Yaliyompata mfalme Abraha yanamnyemelea Benjamin Netanyahu

Mkasa wa mfalme Abraha umetajwa ndani ya Qur'an suraul Fiil tukio lililotokea mwezi kama huu aliozaliwa mtume Muhammad swalaLlaahu alayhi wasaLlam.Na ndio mwezi huu huu Hamas walipofanya kile kilichoonekana hakiwezekani.

Abraha alikuwa ni mfalme wa Yemen ya sasa na alikuwa mkristo..Aliposikia kuna Alkaaba kule Makka ambako watu wanatoka miji ya jirani kwenda kuabudu. Na yeye akajenga kanisa kubwa na kuwataka watu wote waende kuabudu hapo badala ya Makka.Watu wengi wakakaidi na yeye akaamua kwenda kuivunja alkaaba iliyoasisiwa na mtume Ibrahim na mwanawe Ismajil alayhimaa salaam.

Akaondoka na jeshi bora la wakati huo lililokuwa likitumia tembo. Kwa jeuri kubwa na kujiamini akaelekea huko.Waarbu walipopata habari hizo wakaamua kwenda kujificha. Babu yake mtume Muhammad rehema na amani zimshukie ambaye alikuwa ndiye muangalizi wa nyumba hiyo akabaki kuomba dua ili Mwenyezi Mungu ailinde nyumba yake.Baada ya hapo na yeye akawafuata watu wake mafichoni.

Abraha hakujuwa kuwa msikiti ule ulikuwa na ulinzi imara wa jeshi lililoonekana. Walipokaribia eneo hilo wakaja ndege wadogo kila mmoja akiwa amebeba kijiwe chenye jina la anayekwenda kumpiga na hakikosei shabaha yake tofauti na droni za leo.vijiwe hivyo kutoka jahanamu vikawaangamiza wote wakawa kama majani yaliyoliwa na kutapikwa.Abraha mwenyewe na wenzake wachache akawachwa akiwa mnyonge kama ndege aliyeroweshwa na mvua asiyeweza kuruka anabaki akikutolea macho tu umhurumie.

Kwa jinsi Israel ilivyojisifia kwa ubora wa silaha zake haikutajiwa kuwa iko siku ingevamiwa na kupigwa na watu wenye silaha duni kama ilivyo kwa makundi ya wapalestina kule Gaza.

Kipigo hicho kimewashangaza hata wamarekani ambao ndio wafadhili wakubwa wa Israel.Kwa kuamini kwenye nguvu kubwa za kijeshi walizonazo na bila kujitafakari kilichowakuta iwapo ni wapalestina peke yao au ni nguvu tofauti wasiyoiona, Israel ikiongozwa na Netanyahu wameamua kuipiga Gaza na kuifanyia ukatili wa hali ya juu na katika tangazo la vita Benjamini Netanyahu amemaliza na kibwagizo kuwa tutashinda.

Benjamin Netanyahu hajui kuwa mwenye nguvu za kweli ni Allah aliyetukuka na ushindi wa uhakika ni wake. Kwa hali hiyo kuna dalili zote atakapoamua kufanya kibri zaidi inaweza ikawa ndio mwisho wake na mwisho wa taifa lake kwani Allah hashindwi na kuwageuzia meza ikawa kama yaliyolikuta jeshi la tembo na kamanda wao Abraha.
Ina maana Babu yake Mtume Muhammad (Na amani iwe juu yake) alikuwa Muislamu?

Si alikuwa mpagani?
 
Unajuwa Mwenyezi Mungu ana rehma kwa viumbe wake wote,waislamu na wasiokuwa waislamu. Kuna watu hurehemewa kwa ujinga wao na hupelekewa ujumbe ili wazinduke.Yule aliyepata ujumbe na akafanya kibri ndio huwa havumiliwi.

Abraha alijidai ni mkristo kwa maana anamjua Mungu lakini hakuishia hapo akataka awe Mungu mwenyewe na watu wafuate amri zake.

Alkaaba ilijengwa na waislamu na ni nyumba ya Mwenyezi Mungu.Abdulmutallib atakuwa alikuwa ni muislamu kwa vigezo vya muda ule.Na muhimu zaidi alikuwa akiilinda nyumba ya Mwenyezi Mungu.Hivyo kuadhibiwa Abraha kwa kutaka kuiharabu nyumba ya Mwenyezi Mungu ni jambo jepesi kufahamika.
 
Vijana wengi atujui dini uislamu wala ukristo tunafwata mihemko tu ya kidini
 
Mkasa wa mfalme Abraha umetajwa ndani ya Qur'an suraul Fiil tukio lililotokea mwezi kama huu aliozaliwa mtume Muhammad swalaLlaahu alayhi wasaLlam.Na ndio mwezi huu huu Hamas walipofanya kile kilichoonekana hakiwezekani.

