Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Ali tuliishi mtaa mmoja wote tukiwa tunaishi kwenye government quarters kutokana na ajira za wazazi wetu. Kwao Ali walizaliwa saba na mama yao alikuwa Mama wa nyumbani tofauti na mama zetu waliotoka asubuhi kwenda kibarua ni. Tuliwaonea sana wivu wakina Ali kwa kushinda na mama yao siku nzima.
Siku moja tukiwa tunacheza chini ya mwembe dodo, mama Ali alimuita Alli ili atumwe. Alipewa hela aende Kinondoni gengeni akanunue mchele. Ali alikimbia haraka kwani alimiss kula wali. Kulikuwa na wingu nene la mvua limetanda. Ali alikimbia ili arudi mchele upikwe wale wali.
Baada ya kufungiwa mchele Ali alianza kukimbia. Kufika njiani mvua ilizidi na yeye aliongeza speed. Mpaka anafika nyumbani mfuko wa khaki uliofungiwa mchele ulishalowana kabisa na mchele umekwisha.
Ali alichapwa sana na mama yake. Hii story imenifundisha risk assessment katika kila jambo ninalotaka kulifanya.