kuhusu Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Walifikishwa Mahakamani Tarehe 19 August 2020, Mtuhumiwa Freeman Mbowe alifikishwa Mahakamani Tarehe ipi

Shahidi: Mtuhumiwa Freeman Mbowe alifikishwa Mahakamani Tarehe 26 July 2021

Wakili wa Serikali: Ni tofauti gani ipo Kutokana na Kufikishwa Tarehe tofauti na Wale 3

Shahidi: Utofauti unakuja Kutokana na Kusubiri Kwa Taarifa Ya Uchunguzi Wa Makosa ya Mtandao, ambao Kimsingi Nilipokea Tarehe 10 July 2021

Wakili wa Serikali: Sasa na Upelelezi Wa Kesi inayo wakabili, Ni Ushahidi gani ulipata Kwamba Walikula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi

Shahidi: Ni Kupitia Maelezo Yao ya Onyo ya Mshtakiwa Wa Pili Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya pamoja na Mshitakiwa Wa kwanza Khalfani Bwire Hassan, Pia Ushahidi Mwingine ambao Unaonyesha walikuwa Njama ni Kupitia Maelezo Ya Shahidi Luten Denis Urio,

Shahidi: Maelezo Ya Askari Walio wa kamata, Askari Walio andika Maelezo Ya Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Kuhusiana na Pesa iloyotumwa, Uliiweza Kubaini nini?

Shahidi: Niliweza Kubaini Fedha hiyo ilitumwa kutoka Kwa Freeman Mbowe Kwenda Kwa Luten Denis Urio, Ambapo Fedha hiyo iliweza Kuwawezesha Watuhumiwa Mshitakiwa Wa Pili na watatu pamoja na Mwingine ambaye hajakamatwa Kuweza Kufika Eneo la Uhalifu ambalo lilikuwa Eneo la Moshi Niliweza Kubaini Kuwa Fedha hiyo ilitumwa iliwezesha Watuhumiwa Kufika Eneo la Utekelezaji Wa Uhalifu

Wakili wa Serikali: Unaposema Kwamba Mshitakiwa Wa Pili, Watatu na Mwingine hajakamatwa, Vipi Mtuhumiwa Wa Kwanza Kuhusiana na Fedha hii

Shahidi: Kuhusu Mshtakiwa Wa kwanza Inaonyesha Pia aliweza Kupokea Pesa kutoka kwa Luten Denis Urio Kwa ajili ya Utekelezaji Wa Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Naomba Kukomea hapo Kwenye Examination inchief

Upande wa Utetezi

Wakili Nashon Nkungu: Shahidi Habari za Leo

Shahidi: Njema

Nashon: Shahidi umepona?

Shahidi: Bado

Nashon: Umemeza Dawa zako

Shahidi: Ndiyo

Nashon: nadhani Shahidi unatambua Ukubwa wa hii Kesi

Shahidi: Sahihi

Nashon: Kwamba Ugaidi ni Jambo Serious kwa Nchi na Dunia

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kutokana na Userious wa Mashitaka, Hata Uchunguzi Wako Ulitakiwa Uwe serious Ku Match na Makosa haya

Shahidi: Sahihi

Nashon: Kupitia Ushahidi Wako uliotoa, Unaweza Kusimama Kifua mbele Kwamba ulitendea Haki Uchunguzi Wa Kesi hii

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Makosa ni Vitu Vinavyotengenezwa na Sheria

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kuna Sheria ambazo zilikuwa zinawaongoza

Shahidi: Ni sahihi

Shahidi: Tutajie Sheria zipi Mlikuwa Mnazitumia Kuwa Guide

Shahidi: Sheria Mbalimbali

Nashon: Nitajie Sheria Mbili Mlikuwa Mnazitumia

Shahidi: Sheria ya Kuzuia Ugaidi na Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai

Nashon: Ni nani aliye angalia Sheria akatoa conclusion Kwamba alisema Kwa Story hii, haya ni Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Ni Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi

