Yaliyojiri Mikutano ya CCM: Maridhiano ya kitaifa, Mchakato wa Katiba Mpya, Uteuzi, Pongezi kwa Rais Samia na Mwinyi

Yaliyojiri Mikutano ya CCM: Maridhiano ya kitaifa, Mchakato wa Katiba Mpya, Uteuzi, Pongezi kwa Rais Samia na Mwinyi

Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumatano 22 Juni 2022 Makao Makuu ya CCM katika Ukumbi wa White House Jijini Dodoma kimetoka na maazimio yafuatayo kwa masilahi ya taifa.

1. Maridhiano ya kifaifa.
2. Kufufuliwa kwa mchakato wa Katiba kwa kuzingatia mazingira ya bora ya sasa.
"Chama cha Mapinduzi tunasisitiza umuhimu wa uwepo wa Katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa masilahi mapana ya taifa na maendeleo kwa ujumla." ameeleza Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ya Taifa - Itikadi na Uenezi wakati akizungumza na wanahabari.

3. Ndg. Steven Wassira ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
...............................................................................
TAARIFA KWA UMMA

YALIYOJIRI KATIKA VIKAO VYA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekutana leo tarehe 21/06/2022 Ikulu Chamwino, Dodoma kwa kikao cha siku moja cha kawaida na kuongozwa na Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UTEUZI WA WENYEVITI WA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MAMEYA

Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya uteuzi wa wenyeviti wa halmashauri za wilaya na Mameya kama ifuatavyo:-

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mji
  • Ndg Erasto B. Mpete
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • Ndg Mohamed Festo Bayo
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
1. Ndg Stuart Nathaniel Nkinda
2. Ndg Apaikunda Ayo Naburi
3. Ndg Zuberi Abdallah Kidumo

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kimefanyika leo tarehe 22 Juni, 2022 katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya Chama Jijini Dodoma chini ya Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MARIDHIANO NA PONGEZI KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa ukomavu, ustahimilivu, uhodari na dhamira yake njema ya kufanya maridhiano na vyama vya siasa nchini kwa lengo la kuimarisha umoja, ushirikiano, mshikamano, amani na utulivu kwa maendeleo na ustawi wa watanzania wote.

Halmashauri kuu ya Taifa imevipongeza vyama vyote vya siasa kwa kukubali kuunga mkono hatua hiyo. Chama kimeishauri serikali kuharakisha utekelezaji wa masuala yote yatakayojenga kuaminiana, kuimarisha ushirikiano na umoja wa kitaifa kwa ustawi wa wananchi wote. Miongoni mwa mambo ambayo Halmashauri Kuu imeshauri kutazamwa ni pamoja na kesi zenye sura ya kisiasa kwa wafuasi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.

Chama kimeishauri serikali utekelezaji wa masuala yote ya kuimarisha demokrasia nchini na mazingira ya kisiasa yafanyike bila kuathiri uhuru na usalama wa nchi yetu.

PONGEZI KWA DKT HUSEIN MWINYI

Vilevile Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Husein Ali Mwinyi kwa kuendelea kuonesha uvumilivu na ukomavu wa kiuongozi katika kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa hali inayochochea umoja, amani na utulivu kwa wananchi wa Zanzibar na hivyo kuharakisha maendeleo yao.

UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kauli moja imekubaliana kuwa kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakubaliana na umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na hivyo kinaishauri serikali kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya kwa maslahi mapana ya Taifa na Maendeleo ya watanzania wote.

UCHAGUZI MKUU WA NDANI YA CHAMA

Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea na kuridhishwa taarifa ya maendeleo ya uchaguzi mkuu wa ndani ya Chama ambao umeshakamilika kwa asilimia 99.5 katika ngazi ya mashina na matawi kote nchini na sasa upo katika ngazi ya Kata/Wadi. Chama kimetakiwa kuzifanyia kazi kasoro zilizojitokeza katika ngazi hizi ili kuimarisha ushiriki wa haki, usawa na demokrasia katika ngazi zote zinazofuata kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi ya Chama.

UCHAGUZI WA KUJAZA NAFASI ZA WAJUMBE WAWILI WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya uchaguzi wa kujaza nafasi mbili za wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa zilizokuwa wazi kwa kuwachagua kwa kura Ndugu Stephen Masatu Wassira na Ndugu Theresia Adriano Mtewele.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Itikadi na Uenezi.
22 Juni, 2022.

