Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mkasa wa mfalme Abraha umetajwa ndani ya Qur'an suraul Fiil tukio lililotokea mwezi kama huu aliozaliwa mtume Muhammad swalaLlaahu alayhi wasaLlam.Na ndio mwezi huu huu Hamas walipofanya kile kilichoonekana hakiwezekani.
Abraha alikuwa ni mfalme wa Yemen ya sasa na alikuwa mkristo..Aliposikia kuna Alkaaba kule Makka ambako watu wanatoka miji ya jirani kwenda kuabudu. Na yeye akajenga kanisa kubwa na kuwataka watu wote waende kuabudu hapo badala ya Makka.Watu wengi wakakaidi na yeye akaamua kwenda kuivunja alkaaba iliyoasisiwa na mtume Ibrahim na mwanawe Ismajil alayhimaa salaam.
Akaondoka na jeshi bora la wakati huo lililokuwa likitumia tembo. Kwa jeuri kubwa na kujiamini akaelekea huko.Waarbu walipopata habari hizo wakaamua kwenda kujificha. Babu yake mtume Muhammad rehema na amani zimshukie ambaye alikuwa ndiye muangalizi wa nyumba hiyo akabaki kuomba dua ili Mwenyezi Mungu ailinde nyumba yake.Baada ya hapo na yeye akawafuata watu wake mafichoni.
Abraha hakujuwa kuwa msikiti ule ulikuwa na ulinzi imara wa jeshi lililoonekana. Walipokaribia eneo hilo wakaja ndege wadogo kila mmoja akiwa amebeba kijiwe chenye jina la anayekwenda kumpiga na hakikosei shabaha yake tofauti na droni za leo.vijiwe hivyo kutoka jahanamu vikawaangamiza wote wakawa kama majani yaliyoliwa na kutapikwa.Abraha mwenyewe na wenzake wachache akawachwa akiwa mnyonge kama ndege aliyeroweshwa na mvua asiyeweza kuruka anabaki akikutolea macho tu umhurumie.
Kwa jinsi Israel ilivyojisifia kwa ubora wa silaha zake haikutajiwa kuwa iko siku ingevamiwa na kupigwa na watu wenye silaha duni kama ilivyo kwa makundi ya wapalestina kule Gaza.
Kipigo hicho kimewashangaza hata wamarekani ambao ndio wafadhili wakubwa wa Israel.Kwa kuamini kwenye nguvu kubwa za kijeshi walizonazo na bila kujitafakari kilichowakuta iwapo ni wapalestina peke yao au ni nguvu tofauti wasiyoiona, Israel ikiongozwa na Netanyahu wameamua kuipiga Gaza na kuifanyia ukatili wa hali ya juu na katika tangazo la vita Benjamini Netanyahu amemaliza na kibwagizo kuwa tutashinda.
Benjamin Netanyahu hajui kuwa mwenye nguvu za kweli ni Allah aliyetukuka na ushindi wa uhakika ni wake. Kwa hali hiyo kuna dalili zote atakapoamua kufanya kibri zaidi inaweza ikawa ndio mwisho wake na mwisho wa taifa lake kwani Allah hashindwi na kuwageuzia meza ikawa kama yaliyolikuta jeshi la tembo na kamanda wao Abraha.