Nashon: Wewe huku take part katika Kujua haya ni Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Hata Mimi Mwenyewe pia nilikuwa najua haya Makosa ni ya Ugaidi

Nashon: Una utaalam wa Kung'amua Kuwa haya ni Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Ulisomea wapi

Shahidi: INTERNATIONAL LAW ENFORCEMENT ACADEMY Botswana

Nashon: Kozi gani

Shahidi: FIRST BURST SCENE

Nashon: Kwa hiyo Walimu Wako wakakwambia Kwamba Kozi hiyo ina husika na Ugaidi

Shahidi: Inahusika na Milipuko

Nashon: Shahidi Ulisema Kwamba Mmoja ya Watuhumiwa Katika kesi hii ni Justin Kaaya

Shahidi: Sahihi

Nashon: Uliwahi Kumuandika Kaaya Maelezo Ya Onyo

Shahidi: Hapana

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kaaya alitumiwa pesa na Freeman Mbowe

Shahidi: Ni Kweli

Nashon: Uliwahi Kumuandika Kaaya Maelezo Ya Ushahidi

Shahidi: Sahihi

Nashon: Alikwambia Kwamba aliwahi kutumiwa pesa na Freeman Mbowe

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba alitumiwa pesa kama Watuhumiwa Wengine hapa Mbele

Shahidi: Hapana

Nashon: Justine Kaaya, Khalfani Bwire wote Walitumiwa pesa na Freeman Mbowe

Shahidi: Sahihi

Nashon: Wote hawa Wametumiwa pesa na Freeman Mbowe

Shahidi: Sahihi, lakini Malengo ni tofauti

Nashon: Malengo ya pesa ya Khalfani Bwire unayatoa Wapi

Shahidi: Maelezo ya Mtuhumiwa

Nashon: Maelezo ambayo Washtakiwa Wanataka kwamba hawakuyatoa Kwa hiari yao, Bali kwa Mateso ndiyo Ushahidi Wako wa Pekee?

Shahidi: Maelezo ya Washtakiwa Wengine

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kaaya alisema alikuwa anapewa pesa na Freeman Mbowe Kwa ajili ya Kutoa Taarifa Za Sabaya

Shahidi: Lakini alikuwa hafahamu Malengo

Nashon: Je tangu ugundue hakuwa na Nia Mbaya ilikuwa ni Muda gani baada ya Kumkamata

Shahidi: Zaidi ya Miezi 10

Nashon: Ulimkamata lini

Shahidi: Mwezi September 2020

Nashon: Ukaja Kumuachia lini

Shahidi: Mwezi July 2021

Nashon: Baada ya Mwaka mmoja ndiyo Ukajua hakuwa na Melengo Mabaya

Shahidi: Sahihi

Nashon: Ni sahihi Taarifa za Sabaya Freeman Mbowe alizitoa Kwa Kaaya

Shahidi: sahihi

Nashon: Kwamba alilipwa kwa kazi hiyo

Shahidi: sahihi

Nashon: wewe Hukuona Kosa

Shahidi: sahihi

Nashon: Na Kwamba alikuwa anakaa Kikao na Mbowe Kutoa Taarifa hiyo

Shahidi: Sahihi

Nashon: Kwa Kushiriki Kikao hicho Kaaya alikuwa anashiriki Kikao cha Kigaidi

Shahidi: Alikuwa ajui Dhumuni La Kikao, Kwa hiyo ajashiriki Kikao cha Kigaidi

Nashon: Lakini katika Kikao hicho hicho Mbowe alishiriki Kikao cha Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Mahakama: KICHEKO

Nashon: wakati gani ulipokea Bastola

Shahidi: Baada ya Kutoka Maabara

Nashon: Uli label?

