Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Status
Not open for further replies.
I see.......

Simba kweli raha.....Hongereni sana kwa ushindi huu......Coastal na Azam nao lazima wapate jkichapo kama hiki cha leo mlichoipa Yanga kwenye mechi hizi mbili zinazofuata
Haaaahaaaahhh Mkuu Balantanda heshima yako lakini. Ipi bora Yanga kuharibu kwa Toto au kuharibiwa na Simba ?!!
 
Last edited by a moderator:
sio mnaandika tu, hizo 3 za YANGA zimetoka wap? au zmeshushwa tu?

Simba kuzawazisha kumeniuma sana kama wewe ulivyoumia (pengine zaidi kwani mimi ni mwanachama na mnazi wa Jangwani kupitiliza).

Lakini kiukweli msimu huu Yanga wamekosa ile resilience ya timu inayosaka ubingwa (kumbuka mechi ya Azam). Msimu uliopita Yanga tulikuwa tuna-grind out results za 1-0 na tukachukua ubingwa.

Kwa mwenendo wa msimu huu, na kama hakutakuwa na mkakati wa mabadiliko - no hope! Sorry to disappoint you mwana-Yanga mwenzangu lakini it's a bitter fact!
 
Naona uliingia mitini mtani.......Shabiki lazima ukomae mwanzo mwisho.....

Mkuu, wanaojisifu wana timu mwaka huu ni Simba, kulikoni mkaruhusu bao 3 kipindi cha kwanza mtani?

Nimekuwepo online kuanzia tu JF ilivyorudi hewani hadi sasa, pamoja kutangulia kutufunga zile tatu nilikuwa natupia post za kihuzuni huzuni huwa sina kawaida ya kukimbia usiponiona ujue nimetingwa na majukumu lakini sio woga.
 
Sijakuelewa mkuu......Nieleweshe tafadhali (Kama hautojali)

By real sense kupigwa na ndugu yetu[azam au coastal union] ni kesi ndogo ukilinganisha na mlivyotaka kutufanyia. Vice versa is true too... Bora yanga ipigwe na Toto kuliko kupigwa na Simba. SIJUI NIMEELEKA Balantanda ?!
 
Last edited by a moderator:
ila yanga muache uchawi wa kufanya watu wazimie ili mpate magoli, kila akizimia mtu bao linaingia..
 
Ila wana Simba tusisherehekee tu ushindi wa leo tuliomfunga Yanga bali ni sahihi sasa wa kuwakumbusha wale vibosile wetu wa Msimbazi ile ahadi ya kununuwa kila goli kwa cash, ahadi ni deni. Wawape vijana mpunga wao.

Kweli kabisa. madogo wamepigana kiume. Madogo wamepambana kiume na litimu lenye wachezaji wakongwe wenye uzoefu wa kimataifa na yenye kocha wa "kimataifa" mwenye rangi nyeupe.
 
Hongereni sana kwa ushindi huu mtamu mkuu....

Ubingwa wenu mwaka huu mtani....
 
There are currently 1993 users browsing this thread. (176 members and 1817 guests:shocked🙂
 
By real sense kupigwa na ndugu yetu[azam au coastal union] ni kesi ndogo ukilinganisha na mlivyotaka kutufanyia. Vice versa is true too... Bora yanga ipigwe na Toto kuliko kupigwa na Simba. SIJUI NIMEELEKA Balantanda ?!
I see......

Kumbe Simba ni heri ifungwe na Azam ama Coastal kuliko kufungwa na Yanga!!....... Masuke upo?, msikilize mdau wako huyu.....

Una tofauti yoyote na mzee Ibrahim Akilimali wa Yanga?, ambaye anaamini Yanga kumfunga Simba ni sawa na kuchukua ubingwa....

Hongera sana kwa ushindi mkuu wangu, naona mmeshachukua ubingwa tayari.....

Simba hoyeeeeeeeeeeeee.....

Huo ujinga wa Yanga na Toto ulishaisha siku nyingi, siku hizi Yanga akikutana na Toto ni kazi mtindo mmoja, ndio maana kuna msimu Toto alimpiga Yanga na kumtibulia nafasi yake ya kutwaa Ubingwa....
 
Last edited by a moderator:
Hongereni sana kwa ushindi huu mtamu mkuu....

Ubingwa wenu mwaka huu mtani....

Mkuu msinune sana, mlitamani sana mtufunge mengi lakini ndo hivyo uwezo tuliodisplay kipindi cha pili pamoja na bahati ndo vimefanya matokeo yasomeke hivyo.
 

Hayo ni ya kwake aliyesema mimi hayanihusu, ningekuwa nimesema mimi ningekuwa tayari kuyatetea.
 
Hayo ni ya kwake aliyesema mimi hayanihusu, ningekuwa nimesema mimi ningekuwa tayari kuyatetea.
Hahaaaaaaaaaaaa.........

Sijamaanisha kwamba yanakuhusu mkuu wangu....

Nilitaka tu nikuoneshe aina ya wadau wa mpira tulionao Tanzania, watu wa aina ya Ibrahim Akilimali wa Yanga, ambao kwayo Yanga kumfunga Simba ni sawa na kutwaa ubingwa, wao ni heri Yanga akose ubingwa lakini amshinde Simba......

Ndio maana nimekuonesha huyo mdau wa Simba hapo juu ambaye anasema ni heri Simba ifungwe na Azam ama Coastal Union kuliko kufungwa na Yanga....

Niwie radhi kama nimekukwaza mtani....My bad
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…