Habari za CCM hazina mvuto, labda kama zitavutia vyombo vya dola.
 
Kama Mtanzania Mzalendo, naunga mkono azimio namba 1 na 2. Na itapendeza sana kama haya maazimio mawili yatatanguliza maslahi ya Taifa, badala ya maslahi ya watu wachache, au vyama vyao vya kisiasa.
 
Moja ya point muhimu ambazo CCM imechelewa kuzichukua ni point kuhusu ishu ya Katiba mpya. Suala la umuhimu wa katiba mpya ni la wazi mno na hii ajenda ilipaswa ibebwe na CCM toka mwanzo hasa ukizingatia kuwa Mama alikuwa ndio makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Hata hivyo hatua iliyofikiwa ni nzuri sana na ya kupongezwa.

Kimsingi sio kila hoja inayoshikiliwa na wapinzani ni mbaya, hoja nyingine ni nzuri tu, na ni muhimu CCM ikawa inazichukua na kuzifanyia kazi hoja za msingi kama inavyofanya awamu ya 6. Kwa kufanya hivyo, inaufilisi upinzani kihoja na wanajikuta hawana hoja yoyote ya msingi. Huko nyuma tuliwahi kuwa na kiongozi mwoga wa hoja, haifahamiki alikuwa anagopa nini maana vyama vya upinzani Tanzania ni wepesi sana.

Ukweli ni kwamba CCM bado ni chama chenye utajiri mkubwa wa rasilimali watu ya kutosha na yenye uwezo mkubwa sana ukilinganisha na vyama mbadala. CCM ina rasilimali vitu na ushawishi vile vile ukilinganisha na vyama mbadala. CCM bado inao uwezo wa kushinda chaguzi vizuri kabisa pamoja na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Changamoto iliyopo tu ni kwamba baadhi ya wana CCM wanakuwa hawana courage ya kutosha ya kutoa hoja zao na kuzitetea. Hali hiyo hufanya upinzani uonekane kama una hoja fulani hivi, japo kiuhalisia hoja zao ni nyepesi kama unyoya.

Trust me, upinzani wa Tanzania hauna stability yoyote. Hawana hoja za msingi isipokuwa chache tu kama Katiba mpya, Maridhiano na haki ambazo zimeshafanyiwa kazi na awamu ya Sita tena kwa ufanisi mkubwa sana.Uzuri ni kwamba mama hana woga kusimamia mambo ya msingi ambayo yana maslahi kwa Taifa.

CCM tuna uwezo mkuwa sana na nafasi nzuri ya kupambana kwa hoja na tukafanya vizuri sana. By the way sio lazima tuwe tunashinda kwa 99%k wenye chaguzi. Ushindi wa 70% tu unaopatikana kwa haki na kila mtu akiona haki ilivyotendeka inatosha sana. Raha ya mechi ushinde kwenye mchuano mkali na haki iliyo wazi kabisa na kila mtu aone unavyopiga mabao.

CCM tuna uwezo wa kushinda kwa hoja kwa sababu kuna vitu vingi vikubwa vinafanywa na Serikali ya CCM hasa katika kipindi hiki.CCM ina wasomi na rasilimali watu yenye uwezo mkubwa mno. No need to worry on anything.

Kwa sasa mtu anaweza kuitetea CCM kwa confidence kubwa sana na kwa hoja madhubuti kabisa.

Mungu Mbariki Kiongozi wetu umjaze hekima na busara zaidi. Naiona ile tuzo ya Utawala Bora Afrika ambayo imekuwa ikikosa mshindi sasa itakuja Tanzania. Mbele ni kuzuri na matumani kwa watanzania ni makubwa mno kwa sasa.
 
Uwepo wa Katiba mpya utaifanya Zanzibar isinjonywe na Tanganyika.
Maana wazenzi walio wengi hawaupendi huu Muungano ulivyo sasa.

Mama amefanya vizuri kuruhusu huu mchakato ili tufikie muafaka. Maana Marais wote wanaotokea Tanganyika hawakuwa wakiwasikiliza malalamiko ya wazenji.

