Mr Devil
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 15,410
- 35,923
Watanzania bado tunaendelea kubeba maumivu ya yaliyotokea. Lakini kushindana na mwenye silaha hakutaleta suluhisho, bali Maumivu zaidi. Waliotenda mauaji walifanya hivyo si kwa uungwana wala kuzingatia utu na utanzania wetu, Hata hivyo kila jambo lina mwisho.
Maisha lazima yaendelee. Heshima na ushirikiano lazima ziendelee kwa Mheshimiwa Rais na serikali yake, kwani pambano limekwisha na hatuna budi kuendelea na maisha yetu ya kila siku.
Natoa ushauri kwa wananchi na vyombo vya dola:
Huu sio wakati wa kuanza kutafuta waandamanaji au kulipiza kisasi. Kitendo kama hicho kitaleta mpasuko na chuki zaidi. Hakuna haja ya haya yote. Badala yake, tuachane na chuki; serikali isahau, isamehe, na Watanzania waendelee na maisha kwa amani kwani ili ni doa tayari na hatuna budi kuacha yote yaliyo tufikisha hapa.
Mwisho, Tulinde Amani kwa wivu mkubwa mno na tuidumishe kwa pamoja. 🙏
MTANZANIA 🇹🇿