Abraha alikuwa ni mfalme wa Yemen ya sasa na alikuwa mkristo..Aliposikia kuna Alkaaba kule Makka ambako watu wanatoka miji ya jirani kwenda kuabudu. Na yeye akajenga kanisa kubwa na kuwataka watu wote waende kuabudu hapo badala ya Makka.Watu wengi wakakaidi na yeye akaamua kwenda kuivunja alkaaba iliyoasisiwa na mtume Ibrahim na mwanawe Ismajil alayhimaa salaam.

Akaondoka na jeshi bora la wakati huo lililokuwa likitumia tembo. Kwa jeuri kubwa na kujiamini akaelekea huko.Waarbu walipopata habari hizo wakaamua kwenda kujificha. Babu yake mtume Muhammad rehema na amani zimshukie ambaye alikuwa ndiye muangalizi wa nyumba hiyo akabaki kuomba dua ili Mwenyezi Mungu ailinde nyumba yake.Baada ya hapo na yeye akawafuata watu wake mafichoni.

Abraha hakujuwa kuwa msikiti ule ulikuwa na ulinzi imara wa jeshi lililoonekana. Walipokaribia eneo hilo wakaja ndege wadogo kila mmoja akiwa amebeba kijiwe chenye jina la anayekwenda kumpiga na hakikosei shabaha yake tofauti na droni za leo.vijiwe hivyo kutoka jahanamu vikawaangamiza wote wakawa kama majani yaliyoliwa na kutapikwa.Abraha mwenyewe na wenzake wachache akawachwa akiwa mnyonge kama ndege aliyeroweshwa na mvua asiyeweza kuruka anabaki akikutolea macho tu umhurumie.

Kwa jinsi Israel ilivyojisifia kwa ubora wa silaha zake haikutajiwa kuwa iko siku ingevamiwa na kupigwa na watu wenye silaha duni kama ilivyo kwa makundi ya wapalestina kule Gaza.

Kipigo hicho kimewashangaza hata wamarekani ambao ndio wafadhili wakubwa wa Israel.Kwa kuamini kwenye nguvu kubwa za kijeshi walizonazo na bila kujitafakari kilichowakuta iwapo ni wapalestina peke yao au ni nguvu tofauti wasiyoiona, Israel ikiongozwa na Netanyahu wameamua kuipiga Gaza na kuifanyia ukatili wa hali ya juu na katika tangazo la vita Benjamini Netanyahu amemaliza na kibwagizo kuwa tutashinda.

Benjamin Netanyahu hajui kuwa mwenye nguvu za kweli ni Allah aliyetukuka na ushindi wa uhakika ni wake. Kwa hali hiyo kuna dalili zote atakapoamua kufanya kibri zaidi inaweza ikawa ndio mwisho wake na mwisho wa taifa lake kwani Allah hashindwi na kuwageuzia meza ikawa kama yaliyolikuta jeshi la tembo na kamanda wao Abraha.
Avaaye asijiisifu kama avuaye. Hamas hawana cha kujisifia kwa ukatili walioufanya.
 
Visa vilivyotajwa kwenye Qur'an sio muvi ni matukio ya uhakika tunayoletewa tupate mazingatio.
Sawa kwahiyo wale walivyowaua wenzao sawa.........wakirudishiwa sio sawa kweli??
 
Kwahiyo Allah ndio anaruhusu kuuawa watu wasio na hatia?mkijibiwa na Israel mnakuja kutafuta huruma eti ana Allah ana nguvu kwa hiyo anawatetea magaidi
Wanajihami kutokana na uvamizi kama anavyojihami ukrain
 
Hebu oneni mnavyopenda stories za kipuuzi, ndo maana hamuishi kukunyugwa hapo middle east kila siku. Umeleta stori ya kijinga sana isiyo na mantiki yoyote. Huo msikiti wa al haram hapo mecca watu walishauweka under siege kwa siku 14( 20/11-04/12/1979). Allah alikuwa ameenda likizo? Unahisi ni vindege vilivyobeba mawe ndo vilikuja kuukomboa? Acheni kuamini stories za kipuuzi. Saidianeni mkapigane na israel + USA ndugu zenu wanauliwa huko.
 
Mkasa wa mfalme Abraha umetajwa ndani ya Qur'an suraul Fiil tukio lililotokea mwezi kama huu aliozaliwa mtume Muhammad swalaLlaahu alayhi wasaLlam.Na ndio mwezi huu huu Hamas walipofanya kile kilichoonekana hakiwezekani.

Abraha alikuwa ni mfalme wa Yemen ya sasa na alikuwa mkristo..Aliposikia kuna Alkaaba kule Makka ambako watu wanatoka miji ya jirani kwenda kuabudu. Na yeye akajenga kanisa kubwa na kuwataka watu wote waende kuabudu hapo badala ya Makka.Watu wengi wakakaidi na yeye akaamua kwenda kuivunja alkaaba iliyoasisiwa na mtume Ibrahim na mwanawe Ismajil alayhimaa salaam.

Akaondoka na jeshi bora la wakati huo lililokuwa likitumia tembo. Kwa jeuri kubwa na kujiamini akaelekea huko.Waarbu walipopata habari hizo wakaamua kwenda kujificha. Babu yake mtume Muhammad rehema na amani zimshukie ambaye alikuwa ndiye muangalizi wa nyumba hiyo akabaki kuomba dua ili Mwenyezi Mungu ailinde nyumba yake.Baada ya hapo na yeye akawafuata watu wake mafichoni.