Mama apewe tu Nishani ya heshima kwa uamuzi huu mzuri.
 
Zanzibar inanufaika zaidi na muungano kuliko hata sisi watu wa bara. Sema tu kuna watu wachache wanaopenda kulalamika, hao ndio wenye shida. Hata hivyo maridhiano ni kitu cha muhimu ili kusiwe na hisia za kwamba kuna mtu au upande hautendewi haki.
 
Moja ya point muhimu ambazo CCM imechelewa kuzichukua ni point kuhusu ishu ya Katiba mpya. Suala la umuhimu wa katiba mpya ni la wazi mno na hii ajenda ilipaswa ibebwe na CCM toka mwanzo hasa ukizingatia kuwa Mama alikuwa ndio makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Hata hivyo hatua iliyofikiwa ni nzuri sana na ya kupongezwa.

Kimsingi sio kila hoja inayoshikiliwa na wapinzani ni mbaya, hoja nyingine ni nzuri tu, na ni muhimu CCM ikawa inazichukua na kuzifanyia kazi hoja za msingi kama inavyofanya awamu ya 6. Kwa kufanya hivyo, inaufilisi upinzani kihoja na wanajikuta hawana hoja yoyote ya msingi. Huko nyuma tuliwahi kuwa na kiongozi mwoga wa hoja, haifahamiki alikuwa anagopa nini maana vyama vya upinzani Tanzania ni wepesi sana.

Ukweli ni kwamba CCM bado ni chama chenye utajiri mkubwa wa rasilimali watu ya kutosha na yenye uwezo mkubwa sana ukilinganisha na vyama mbadala. CCM ina rasilimali vitu na ushawishi vile vile ukilinganisha na vyama mbadala. CCM bado inao uwezo wa kushinda chaguzi vizuri kabisa pamoja na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Changamoto iliyopo tu ni kwamba baadhi ya wana CCM wanakuwa hawana courage ya kutosha ya kutoa hoja zao na kuzitetea. Hali hiyo hufanya upinzani uonekane kama una hoja fulani hivi, japo kiuhalisia hoja zao ni nyepesi kama unyoya.

Trust me, upinzani wa Tanzania hauna stability yoyote. Hawana hoja za msingi isipokuwa chache tu kama Katiba mpya, Maridhiano na haki ambazo zimeshafanyiwa kazi na awamu ya Sita tena kwa ufanisi mkubwa sana.Uzuri ni kwamba mama hana woga kusimamia mambo ya msingi ambayo yana maslahi kwa Taifa.

CCM tuna uwezo mkuwa sana na nafasi nzuri ya kupambana kwa hoja na tukafanya vizuri sana. By the way sio lazima tuwe tunashinda kwa 99%k wenye chaguzi. Ushindi wa 70% tu unaopatikana kwa haki na kila mtu akiona haki ilivyotendeka inatosha sana. Raha ya mechi ushinde kwenye mchuano mkali na haki iliyo wazi kabisa na kila mtu aone unavyopiga mabao.

CCM tuna uwezo wa kushinda kwa hoja kwa sababu kuna vitu vingi vikubwa vinafanywa na Serikali ya CCM hasa katika kipindi hiki.CCM ina wasomi na rasilimali watu yenye uwezo mkubwa mno. No need to worry on anything.

Kwa sasa mtu anaweza kuitetea CCM kwa confidence kubwa sana na kwa hoja madhubuti kabisa.

Mungu Mbariki Kiongozi wetu umjaze hekima na busara zaidi. Naiona ile tuzo ya Utawala Bora Afrika ambayo imekuwa ikikosa mshindi sasa itakuja Tanzania. Mbele ni kuzuri na matumani kwa watanzania ni makubwa mno kwa sasa.
Kuzaliwa Kwa KATIBA mpya kutatimiza Unabii wa KIFO Cha KINYONGA wa KIJANI na MANJANO.

Kifo Cha KINYONGA huyo kitasababisha KUZALIWA Kwa Chama kingine Kutoka ndani ya Kinyonga.