Shahidi: Siku Label

Nashon: Lakini Simu za Mshtakiwa Wa kwanza ndiyo Uli Label

Shahidi: Hapana Siku Label

Nashon: Wewe Uli Label Simu za nani

Shahidi: Luten Denis Urio

Nashon: Na uli Label lini

Shahidi: Tarehe 11 na 13 August 2020

Nashon: Je ni sahihi Kwamba Ulichukua Bastola ya A5340 pamoja na Risasi kutoka Kwa Coplo Hafidh

Shahidi: Nilipokea Silaha A5340 aina ya Luger kutoka Kwa Hafidh Ikiwa na Risasi Moja, Maganda Mawili

Nashon: Ulipokea Vielelezo Kutoka kwa koplo Hafidh

Shahidi: Sahihi

Nashon: Naomba Upokeee Simu, Mheshimiwa Jaji ni Kutoka Katika Kielelezo P28

Nashon: hii aina au dizaini la Ku Label unaitolea wapi

Shahidi: Kipo Kwenye Sheria

Nashon: Sheria ambayo unaitumia ni Sheria gani

Shahidi: Ni PGO

Nashon: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama ulijaza Makabidhiano wakati wa Makabidhiano

Shahidi: Humu sijaandika

Nashon: Unafahamu Kwamba Katika Kielelezo, Lebel ya Kielelezo pale Unapo ambatanisha namba ambayo unaambatanisha inatakiwa uwe namba ya Jalada la Kesi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Unafahamu Kwamba Unatakiwa pia uwe na Exhibit Serial number

Shahidi: Siyo lazima, Kwa sababu hivi Vielelezo Vilikuwa kwenye Mfuko kwa hiyo Exhibit Serial number inakuwa kwenye Mfuko

Nashon: Hiyo PGO Unayosema Ulitumia inataka uwe na Mahala, namba na Tarehe mnayokabidhiana

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Lakini hapa Hakuna hata Moja

Shahidi: Ndiyo hapo Hakuna

Shahidi: SAMAHANI MHESHIMIWA JAJI NAOMBA NIENDE WASHROOM (CHOONI)....

Shahidi karejea

Nashon: Nipo interested na Shahidi ambaye alikuwa Mtuhumiwa akaachiwa

Nashon: Je ni sahihi Katika Maelezo Uliyo Mwandika Wewe, aliandika Kuwa aliwahi Kuwa Msaidizi Wa Katibu wa CCM Wilaya ya Meru

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Pamoja na Kwamba kapokea Fedha, na Kashiriki Vikao ila akaachiwa

Shahidi: Sahihi

Nashon: nani ni Mwamuzi ambaye aliamua kuwa Pesa hizo siyo za Ugaidi

Shahidi: ni Upelelezi

Nashon: Ni nani hasa

Shahidi: Mchakato Wa Upelelezi

Nashon: Ni sahihi Kwamba Uliwahi kuandila Maelezo Yako Mwezi 6 August 2020

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kuwa katika Maelezo yako Uliwahi Kusema Kuwa Mbowe ameshiriki Vikao Vya Kigaidi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Na Katika Maelezo yako Ulisema Kwa, Kuthibitisha hilo ni Kupitia Maelezo ya Onyo ya Washtakiwa Wenzie

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba wewe na Wapelelezi Wenzio hamkuwahi Kushuhudia Mbowe akiwa katika Kikao cha Ugaidi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba Wewe na Wapelelezi Wenzio hamkuwahi Kushuhudia Mbowe akiwa katika Kikao Mbeya au Arusha?

Shahidi: Sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba pia nyie Kama Wapelelezi wa Kesi hii hamna CCTV Camera

Shahidi: Ni sahihi hatuna

Nashon: Ni sahihi Kwamba wewe na Wapelelezi Wenzio hamna hata Sauti ya Mbowe akipanga Ugaidi

Shahidi: Ni sahihi hatuna

Nashon: Ni sahihi Kwamba Jeshi la Polisi lina Vifaa Vya Kurekodi Sauti

Shahidi: Siwezi Kuzungumzia hilo

Nashon: Lakini Unafahamu Kwamba Simu inaweza Kurekodi Sauti

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Na Jeshi la Polisi hamkazwi kutumia Simu Kurekodi Sauti