Abraha hakujuwa kuwa msikiti ule ulikuwa na ulinzi imara wa jeshi lililoonekana. Walipokaribia eneo hilo wakaja ndege wadogo kila mmoja akiwa amebeba kijiwe chenye jina la anayekwenda kumpiga na hakikosei shabaha yake tofauti na droni za leo.vijiwe hivyo kutoka jahanamu vikawaangamiza wote wakawa kama majani yaliyoliwa na kutapikwa.Abraha mwenyewe na wenzake wachache akawachwa akiwa mnyonge kama ndege aliyeroweshwa na mvua asiyeweza kuruka anabaki akikutolea macho tu umhurumie.

Kwa jinsi Israel ilivyojisifia kwa ubora wa silaha zake haikutajiwa kuwa iko siku ingevamiwa na kupigwa na watu wenye silaha duni kama ilivyo kwa makundi ya wapalestina kule Gaza.

Kipigo hicho kimewashangaza hata wamarekani ambao ndio wafadhili wakubwa wa Israel.Kwa kuamini kwenye nguvu kubwa za kijeshi walizonazo na bila kujitafakari kilichowakuta iwapo ni wapalestina peke yao au ni nguvu tofauti wasiyoiona, Israel ikiongozwa na Netanyahu wameamua kuipiga Gaza na kuifanyia ukatili wa hali ya juu na katika tangazo la vita Benjamini Netanyahu amemaliza na kibwagizo kuwa tutashinda.

Benjamin Netanyahu hajui kuwa mwenye nguvu za kweli ni Allah aliyetukuka na ushindi wa uhakika ni wake. Kwa hali hiyo kuna dalili zote atakapoamua kufanya kibri zaidi inaweza ikawa ndio mwisho wake na mwisho wa taifa lake kwani Allah hashindwi na kuwageuzia meza ikawa kama yaliyolikuta jeshi la tembo na kamanda wao Abraha.
Hivi kweli mtu mwenye akili timamu anaweza amini vitu vya hivi? Uislam umeundwa kwa kuchakachua yaliyo kwenye Torati, Biblia na kuongeza tamaduni za kiarabu na wivu mkubwa wa kimapenzi.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi nahisi Kuna mambo hayapo sawa kwenye historia.
Na nafikiria Kwa sasa Israel itaitwaa Gaza tena na kuwa Mali yake na huenda ikatwaa Westbank na kuwa yake,na huenda ikatwaa maeneo makubwa East bank na kuyafanya sehem yake ambapo "Hebron na Bethlehem" zitakuwa milki ya Israel.
Na Kwa hili,tusishangae msikiti WA Al Aqsa ukivunjwa na kujengwa hekalu la kiyahudi.
 
Hicho kitu hakitatokea kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Nabii Musa alayhi salaam aliletwa na miujiza wakati uchawi ulikuwa umeshamiri na kashinda mpaka wachawi wake wakamuasi.Nabii Muhammad aliletwa na kitu kama mashairi lakini sicho wakati Makka walikuwa wamebobea kwa lugha.
Hamas wapo bila silaha na teknolojia kubwa muda huu ambapo Israel inajivunia teknolojia na mabomu mazito.Yatakaposhindwa kuwazima Hamas ndipo mabadiliko makubwa ya kiimani yatakapoanza.
 
enjamin Netanyahu hajui kuwa mwenye nguvu za kweli ni Allah aliyetukuka na ushindi wa uhakika ni wake. Kwa hali hiyo kuna dalili zote atakapoamua kufanya kibri zaidi inaweza ikawa ndio mwisho wake na mwisho wa taifa lake kwani Allah hashindwi na kuwageuzia meza ikawa kama yaliyolikuta jeshi la tembo na kamanda wao Abraha.
Mleta mada unatuaminisha kuwa allah ndie kawatuma hawa hamas kuvamia raia na kuwaua bila kosa lolote?
Unatueleza kuwa huyu allah anawachukia waisrael kujilinda na kujibu uovu huu wa wapalestina?
 
Sio lengo langu kukuaminisha chochote.Nakupa dalili za uwezo mkubwa wa Allah akiamua kumsikiliza anayeonewa.Hakuna teknoloji wala nini inayofanya kazi.
Mimi mwenyewe ndio naamini na naona ishara kuwa kuna kitu kinakuja ulimwenguni kudhihirisha uwezo mkubwa wa Allah ambao kuna watu wengi wameanza kudharau uwepo wake na ahadi zake kwa kupimo cha maendeleo ya kiteknolojia na umiliki wa silaha za kuripuka na kuangamiza kitu kwa sekunde chache.
Kauli kama hizi za kibri cha Netanyahu na yale yanayosemwa na Marekani chukua dondoo huku ukiendelea kufuatilia huu mzozo.

Every Hamas member is a dead man, Netanyahu says

1697090318574.png
 
Attachments

  • 1697090318760.png
    1697090318760.png
    126.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom