Yaliyomkuta rafiki yangu Ali

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ali tuliishi mtaa mmoja wote tukiwa tunaishi kwenye government quarters kutokana na ajira za wazazi wetu. Kwao Ali walizaliwa saba na mama yao alikuwa Mama wa nyumbani tofauti na mama zetu waliotoka asubuhi kwenda kibarua ni. Tuliwaonea sana wivu wakina Ali kwa kushinda na mama yao siku nzima.

Siku moja tukiwa tunacheza chini ya mwembe dodo, mama Ali alimuita Alli ili atumwe. Alipewa hela aende Kinondoni gengeni akanunue mchele. Ali alikimbia haraka kwani alimiss kula wali. Kulikuwa na wingu nene la mvua limetanda. Ali alikimbia ili arudi mchele upikwe wale wali.

Baada ya kufungiwa mchele Ali alianza kukimbia. Kufika njiani mvua ilizidi na yeye aliongeza speed. Mpaka anafika nyumbani mfuko wa khaki uliofungiwa mchele ulishalowana kabisa na mchele umekwisha.

Ali alichapwa sana na mama yake. Hii story imenifundisha risk assessment katika kila jambo ninalotaka kulifanya.
 

Sa mimi ndio yule Ali. Nimekuwa sasa
 
Ali Ali Ali kavaa koti na msumari...
 
Acha Ali Ale Wali Bila Wali Ali Hali

Sawa Mama Ali Ali Risk Kumtuma Ali Mbali Kwa Ajili Wale Wali, Ila Kwa Mboko Alimuonea, Maana Ali Hakucheza Njiani, Mvua Hakuileta Yeye, Mfuko Wa Khaki Uliowekewa Mchele Hakuutengeneza Yeye. Wazazi Sometimes!
 
Wali ukijulikana kwa jina na cheka na watoto enzi hizo.
 
CC:-
Paul Makonda
 
Mke... tutakaokuelewa hapa ni wachache sana. Hivi yule mtoto wa malaika kashaanza kunyeshewa mvua akiwa na mchele? Nasikia kafanikiwa kuleta kiumbe... made in China, assembled at Muhimbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…