Na CHAMA hicho kipya kitakuwa ni Kwa maslah mapana ya nchi. Amen
 
Ninyi ni watu wa ajabu sana. Watu ambao msichopenda kufanyiwa ndicho mnachopenda kuwafanyia wenzenu. Mfano hamtaki kutukanwa ila mnatukana wenzenu, Hamtaki udikteta, ninyi wenyewe hamna uvumilivu kabisa na mtu mwenye mawazo tofauti na yenu.

Ndio maana tunasema upinzani wa Tanzania sio wakuaminika kabisa maana waliopo humo hawana moral standards, ni wapiga kelele tu.
 
Habari za CCM hazina mvuto, labda kama zitavutia vyombo vya dola.
Hivi mkuu unajua unachotafuta kwa maslahi ya taifa?
Inaonyesha pengine hujui unachotafuta , na hivyo utajikuta unapinga hadi mambo ya maana yenye maslahi ya taifa
 
Ni jukumu sasa wadau wote wajue kwamba awamu ya 6 ipo kwa ajili ya ustawi wa taifa katika mapana yake na yanapokuja mambo serious ni muhimu kutanguliza maslahi ya taifa mbele, vinginevyo tutakwama tena mahali halafu tutaanza kulaumiana kumbe tunajikwamisha wenyewe kwa sababu ya ushabiki wa kitoto tu.
 
..mchukue na hoja ya muungano wa serikali 3.

..kuondoa madaraka ya ki-mungu-mtu ya raisi.

..ugatuzi wa madaraka. Ama kuanzisha mfumo wa serikali za majimbo.

..kuanzishwa kwa tume huru ya uchaguzi.

..na kuundwa kwa Tume ya ukweli na maridhiano.
 
Ninyi ni watu wa ajabu sana. Watu ambao msichopenda kufanyiwa ndicho mnachopenda kuwafanyia wenzenu. Mfano hamtaki kutukanwa ila mnatukana wenzenu, Hamtaki udikteta, ninyi wenyewe hamna uvumilivu kabisa na mtu mwenye mawazo tofauti na yenu.

Ndio maana tunasema upinzani wa Tanzania sio wakuaminika kabisa maana waliopo humo hawana moral standards, ni wapiga kelele tu.
Mimi ni MTANZANIA, nafuatilia siasa bt Sina Chama chochote.

Niko NEUTRAL, CCM Leo imenifurahisha kuridhia mchakato wa KATIBA mpya uanze.

Bt CCM ikikosea nairudisha Kwa mstari, CDM vile vile.

Msisahau kuwa Vyama vyote Kwa ujumla havifikishi wanachama mil 10 bt TANZANIA tupo zaidi ya Mil 60.

Lipo kundi kubwa sana msisahau ni Watanzania, wanashiriki siasa bila kuwa na vyama. Amen
 
Katika Hali ambayo haikutarajiwa hasa na CCM wenyewe, Katibu wao mwenezi amejitokeza na kutangaza hadharani kuwa CCM wako tayari kendeleza mchakato wa Katiba Mpya.

Katika hafla Ile wengi walionekana kupigwa butwaa huku wakishangilia kwa shangilio feki.
 
Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kauli moja imekubaliana kuwa kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakubaliana na umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na hivyo kinaishauri serikali kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya kwa maslahi mapana ya Taifa na Maendeleo ya watanzania wote.
Pongezi kwa wote waliopiga kelele mpaka kelele zao zikasikika.
hii imenikumbusha migomo ya vyuoni kudai bumu litoke,Unashangaa kabla ya watu kugoma bumu lilikuwa
halitoki,wakigoma linatoka mpaka unajiuliza,kama tatizo lilikuwa ni ukosefu wa fedha
sasa fedha imetoka wapi baada ya wanachuo kugoma?

All in all nawapongeza halmashauri ya chama cha mapinduzi,kwa kuona nguvu ya hoja ya katiba mpya
 
Safi sana..haya ndio masuala ya kinchi..katiba mpya ni hitaji la wananchi.

Wapeni mwanachi katiba mpya...hizi kelele ziishe mbona simpo tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hivi mkuu unajua unachotafuta kwa maslahi ya taifa?
Inaonyesha pengine hujui unachotafuta , na hivyo utajikuta unapinga hadi mambo ya maana yenye maslahi ya taifa

Mambo gani yenye maslahi ya taifa? Au huko kuingizana mjini ndio maslahi ya taifa?
 
Back
Top Bottom