Shahidi: Ndiyo

Nashon: unajua Kuwa Mahakama Inaruhusu Kutumia Video na Sauti katika Ushahidi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Nikumbushe Cheo Chako huko Polisi

Shahidi: Inspector Wa Polisi

Nashon: Na Inspector Wa Polisi Ujui Kuwa Mahakama Inatumika Video na Sauti Katika Ushahidi

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Ndiyo Maana hamkuleta Video wala Sauti Mahakamani Kwa sababu ufahamu Ka Inatumika Mahakamani Kama Ushahidi

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Nionyeshe Sasa sehemu ambayo Mahakama itaona Mbowe alikaa Vikao Vya kigaidi

Shahidi: Ilikuwa Kwenye Gari, Ukisoma Maelezo Utaona

Nashon: Naomba Sasa Mahakama Ikupatie hizo Meseji Shahidi: Nimeona Meseji ya Tarehe 22 July 2020 Muda wa Saa 7 na Dakika 49 "Kutakuwa na Safari ya kwenda Hai, Leo Usiku au Asubuhi" Mahakama

Nashon: Naomba Sasa Mahakama Ikupatie hizo Meseji

Shahidi: Nimeona Meseji ya Tarehe 22 July 2020 Muda wa Saa 7 na Dakika 49 "Kutakuwa na Safari ya kwenda Hai, Leo Usiku au Asubuhi"

Mahakama: Kicheko

Shahidi:
hii Inaelezea Sasa Kwamba Kutakuwa Kuna Kikao

Nashon: Katika hiyo Meseji wataje Wanaokutana

Shahidi: Mtuhumiwa Wa Kwanza, Wa pili, Watatu na Wanne

Nashon: Kwa hiyo akisoma hiyo Meseji ataona Kwamba Kuna Kikao cha Ugaidi

Shahidi: Ushahidi ni Kuunganisha Dot

Nashon: Kwa hiyo Nikisoma Meseji ipi nitaona nani na nani wametajwa, Saa ngapi na Wapi

Shahidi: Kwenye Meseji Hauwezi Kuona, ila Kwa Kuunganisha Dot

Mahakama: Kicheko

Nashon: Tutoke hapo umesha Sema hatutoona. Meseji Twende Kwingine

Nashon: Ni kweli Kwamba Mlikuwa na Msiri wenu Denis Urio

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Baada ya Kuona hiyo Meseji Kwamba wanaenda Hai, nyie Hamku fuatilia

Shahidi: Hatukufutilia

Nashon: Mnafahamu Kuwa Aishi Hotel Ina CCTV Camera

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Na hufahamu kwa sababu hujawahi Kufika Aishi Hotel

Shahidi: Kimya

Nashon: Sasa Ulifanya Juhudi zozote za Kwenda Pale Aishi Hotel kama Mpelelezi ambaye Yupo serious, labda Kuandaa Warranty, CCTV CAMERA Kuangalia List ya Wageni

Shahidi: Sikuwahi Kufanya hivyo

Nashon: Kwa ujasiri kabisa Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Uliwezaje Kuwaleta Watuhumiwa Mahakamani Kwamba Wamekutana sehemu fulani ambayo wewe na Polisi Wengine hamjawahi Kufika

Shahidi: Mimi nilikuwa sehemu ya Upelelezi tu, Kuna wengine ambao walikuwa Arusha na Kilimanjaro

Nashon: Kwa hiyo Wewe Kwa sababu upo Dar es Salaam hukuona Sababu

Shahidi: Hapakuwa na Ulazima

Nashon: Sasa Pale Aishi Walifanya Nje au Ndani

Shahidi: Nje Kwenye Garden

Nashon: Garden ya upande upi

Shahidi: Sifahamu Sijawahi Kufika

Nashon: Katika Ushahidi Wako Nimekusikia Mahala Kwamba Unasema Ulikuwa unapokea Vielelezo na Kuvitunza, Je Hapa Mahakamani umewahi Kusema Kuwa Uliwahi Kuwa Forensic Beaural

Shahidi: Sijawahi Kusema

Nashon: Wewe Ulikaa na Vielelezo Vipi ambavyo Uliviandaa Kwa ajili ya Ushahidi

Shahidi: Simu za Urio Nashon Simu za Urio tu?

Shahidi: Simu zote Nane

Nashon: za Kwanza

Shahidi: Nilipokea Tarehe 07 August 2020 Mpaka Tarehe 13 August 2020

Nashon: tukumbushe nani alivileta Mahakamani

Shahidi: Hivyo Vielelezo Nilimpa Inspector Ndowo

Nashon: Lini

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: Kwa sababu hamkuandikishana

Shahidi: Tuliandikishana

Nashon: Lakini Tukiangalia katika PF 145 Hatuoni sehemu Mliyo kabidhiana

Shahidi: Ni sahihi Hakuna

Nashon: Ulikuwa unafahamu kuwa Sheria inataka uonyeshe Katika PF 145

Shahidi: Nilikuwa nafahamu

Nashon: ila Ukaamua Kupuuza Sheria

Shahidi: Hapana

Nashon: Ni sahihi Uliondoka HQ August 2021

Shahidi: sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba hujaeleza Mahakama Baada ya Kuondoka Ofisini Kwako Vielelezo ulimuachia nani

Shahidi: Usipotoshe Mahakama, Nilisema Kwamba Vielelezo Vyote nilikuwa nimepeleka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Nashon: Unakumbuka Muda ambao Ulikaa na Vielelezo, Ambapo Vilienda Polisi Kati Dar es Salaam na kukaa navyo katika Kabati la Chuma

Shahidi: Kwa nani? Kwa Tarehe ipi?

Nashon: Je ni sahihi Kwamba Ulichukua Vielelezo Kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Yes or No Shahidi Yes

Nashon: Kwanini Sasa unapoteza Muda Wa Mahakama

Nashon: Baada ya Uchunguzi Ulikaa navyo au ulipitiliza Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Nilipeleka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Nashon: Kwa hiyo ni sahihi Kwamba Ulikuwa Umekaa na Vielelezo Katika Kabati lako wakati wewe siyo Mtunza Vielelezo

Shahidi: Nilikaa navyo Kwa ajili ya Kuviandikia Barua, Sababu ya Upelelezi

Nashon: Ilikuwa inashindikana Kwa wewe Kuandika Barua Vielelezo Vikiwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Ilikuwa Haiwezekani

Nashon: Unafahamu Kwamba OC Forensic Beaural ndiye anaye husika Katika Kuandaa na Kutunza Vielelezo Kabla ya Kwenda Kufanyiwa Uchunguzi

Shahidi: OC wa Forensic Beaural anapelekewa na Mpelelezi

Nashon: Je Unafahamu Kwamba OC Forensic Beaural ndiye anaye husika Katika Kutunza, Kuandaa na Kupeleka kwa Expert Examination

Jaji: sijui Mimi Ndiyo sielewi, Naomba Wakili unisaidie

Wakili Kihwelo: Swali lake linahusu Custodian wa Kutunza kabla ya kwenda Kwa Expert Examination

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Katika Ushahidi Wako Kuna sehemu Kwamba Ulisema DCI alikwambia pamoja na OC Forensic Beaural ndiyo Mtunza Kielelezo, lakini wewe Kaa navyo

Shahidi: Sikueleza hayo

Nashon: Kwakuwa Umeibuka Mjadala hapo, Na Kwakuwa Mheshimiwa Jaji Shahidi alisema anaifahamu PGO naomba ni Muonyeshe Shahidi PGO hii ambayo alikuwa anaitumia Wakati wa Kufanya Kazi, PGO ya 8 Paragraph ya 9

Jaji: Rudia na uongeze Sauti

Nashon: Soma Kipengele (e)

Jaji: Samahani, Hapa OC anahusika baada ya OC kuwa ameletewa Vielelezo Hapa Sheria inasema Kwamba OC Forensic Beaural, Ndani ya Forensic baada ya Kuvipokea Nataka sasa Kufahamu Premise ya swali lako naandikaje, Inawezekana Unahoja ila namna ya ulivyoliweka ndiyo Unanichanganya

Nashon: labda Kwako Mheshimiwa Jaji, lakini najua siyo sawasawa.

Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji Kwa Kuokoa Muda, wakili aende Kwenye eneo lingine baadae ndiyo arudi kuunganisha hapo

Jaji: Sawa

Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji hata sisi tunapata tabu sababu Shahidi Alisha Sema siyo Utaratibu, nilifikiri Kuanzia pale ndiyo tuelezwe Jaji Ndiyo Maana wanasema Watarudi Baadae

Nashon: Shahidi Ni sahihi Kwamba Wewe ndiyo ulimuandika Maelezo Luten Denis Urio

Shahidi: Sahihi

Nashon: Je Hukuona Kosa pale Ambapo Luteni Denis Urio aliposema Kwamba "Mlimkubalia kwa kwenda Kutafuta Watu wa Kufanya Vitendo Vya Kigaidi" alikuwa anatenda Kosa

Nashon: Shahidi Soma yote ndiyo Utaona siyo Kosa

Wakili Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji naomba hapa Kuweka Sawa, Shahidi anaitwa kwa Sheria tofauti na Kifungu tofauti, Sasa anapoelekea Wakili akatazwe, shahidi awezi Kuwa mtuhumiwa

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji kumsitiri Kaka Yangu Abdallah Chavula PGO 236 Paragraph 08 ambapo inasema During police officers during taking statement.................

Wakili Wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Nafikiri aendelee

Nashon: Kwa Ufahamu Wako Kumtafutia Mhalifu Wahalifu Wa Kwenda Kutimiza Uhalifu Siyo Kosa

Shahidi: Inategemea

Nashon: Huyu Luteni Denis Urio alikuwa ni Askari Polisi

Shahidi: Hakuwa Askari Polisi

Nashon: Je huyu Luteni Denis Urio Mlimpa Ulinzi Wa Kisheria

Shahidi: Siyo Mimi niliye pokea Taarifa zake, Mara ya Kwanza alitoa Taarifa Kwa DCI

Nashon: Kwani huyu Luteni Denis Urio alikuwa na Taaluma ya Upelelezi

Shahidi: Siyo Mimi niliye pokea Taarifa

Nashon: Kwani Luten Denis Urio Mlimfundisha Kuhusu Kufanyia Watu Upelelezi

Shahidi: Mimi Sikuwahi Kumuona Luten Denis Urio kabla

Nashon: Umesikiliza Ushahidi Wa Luten Denis Urio

Shahidi: Wapi

Nashon: alipokuwa hapa Mahakamani

Shahidi: Sikuwepo Mahakamani

Nashon: Sawa, Ngoja ni kwambie sasa, Urio Mada aliwatafuta Watuhumiwa lakini hawakuwa wanajua Kuwa wanaenda Kufanya Ugaidi

Nashon: Je Muda gani sasa Khalfani Bwire alipata Guilty Mind

Shahidi: anafahamu Mwenyewe

Nashon: Je ni muda gani Adam Kasekwa alipata Guilty Mind

Shahidi: anajua yeye Mwenyewe

Nashon: Je ni Muda gani Mohammed Ling'wenya alipata Guilty Mind

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Katika Ushahidi Wako Ulisema Uliitwa Tarehe 14 July 2020 kwa Mkurugenzi, Je ni sahihi

Shahidi: Siyo Sahihi

Nashon: Wacha nisome... Wakili anasoma

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwa hiyo Tarehe 14 July 2020 Taarifa zimekuja tayari Kuna Kundi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Unafahamu Kwamba Pesa zimeanza kutumwa Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Je hilo Kundi lililkuwepo Kabla halijakutana Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Lilikuwepo Kabla

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kundi Lilianza kutengenezwa na Luteni Denis Urio Tarehe 20

Shahidi: Kundi Lilikwepo Mara baada ya Luteni Denis Urio Kukutana NA Freeman Mbowe

