Yaliyonikuta jana sitasahau.

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Jana kwangu nilikuwa nimetulia usiku saa 5,
Mara ghafla nikaskia mayowe kwa jirani, majirani wote tukatoka kwenda kumsaidia mwenzetu huku tukiwa tumejihami kwa mawe, marungu na mapanga.
Na tuliooingia kwake tulimkuta chatu mkubwa ajabu! Wakati tukitafakari jinsi ya kumuua usiku ule ..
Mara ghafla bin vuu umeme ukakata mtaa mzima!
Naomba malizia stori kwanza wakati mimi nafungwa bandeji hapa hospitali.
Sababu nimeshonwa nyuzi kumi kichwani!
Maana yake kila uliekuwa ukimgusa alikuwa anakufumua na kitu kizito na chenye ncha kali!
Hata sijui nilipigwa na nini??
😢 😢 😢
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…