Nashon: Kwani hilo Kundi ni hili au Kundi lingine

Shahidi: Ni hili

Nashon: Kwa hiyo Wewe na Luteni Denis Urio Mahakama iangalie nani anasema Kweli

Shahidi: Mahakama ndiyo itajua

Nashon: Shahidi Ni sahihi Ulisema Kwamba Hamkuandikisha Jina la Freeman Mbowe Kwa sababu Taarifa zingevuja

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwa hiyo Kuna Askari siyo Waaminifu

Shahidi: Tulihofia Kwamba Kile Kitabu kinasomwa na kubadilishana Taarifa Kwa Polisi

Nashon: Kwani wewe Unafahamu sheria yoyote inayoruhusu Kufungua Kwa Jalada bila Kujaza Jina

Shahidi: Hakuna

Nashon: Lakini Unafahamu Sheria ambayo Inaelekeza Majina yajazwe

Shahidi: Nafahamu

Nashon: Shahidi Wakati Unaenda Kule Coco beach, Kumtafuta Khalfani Bwire, Hukuona haja ya Kuwa chukua Watuhumiwa Wenzake Kwenda pamoja Kumtafuta Khalfani Bwire Kwa sababu wangemtambua hata Kama kawapa Mgongo

Shahidi: Hapakuwa na haja hiyo

Nashon: Shahidi, Ulisema Kuna Kidaftari

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ulisema Kile Kidaftari Kina Michoro Ya Ramani

Shahidi: Sahihi

Nashon: Kwani wewe Unataaluma Ya Ramani

Shahidi: Hapana, ila naweza Kusoma Ramani

Nashon: Kwani Nikochora Duara Utajua ni Kisima

Shahidi: Hapana

Shahidi: waliandika Majina ya Barabara, na Mishale ya Kuingia na Kutoka

Nashon: Kwani Walitaja Mikoa

Shahidi: Hapana

Nashon: GBP na Bigbon

Shahidi: sahihi

Nashon: Kilicho Kufanya Ujue ni Kariakoo na Morocco uliyokwenda ni ipi

Shahidi: Sababu palikuwa na Majina ya Barabara
Hivi Mh. wakili Nashon wakati anasoma HGL A- level na Geography O- level hakufundishwa map reading- ALIPATAJE UWAKILI HUYU?!
 
Nani anaweza kuandaa Rasimu ya Kitabu kuhusu maisha ya Freeman Aikael Mbowe.

Kitabu kichapwe mwaka 2030 kwa ajiri ya vizazi vijavyo katika vita ya kupigania demokrasia na haki za binadamu Tanzania.

Tittle : The life and times of Freeman Aikael Mbowe. A true son of the soil.

FAM ni tunu kwa wapenda haki wote,tumuweke FAB katika maandishi kwa faida ya vizazi vijavyo. Nipo tayari kutoa fedha na nyenzo kumuweka FAB katika maandishi.

Sina chama chochote lakini napenda ujenzi wa demokrasia na haki za binadamu.
Mbowe siyo son of the soil- Mbowe ni Mnyasa wa Malawi
 
Yaani huyu kakarishwa tu kusema sio sahihi,hata akiulizwa ulienda msalani muda mfupi uliopita atasema sio sahihi[emoji3][emoji3]
Nashon: Katika Ushahidi Wako Ulisema Uliitwa Tarehe 14 July 2020 kwa Mkurugenzi, Je ni sahihi

Shahidi: Siyo Sahihi

Nashon: Wacha nisome... Wakili anasoma

Shahidi: Ni sahihi
Anasema siyo sahihi.akisomewa kielelezo/ushahidi anasema ni sahihi. Wenye picha yake atuwekee huyu utopolo
 
Leo lazima ifanyike cross examination so Afande swila kwa kuonesha ushirikiano angevaa kabisa pempasi

Hizi habari za kwenda chooni mara kumi kumi ni kupotezeana muda tu na kufanya kesi ionekane ndefu
maswali ya wakili msomi yamemvuga tumbo
 
Back
Top Bottom